Gavinci
Member
- Mar 12, 2021
- 48
- 45
Habari wakuu, naombeni uzoefu wenu hasa kwenye sekta hii ya kuku wa mayai. Binafsi nimewahi kufuga kuku wa kienyeji, chotara, na broilers kwa uchache, ila kwa sasa nahitaji kufuga kuku wa mayai 600 hivyo ningependa kujua gharama zao hasa kwenye upande wa chakula, vifaranga na madawa tuu ukiacha gharama zingine kama banda na vifaa kama drinkers na feeders maana vipo. Bajeti niliyo nayo ni ml.8 naombeni muongozo wenu kama itatosha au kama haitoshi je inaweza angalau kutosha kuku wangapi wa mayai. Kimakazi naishi Tanga~Pande. Ahsanteni na karibuni kwa michango wakuu.