Je, mita za LUKU zinawasilianaje na server za TANESCO?


acha uongo hakuna cha camera wala bibi yake na camera na siku wakidanya hivyo tanesco watakuwa matajili sana..
 
mawasiliano yanapita kwenye nyaya hizo hizo za umeme.

Niliambiwa Tanesco wana uwezo wa kuwasiliana kupitia nyaya zao za umeme na ni kwa kasi na usikivu uliotulia.

Mawasiliano ya kutumia waya za grid yapo,wao wanaziita simu za carrieraa
 

kuna njia nyingi za kuchakachua,inategemea unatumia njia gani,kuna ya kiwaya,sumaku kwa meter za zamani na nyingine,mimi ninaye mtu namfahamu toka mwaka jana hadi leo luku yake inaunit 3 haipungui wala haizidi
 
Kweli jf member ni great thinker nimejifunza mengi sana.
 
So zile code unazopewa baada ya kununua units zinaenda kutafsiriwa na luku ni units ngapi, na si kwamba unapo ziingiza zile code zinatumwa Tanesco kuwa verfied
Kwamaana hiyo LUKU haiwasiliani na server za Tanesco

kipindi code zinakuwa.verified na luku,wapi inafanywa comparison ya hzo kodi??au unataka kusema luku zinakuwa na memory ambayo inakodi zote za tanesco?
 
Nadhani msingi wa swali upo hapo kwenye bold. Una maana kila kiasi cha units tunazonunua kina corresponding numeral arrangement?

sasa kama maelezo ndyo hayo,kutokana na mawazo yangu..wanataka kutuaminisha kwamba luku zinakuwa na memory{sijui GB ngapi} ambayo inakuwa na kodi namba zote za tanesco.Yaani inafanya konfirmation of code ili igenerate umeme,!na kitu hiko kwangu hakiingia akili hata kidogo
 
Kwanza mita za luku zinatofutina, zipo zilizoungwa na server i.e kwa wateja wakubwa na luku zilizo makumbani.Nafikiri wakati mita za luku zinasajiliwa na tanesco huwa zina unique key generator ambazo meter hiyo tu ndio itaweza kudekripti token ulizonunua. Hii inafanya token kuwa sahihi kwenye meter hiyo tu na si mita nyingine. Bila kumanisha zimeungwa na server. Ingalikua tofauti basi ungalinunua umeme kama ka vocha za voda.
 

Mkuu INSULIN, ni kweli kwamba mita za AMR (Automatic Meter Reader) zina chip kwa ajili ya mawasiliano.
Ninajiuliza, je inakuwaje kwa yule mtu aliye tamper mita, inawezekana akaonyeshwa LUKU meter purchase history kutoka kwa maafisa wa TANESCO kwa kutumia server; hii ni kuthibisha kuwa mita ilichezewa. Inawezekanaje kufahamu matumizi ya mteja ikiwa mita ya LUKU haina connection na server?
 
Last edited by a moderator:
wote mna bashiri na kubisha tu , MJIMPYA ..ANAVYOSEMA NI kweli kabisa unaponunua umeme kwa njia ya luku unauziwa umeme(token maalumu kwa ajili ya mita no husika)na ndio maana ni rahisi kwa tanesko kukata deni lao mita yako....zile token haziwezi kutumiwa na mita namba nyingine yoyote na mawasiliano kati ya mita na tanesco hawatumii netiwork nyingine yoyote zaidi ya nyaya zao....pia mawasiliano ya transforma shot..au tatizo lolote la kiufundi..hufanya mawasiliano au kujua tatizo lipo wapi kwa kupitia nyaya zao..ukibisha bado utauwa unabisha pasipo kukjua
 

hapo ktk red, nakupa pole sana.
 
Kama line zako ni 3 phase moja kwa moja wewe ni mtumiaji mkubwa lakini km single phase ujue upo kundi la pili.
 
Mie nadhani kila transaction inayofanyika ya kununua umeme unahusiana na Tanesco kwa namna moja au nyingine iwe ni wakala au kwa kutumia mobile phones maana verification ya kuwa mita no ni sahihi lazima ifanyike wakati unanunua na wakati una-recharge. Na kama walivyosema Sirs huku juu ni kweli kwa Tanesco wire data zinapita through na umeme na hii sio ngeni kwani kuna baadhi ya nyumba nishaingia nikakuta socket za ukutani zinakuwa controlled na pc wireless kwamba unaweza kuzima socket ya fridge ukiwa chumbani au ukizima umeme socket zote kwa kutumia pc na gadget moja inayochomekwa kwenye umeme.
 
Kwahiyo hitimisho ni Mita za LUKU hazina mawasiliano ya moja kwa moja na mitambo ya tanesco kwenye swala la kuverfy vocha
 

Unaandika kwa makini utadhani unasema ukweli !
Acha kudanganya na kupotosha watu.
Mita zinawasiliana na server za tanesco km ilivyo kwa mpesa, simbanking, paypoints nk.
Mawasiliano ni kupitia hizohizo nyaya za umeme.
Ndio maana wale wateja wapya huwa wanaenda tanesco ku activate mita zao kupitia computer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…