Sasa haya maswala ya Sheikh Yahya ,maanake utaweza vipi kutabiri wakati hatuna majina ya wanaotaka kugombea?..
Kifupi kama vyama vya Upinzani vitajipanga vizuri na kufikiria kwamba Ushindi mwaka huu 2010 haupo na hauwezi kupatikana isipokuwa ni mwaka wa JK kumalizia ngwe zake, basi ni bora wacheze kamali na kurudi majimboni. Wamtafute mgombea nje kabisa ya fikra zao za kisiasa!
Mbowe, Lipumba, Mrema, Cheyo hawa wote hawana haja wala sababu ya kugombea mwaka kesho kwa sababu Matokeo ya mwaka 2005 ni ushahidi tosha kwao kuwa hawawezi kumshinda JK...Hivyo baina yao kam akuna ushindani ni bora wasubiri wote mwaka 2015 warudishe majina yao kugombea na mtu mwingine wa CCM atakaye kuja.
wanachotakiwa kukifanya sasa hivi ni kumchagua mtu tofauti kabisa.. Kama Dr. Slaa au Mzanzibar anayekubalika kama Salim A Salim ambaye hapendwi na ASP na kajitoa ktk siasa meaning hayupo ktk Uongozi wa CCM Hivyo wanaweza kumvuta toka ktk retirement kwa kazi moja tu.. Kuidondosha CCM na Mtandao na kizuri zaidi ni kwamab yuko kati neutral siii Chadema, CUF, TLP wala NCCR...Wakisha mwondoa CCM mwaka 2010 then mwaka 2015 wanaweza jitenga tena kama ilivyokuwa Kenya kila mmoja wao arudi ktk mrengo anaukubali.. Thats the Only way ya kumshinda CCM.
Hapo naweza kuona ushindani kwa JK.. kwa hali ya leo kisiasa ni watu wawili tu wanaoweza kupambana na JK - Dr. Slaa na Salim.A. Salim kwa sababu hawa wagombea wawili wanakubalika hadi vijijini bila siasa na ahadi za uongo.