Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Ubin WA Ibrahim
Huyo si mtoto wa kijakazi na umesema kuwa uislam unaharamisha mtoto wa nje kuitwa ubin wa baba yake?

Wote tunajua mke halali wa Ibrahimu ni Sara na Hajiri alikuwa kijakazi au dada wa kazi
 
Dini inawatambua kama haramu…sasa yanini kujipendekeza kwa watu wasiokuona wathamani?
Chief hapa kuna uelewa mbaya Sana juu ya hawa watoto

Kitendo cha kupatikana kwao ndio haramu Ila wao kama sio haramu

Ni watoto ambao hawana makosa wala dhambi yoyote Ile,wenye kubeba hiyo dhambi ni wazazi wake.

Qur'an inasemaje kuhusu dhambi?

"Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana."

6:164
 
Huyo si mtoto wa kijakazi na umesema kuwa uislam unaharamisha mtoto wa nje kuitwa ubin wa baba yake?

Wote tunajua mke halali wa Ibrahimu ni Sara na Hajiri alikuwa kijakazi au dada wa kazi
Nilikuwa nakusubir Kwanza ucheke hlf nilijua utakuja Tu

Chief Manabii na Mitume walipewa privilege ambazo Mimi na wewe hatuna,kwahiyo kwao wao ilikuwa ni sahihi na hakuna ubaya wowote na hata hiyo sheria ilikuwa bado haijaletwa

Karibu sana
 
Wenye dini hiyo ndo hao hao waliomtambua Ismail kuwa mtoto halali wa Ibrahimu. Watoto wote wana haki ya kupata ubini wa baba, kuwajua wazazi wake wote wa kibaolojia pamoja na kuwajua ndugu zake wote. Period.
 
Mkuu mimi sio mpenzi wa mabishano ila ninachokijua ni kuwa Mungu alikuwepo kabla ya ujio wa hizi dini na ninachoamini ni kuwa kuwa mtu wa Mungu ni matendo mema na kuamini uwepo wake.

Hivyo dini ni sehemu tu ya kutafuta njia sahihi ya kumjua/ kumfuata Mungu. Kwa hiyo hata bila dini mwanadamu anayetenda mema na kumtegemea Mungu katika maisha yake huyo ni mtu wa Mungu. La sivyo kusingekuwepo dini nyingi na bado zote zikajinadi kuwa ndio zilizo sahihi.
 
Wenye dini hiyo ndo hao hao waliomtambua Ismail kuwa mtoto halali wa Ibrahimu. Watoto wote wana haki ya kupata ubini wa baba, kuwajua wazazi wake wote wa kibaolojia pamoja na kuwajua ndugu zake wote. Period.
Sawa period Kwako wewe chief

Sheria ya mwisho ambayo ndio Qur'an kuletwa hapa duniani imesema hivyo sasa sijui Mimi na wewe tuna haki gani ya kuipinga
 
Sawa nimekuelewa vizur Sana, je point yako ni ipi katika hili swala

Au

Wewe umeongea general Tu,kama ni general hakuna shida
 
Kwa ufupi hamna mtoto haramu wala wa nje. wote ni watoto kama ilivyo kwa PERESI (Babu wa Daudi), Suleiman (toka kwa mke wa Uria), Ismail-toka kwa hajira, Yesu-toka kwa baba anayemjua Mariamu n.k
 
Kwa ufupi hamna mtoto haramu wala wa nje. wote ni watoto kama ilivyo kwa PERESI (Babu wa Daudi), Suleiman (toka kwa mke wa Uria), Ismail-toka kwa hajira, Yesu-toka kwa baba anayemjua Mariamu n.k
Kwanza nikuwepe Sawa hakuna mtoto wa haramu Sawa?

Uharamu ni zinaa iliyofanywa na hao wazazi, Yule atabakia kuwa mtoto Safi Bila shida yoyote Ile.

Hapa naweza mzungumzia Yesu hakuwa na Baba ndio maana akaitwa Kwa ubini WA mama yake.

Chief hapa hatubishani na Mimi sio mpenzi WA mabishano, kwahiyo upo huru kuamini unachoamini
 
Takataka
 
Asante kwa kunisubiri sasa niambie ni wapi manabii walipewa hiyo privilege na ni wapi watoto "wa nje" wameharamishwa kutumia majiba ya baba zao
 
Katika haya tunajifunza nini?

Tuache kuzaa ovyo nje ya ndoa,Sisi sio wanyama,tulipoambiwa tuje kuijaza dunia tulitakiwa tufuate utaratibu maalum ambao ndio hadhi ya mwanadamu inapatikana hapo nayo ni NDOA.

Kwahiyo tusitafute sababu ambazo hazina msingi wowote ili mradi tuhalalishe maovu yetu.

Tubadilike guys.
 
Asante kwa kunisubiri sasa niambie ni wapi manabii walipewa hiyo privilege na ni wapi watoto "wa nje" wameharamishwa kutumia majiba ya baba zao
Katika Qur'an watoto wa nje ya ndoa wameharamishwa kuitwa majina ya Baba zao

Kwa asili kitu chochote ni halali mpaka kiharamishwe,kwahiyo maadam enzi za Manabii na Mitume hakukuwa na hizo sheria basi ilikuwa ni halali.
 
Kwenye hio Qur'an nani aliharamisha? Dini iliyotokana na ukoo wa mtoto wa kambo leo inakataa asili yake 🤣🤣🤣🤣
 
Kwenye hio Qur'an nani aliharamisha? Dini iliyotokana na ukoo wa mtoto wa kambo leo inakataa asili yake 🤣🤣🤣🤣
Naona unajitekenya mwenyewe halafu unacheka chief.

Asili gani iliyokatiliwa,kama wewe hutaki kuelewa hoja yangu basi endelea kuamini kile unachoamini

Shukrani
 
Naona unajitekenya mwenyewe halafu unacheka chief.

Asili gani iliyokatiliwa,kama wewe hutaki kuelewa hoja yangu basi endelea kuamini kile unachoamini

Shukrani
Kama tunaamini kuwa Ishmael ambaye ni mototo wa kambo kaanzisha uislam vipi mnakuja na vijisheria vya kukataa asili yenu
 
Kama tunaamini kuwa Ishmael ambaye ni mototo wa kambo kaanzisha uislam vipi mnakuja na vijisheria vya kukataa asili yenu
Unahakika Uislamu ulianza na Ismail?

Mkuu naomba uwe na siku njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…