Binafsi sijawahi kuibiwa nawashangaa wanaolalamika
wengi wanalalamika kuibiwa kwasababu hapa bongo;
Pc nyingi zina windows ambazo ni pirated, yani za kudownload zilizochakachuliwa ambazo kuna nyingine zinaingizwa spyware, malware, miners, n.k ambazo zinanyonya data bila wewe kujua, ingia mfukoni utoe laki 3 upate window genuine
Pc nyingi zina softwares nazo zimechakachuliwa ivyo ivyo kama hizo window, mtu hata idm hawezi kununua.
Watu hawazimi updates, yani watu kibao hawajui haya mambo, mtu analalamika bando linaenda wakati hajaweka network yake iwe metred achilia mbali pc kuwa na rundo la software ambazo hazijazimwa automatic updates
Mtu anachomeka chomeka maflashi yenye virus wanaonyonya data wakati pc haina kinga ya antivirus
Watu hawazimi torrents, mwengine anachojua ni kudownload tu hajui kabisa kwamba torrent ikimaliza inaendelea kupandwa.
Kwa hio kabla ya kufungua bakuli hakikisha una windows orijino ya laki 3, softwares zako uwe umelipia mfano hii microsoft word ujichange laki 3, hakikisha pia umeweka bajeti ya anti virus kama kaspersky kila mwaka
, hakikisha unanunua movies zako achana na mambo ya torrents, movies nyingi ni kama elf 30 tu.