Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kwa mujibu wa imani ya kiislamu mtoto ambaye amezaliwa nje ya ndoa hatambuliki Kwa mujibu wa Sheria kama mtoto wa Baba husika.

Kwasababu kizazi au uzao WA familia unatakiwa upatikane ndani ya ndoa ya kisheria au ndoa iliyofungwa Kwa misingi ya Dini,na nje ya hapo huyo ni mtoto wa zinaa ambaye kisheria anatambulika kama mtoto wa mama aliye mzaa Tu.

Ingawa kikawaida atafahamika kama mtoto wa Baba Fulani lkn kidini huyo Baba hatambuliki na hivyo kuna haki Fulani ambazo Baba hawezi kumfanyia mtoto wake.

Moja wapo ni huyo mtoto hafai kuitwa Jina la ubini WA Baba yake,Hilo Jambo ni haramu Sana na Mungu ameshalikemea tayari, ingawa Kwa bahati mbaya Sana Kwa kutojua wengi wamewapa majina ya ubini wao hao watoto wa nje ya ndoa.

Na lingine ni kumuozesha kwenye ndoa, Baba Hana haki ya kumuozesha binti yake WA nje ya ndoa Kwa mumewe kwani ndoa hiyo ni batili na haifai kabisa.

Lingine huyo mtoto hawezi kumrithi Baba yake kwasababu kisheria huyo mtoto sio WA huyo Baba,Bali Baba anaweza kumpa sehemu ya Mali huyo mtoto,lkn mara Tu huyo Baba anapokufa basi huyo mtoto Hana haki ya Kurithi chochote.

Lakini sio vibaya huyo Baba kumhudumia huyo kijana Kwa malezi na mahitaji mbali mbali maadam Tu yeye ndiye sababu ya kuja Hicho kiumbe hapa duniani.

Na mtoto ambaye Hana Baba kisheria anaweza kuitwa Kwa jina la mama yake, Kwa mfano ETUGRUL BEY ASHA au Kwa jina la ubini Kwa upande wa mama yake.

Kubwa ni kutambua uzao mzuri ambao hata kizazi chako kinaweza pata haki stahiki ni kizazi ambacho kinatokana na ndoa takatifu ambayo IPO Kwa mujibu wa Sheria.

Na hata wale ambao wanafunga ndoa za kiserikali basi watambue kidini Hicho kizazi Chao hakitambuliki na Sheria za Dini Kwa maana Baba Hana watoto hapo Ila watoto ni WA mama.

Ni hayo Tu!

Kazakh destroyer
Msonjo
Nurain
adriz
professional Driver
baby zu
 
Hizi dini za kuletewa hizi zinavioja Sana. Mungu mlikutana nae wapi akayasema yote hayo? Au utashi wa binadamu ndio umepelekea kuyaandika hayo? Labda tuwaulize Ismail ni mtoto wa nani? Maana Abraham alimpata nje ya ndoa.

Masuala ya kusema ndoa ya kanisani au msikitini ni halali na nje ya hapo ni haramu yanaudhi Sana. Yaani mwanangu asirithi Mali au asitumie jina langu kisa dini! Basi Bora niachane na hiyo dini kuliko kupoteza uhusiano wa damu baina yangu na mtoto.

Jambo la kushangaza mtoto huyo huyo anakua na majina meeengi ya kumlaani. Lakini iwapo mama yake ukafunga nae tu ndoa japo Kwa kuchelewa yanabadilika. Kwahiyo kumbe shida sio mtoto Bali mnataka mwenye mtoto afunge ndoa na baba wa mtoto bila kujali ni mke wa pili, tatu au nne Sasa ndio Nini?

Waliowaletea dini wenyewe juzi wametengua kauli inayosema kuishi bila ndoa ni haramu na adhabu yake ni kifo. Walitengua Ili Ronaldo na mchumba wake waendelee na maisha, je nao waliambiwa na Mungu kuwa iwapo mtu ni maarufu Sheria haimhusu? Na wewe ambae upo kwenye familia ya kindoa utasema maneno hayo hayo iwapo mama Yako akisema huyo sio baba Yako? Muache kukalili na kuita binadamu wenzenu majina mabaya.

Kanuni zenu hizo hizo zimepelekea mabinti wengi kupoteza Malinda kabla ya ndoa Kwa hofu ya kupoteza bikra kabla ya ndoa au kuzaa kabla ya ndoa. Sasa unakua unafanya Nini Kama mtu unahofia kuchepuka Ili usizae haramu badala yake unatindua Malinda ya watoto wakiume Ili kutimiza haja zako? Na kanda zenye watu Kama nyinyi magasho wengi kwasababu ya hofu ya kuzaa nje kwahiyo mnaona Bora kujipooza huko .
 
Hizi dini za kuletewa hizi zinavioja Sana. Mungu mlikutana nae wapi akayasema yote hayo? Au utashi wa binadamu ndio umepelekea kuyaandika hayo? Labda tuwaulize Ismail ni mtoto wa nani? Maana Abraham alimpata nje ya ndoa...
Pole Sana mkuu ndio Hali halisi kwa Sisi ambao tutafuata misingi ya Dini zetu
 
Hizi dini za kuletewa hizi zinavioja Sana. Mungu mlikutana nae wapi akayasema yote hayo? Au utashi wa binadamu ndio umepelekea kuyaandika hayo? Labda tuwaulize Ismail ni mtoto wa nani? Maana Abraham alimpata nje ya ndoa...
Tatizo mtazamo wako hauwezi kubadilisha ukweli.

Kuna watu hawa kubaliani na utawala wa Samia lakini hilo haliondoi ukweli kuwa ndo kiongozi wa nchi hii.

Kitu chochote kinacho patikana nje ya utaratibu ulio wekwa na mungu aliye kuumba ni haramu.
 
Swadakta mkuu
 
Mungu hajawahi kuweka utaratibu wowote na popote zaidi ya binadamu wenye roho mbaya kusingizia Mungu. Kila kitu Cha ovyo hufanyika Kwa kigezo Cha Mungu, Mauaji ya kujitoa mhanga(MUNGU).
 
Mungu hajawahi kuweka utaratibu wowote na popote zaidi ya binadamu wenye roho mbaya kusingizia Mungu. Kila kitu Cha ovyo hufanyika Kwa kigezo Cha Mungu, Mauaji ya kujitoa mhanga(MUNGU).
Kwa hiyo mungu kukataza uzinzi ni hiyo ni roho mbaya?

Kwa hiyo binti yako huyo unaye mlea ukija kugundua kuwa ndo kipozeo cha nyege za vijana hapo mitaani kwako utamuita umpongeze?

Mungu kuja kukataza kitu ujue kina madhara, uzinzi umeshababisha matatizo makubwa ndani ya jamii.
 
Swadakta mkuu yaani unatembea mule mule
 
Kwa hiyo mungu kukataza uzinzi ni hiyo ni roho mbaya?
Kwa hiyo binti yako huyo unaye mlea ukija kugundua kuwa ndo kipozeo cha nyege za vijana hapo mitaani kwako utamuita umpongeze?
Mungu kuja kukataza kitu ujue kina madhara, uzinzi umeshababisha matatizo makubwa ndani ya jamii.
Ngoja niachane na huu mjadala lakini Mimi nitabaki na kile ninachokiamini kuwa ni sahihi. masuala ya Mungu kasema huku tunawatesa wengine siwezi kuunga mkono.
 
Hizi dini bwana.
Ommy dimpos kawa tajiri baba na ndugu wanajipendekeza kumjua mtoto wao mlikuwa wapi na dini zenu.

Domo leo ni tajiri kila ndugu na masheik mnajazana kwake mlikuwa wapi pindi maskini.
Hayo ni mapungufu Yao kama wazazi wake, lakini ukweli utabakia pale pale kuwa huyo ni mtoto wa mama kama ni kweli hakuzaliwa ndani ya ndoa

Kwahiyo mama ndo ana haki zote
 
Back
Top Bottom