Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Sijui kama nimekuelewa vizur au laa

Zinapokuja Sheria za Mungu hatuna mamlaka ya kusema ni za zamani au laa, kwakuwa haijasemwa zinatumika Kwa kipindi Fulani Tu?

Tunachoweza kubadili na kuweka kifungu kingine ni Sheria zetu wanadamu kama katiba na Sheria zetu ndogo ndogo tulizo jitungia wenyewe.

Na

Katika Uislamu tangu awali hakuna dhambi ya Baba kweenda Kwa mtoto au hakuna dhambi ya kurithi
Ndio maana nimesema haujaleta Swali bali Maelezo... (kwa Imani yako uliyoyaeleza ni sawa) ila kwa kidunia na kwa macho ya mlengwa (huyo mtoto) sio sawa hata kidogo Hapo Kale watu walipata shida sana za kutetwa, kutengwa na kutokupewa wadhifa wowote popote pale sababu walionekana kama Haramu / Bastards... Hio si sawa kwa Bin Adamu mmoja kumtendea mwingine..., ingawa kwa imani yako ni sawa na nitakuwa chizi kukubishia imani yako.....
 
Ngoja nikuelimishe kidogo kila unachokiona duniani kiko chini ya under control hata ww uko chini ya under control.

Mwenyezi mungu kaumba binadamu na kamuwekea na taratibu maalumu ni namna gani aendeshe maisha yake na sio ilimradi tu anaishi.

Mfano leo ww utatafuta pesa kwa nguvu zako utanunua gari lakini hiyo gari huwezi kuiendesha barabarani mpaka upitie utaratibu fulani licha ya kwamba hakuna aliye kusaidia kununua hilo gari.

Au ukitaka kufungua biashara utatakiwa ufuate utaratibu maalumu licha ya sio kufungua kiholela holela.

Hivyo hivyo kwa mungu alikuumba akasema nendeni mkaijaze dunia lakini kaweka utaratibu wa kuzaliana na sio kuzaliana kiholela holela.

Dawa ya kuhepusha haya sio kuukimbia ukweli bali ni sisi kuacha uzinzi wa kiholela, hakika ni ukatiri na ubinafisi mkubwa kwa mwanaume kumpa binti wa watu mimba hali ya kuwa huna mipango ya kumuoa.

Sawa kwanini adhabu apewe huyo mwanamke na mtoto tu? Maana hiyo zinaa hajafanya peke yake
 
Kwa mujibu wa imani ya kiislamu mtoto ambaye amezaliwa nje ya ndoa hatambuliki Kwa mujibu wa Sheria kama mtoto wa Baba husika.

Kwasababu kizazi au uzao WA familia unatakiwa upatikane ndani ya ndoa ya kisheria au ndoa iliyofungwa Kwa misingi ya Dini,na nje ya hapo huyo ni mtoto wa zinaa ambaye kisheria anatambulika kama mtoto wa mama aliye mzaa Tu.

Ingawa kikawaida atafahamika kama mtoto wa Baba Fulani lkn kidini huyo Baba hatambuliki na hivyo kuna haki Fulani ambazo Baba hawezi kumfanyia mtoto wake.

Moja wapo ni huyo mtoto hafai kuitwa Jina la ubini WA Baba yake,Hilo Jambo ni haramu Sana na Mungu ameshalikemea tayari, ingawa Kwa bahati mbaya Sana Kwa kutojua wengi wamewapa majina ya ubini wao hao watoto wa nje ya ndoa.

Na lingine ni kumuozesha kwenye ndoa, Baba Hana haki ya kumuozesha binti yake WA nje ya ndoa Kwa mumewe kwani ndoa hiyo ni batili na haifai kabisa.

Lingine huyo mtoto hawezi kumrithi Baba yake kwasababu kisheria huyo mtoto sio WA huyo Baba,Bali Baba anaweza kumpa sehemu ya Mali huyo mtoto,lkn mara Tu huyo Baba anapokufa basi huyo mtoto Hana haki ya Kurithi chochote.

Lakini sio vibaya huyo Baba kumhudumia huyo kijana Kwa malezi na mahitaji mbali mbali maadam Tu yeye ndiye sababu ya kuja Hicho kiumbe hapa duniani.

Na mtoto ambaye Hana Baba kisheria anaweza kuitwa Kwa jina la mama yake, Kwa mfano ETUGRUL BEY ASHA au Kwa jina la ubini Kwa upande wa mama yake.

Kubwa ni kutambua uzao mzuri ambao hata kizazi chako kinaweza pata haki stahiki ni kizazi ambacho kinatokana na ndoa takatifu ambayo IPO Kwa mujibu wa Sheria.

Na hata wale ambao wanafunga ndoa za kiserikali basi watambue kidini Hicho kizazi Chao hakitambuliki na Sheria za Dini Kwa maana Baba Hana watoto hapo Ila watoto ni WA mama.

Ni hayo Tu!

Kazakh destroyer
Msonjo
Nurain
adriz
professional Driver
baby zu
Nje ya ndoa ndio wapi?
 
Kwa hiyo mungu kukataza uzinzi ni hiyo ni roho mbaya?
Kwa hiyo binti yako huyo unaye mlea ukija kugundua kuwa ndo kipozeo cha nyege za vijana hapo mitaani kwako utamuita umpongeze?
Mungu kuja kukataza kitu ujue kina madhara, uzinzi umeshababisha matatizo makubwa ndani ya jamii.
Hivi vilivyomo ndani ya binadam viliumbwa na Mani?
 
Ndio maana nimesema haujaleta Swali bali Maelezo... (kwa Imani yako uliyoyaeleza ni sawa) ila kwa kidunia na kwa macho ya mlengwa (huyo mtoto sio sawa hata kidogo) Hapo Kale watu walipata shida sana za kutetwa, kutengwa na kutokupewa wadhifa wowote popote pale sababu walionekana kama Haramu / Bastards... Hio si sawa kwa Bin Adamu mmoja kumtendea mwingine..., ingawa kwa imani yako ni sawa na nitakuwa chizi kukubishia imani yako.....
Kuhusu swali katika mada yangu bilashaka halikuwa swali kama swali hasa Ila Ila namna ya kuileta mada husika au kuiweka mada husika.

Nashukuru kwamba umekiri Kwa mujibu wa Imani ni Sawa na hauna haki ya kuhoji Hilo

Ila

Umekiri Kwa Maisha ya duniani ya kawaida ni mtihani na changamoto,nami sipingani na wewe hata kidogo juu ya hilo
 
Ukitaka kuhoji hayo basi itabidi uanze kuhoji je uzao kutoka Kwa adam ilikuwaje kuwaje

Nadhan unatambua wale watoto ilibidi watembee na madada zao ili kizazi kiongozeke, je hapo utasemaje?
Mkuu ni wapi ulisikia watoto wa adammu walizaa na dada zao?. Adamu alipata watoto watatu tu wote wa kiume inamaanisha kulikuwa na jamii nyingine tofauti na mwanzo wa uzao wa adamu.
 
Kuhusu swali katika mada yangu bilashaka halikuwa swali kama swali hasa Ila Ila namna ya kuileta mada husika au kuiweka mada husika.

Nashukuru kwamba umekiri Kwa mujibu wa Imani ni Sawa na hauna haki ya kuhoji Hilo

Ila

Umekiri Kwa Maisha ya duniani ya kawaida ni mtihani na changamoto,nami sipingani na wewe hata kidogo juu ya hilo

Open your mind,usiwe limited nanaamni Mungu amekupa ubongo wa kureason so kujificha kwenye mlango wa maandiko sio sawa
 
mtoto hapo adhabu yake ni hipi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
msababishi mkubwa wa zinaa ni mwanamke,ajabu watu wengi awajui nini maana ya neno bdoa wengine wanajua ila wapinga kwa kusukumwa na chuki ya ushenzi walio nao hata mila zinapinga kujitwalia mtoto wamtu bila talatibu za mila husika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hili la kubagua watoto limeongeza ukatili katika jamii kwa asilimia nyingi mno.
Hapa swala ni watu kubadilika na kuacha kuzaa ovyo kama wanyama nje ya utaratibu

Tukikubali ukweli huu tutabadilika na huo ndio msingi wa maagizo na Sheria za Mungu
 
Open your mind,usiwe limited nanaamni Mungu amekupa ubongo wa kureason so kujificha kwenye mlango wa maandiko sio sawa
Mkuu kuna mambo ya kureason lkn zinapokuja Sheria za Mola wako aliyekuumba wewe na Mimi huna haki ya kuleta maoni yako
 
msababishi mkubwa wa zinaa ni mwanamke,ajabu watu wengi awajui nini maana ya neno bdoa wengine wanajua ila wapinga kwa kusukumwa na chuki ya ushenzi walio nao hata mila zinapinga kujitwalia mtoto wamtu bila talatibu za mila husika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Mmekaa kikandamizi sana,ona lawama zote mnamsukumizia mwanamke…Hata katika mahusiano ya mapenzi kawaida nani huwa initiator kama sio mwanaume? Sasa mwanamke anakujaje hapo?ok sawa na je waliobakwa? Wao ndo wamesababisha?
 
Back
Top Bottom