Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
- Thread starter
- #181
Sina akili chief
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sina akili chief
Kwa hiyo unahalalisha ngono na watu kuzaa kiholela? Huoni kama hizo kanuni zimepunguza watoto wa mitaani kwa kiasi flani?Hizi dini za kuletewa hizi zinavioja Sana. Mungu mlikutana nae wapi akayasema yote hayo? Au utashi wa binadamu ndio umepelekea kuyaandika hayo? Labda tuwaulize Ismail ni mtoto wa nani? Maana Abraham alimpata nje ya ndoa.
Masuala ya kusema ndoa ya kanisani au msikitini ni halali na nje ya hapo ni haramu yanaudhi Sana. Yaani mwanangu asirithi Mali au asitumie jina langu kisa dini! Basi Bora niachane na hiyo dini kuliko kupoteza uhusiano wa damu baina yangu na mtoto.
Jambo la kushangaza mtoto huyo huyo anakua na majina meeengi ya kumlaani. Lakini iwapo mama yake ukafunga nae tu ndoa japo Kwa kuchelewa yanabadilika. Kwahiyo kumbe shida sio mtoto Bali mnataka mwenye mtoto afunge ndoa na baba wa mtoto bila kujali ni mke wa pili, tatu au nne Sasa ndio Nini?
Waliowaletea dini wenyewe juzi wametengua kauli inayosema kuishi bila ndoa ni haramu na adhabu yake ni kifo. Walitengua Ili Ronaldo na mchumba wake waendelee na maisha, je nao waliambiwa na Mungu kuwa iwapo mtu ni maarufu Sheria haimhusu? Na wewe ambae upo kwenye familia ya kindoa utasema maneno hayo hayo iwapo mama Yako akisema huyo sio baba Yako? Muache kukalili na kuita binadamu wenzenu majina mabaya.
Kanuni zenu hizo hizo zimepelekea mabinti wengi kupoteza Malinda kabla ya ndoa Kwa hofu ya kupoteza bikra kabla ya ndoa au kuzaa kabla ya ndoa. Sasa unakua unafanya Nini Kama mtu unahofia kuchepuka Ili usizae haramu badala yake unatindua Malinda ya watoto wakiume wa madrasa Ili kutimiza haja zako? Na kanda zenye watu Kama nyinyi magasho wengi kwasababu ya hofu ya kuzaa nje kwahiyo mnaona Bora kujipooza huko .
Reason inatumika pote maana mwanadamu anao utashi. Kwa hiyo ukiambiwa kitu na mtu mwingine unareason halafu unaamua kukikubali au kukataa.Kuna mambo ambayo yapo wazi kabisa hauhitaji kureason, je kwa mfano kumuabudu Mungu unahitaji kureason?
Kufuata sheria mathalani usizini,usiue au kuiba je unahitaji kureason?
Mungu kuuwawa na watu wake hapo utahitaji reason,Mungu kuwa na mtoto hapo utahitaji kureason
Chief tumepokea maoni yakoLinapokuja suala la kutumia utashi binafsi hawa jamaa waislam na wakristo hawa jamaa ni wapuuzi
Chief bakia na mantiki zako na utashi wakoI only appeal to sense.
Je hayo uliyoandika kwako binafsi yanakujakuja kuwa ni sahihi.
Kimantiki, kibaiolojia huyo ni mtoto wa huyo baba na ndio ukweli. Sasa kikija chanzo kingine au mamlaka nyingine ikasema kinyume na hivyo kimantiki inakuwa inasema uongo(kinyume na ukweli).
Ukweli siku zote haupingani na ukweli bali unajaziaga nyama tu. Maana ukweli ni mmoja. Tafakari. Chukua hatua ...
Naona mtoto haramu unavyo panikiUkitaka kujuwa dini ni Utapeli waulize pesa imeumbwa na Mungu au binadamu?
Wakikujibu ni binadamu Sasa wahoji ni kwa nini Mungu huyu huyu anataka pesa za binadamu atolewe sadaka?
Na kwenye Utapeli huo dini zote hazipingani wanataka sadaka na fungi la 10.
Yani Mungu eti naye anamuomba binadamu commission ya pesa. Vichekesho haviishi ujinga mtupu.
Kwahiyo point yako ni nini chief?Namaanisha kuna version za mitazamo Africa ilikuwa Mungu yuleyule wa Jana Leo na kesho hata bila uwepo wa Biblia ya Leo, Wala ukristo na uislam
Kuna miungu mingi sana duniani, au hujui hilo? Au unafikiri mungu ni Alah peke yake?Kwahiyo wadiz unataka kusema kuna Mungu wa Africa na Ulaya?
Anyways linapokuja swala la Imani ni kubwa Sana na very complicated lakini naheshimu maoni yako brother
Katika Dini ambazo zimewapa haki wanawake basi ni Uislamu.Hili li dini linakandamiza wanawake
Huyo Mungu unayedai amekuambia Umtenge mwanao wa damu, amewahi kukuambia wewe hayo maneno AU ni umesoma na kukariri maandiko yaliyoandikwa na waarabu ambao walidai yanatoka kwa mungu???!!Kuna mambo ambayo yapo wazi kabisa hauhitaji kureason, je kwa mfano kumuabudu Mungu unahitaji kureason?
Kufuata sheria mathalani usizini,usiue au kuiba je unahitaji kureason?
Mungu kuuwawa na watu wake hapo utahitaji reason,Mungu kuwa na mtoto hapo utahitaji kureason
Afadhali madam nawe umeliona hiliKwa hiyo unahalalisha ngono na watu kuzaa kiholela? Huoni kama hizo kanuni zimepunguza watoto wa mitaani kwa kiasi flani?
Wengi wanaotetea kuzaa nje ni mabingwa wa kuzalisha nje
Nimepokea maoni yakoReason inatumika pote maana mwanadamu anao utashi. Kwa hiyo ukiambiwa kitu na mtu mwingine unareason halafu unaamua kukikubali au kukataa.
Mungu akishuka analingania ukweli, kwa hiyo hata ukireason kiusahihi utakubali tu. Ukweli huwa hauumizwi na maswali au reason. Kinachoumiaga huwa ni uongo.
Sasaa hizi sheria zote, na maneno yote yanayosemwa kuwa ni ya Mungu ni lazima tunayasikia kupitia kwa wanadamu (mitume, manabii, vitabu) ndio maana lazima tureason na sisi.
Kama una njia ya kuongea na Mungu mojakwamoja hakuna haja ya reason maana utapokea pure madini.
Mtoto wa nje ya ndoa ni haramu kwenye Ukristo?Mtoto wote walio zaliwa nje ya ndoa ni haramu kwa mujibu wa dini zote kuanzia Ukristo, Uislamu, na hata uyahudi usitake kujifariji hapa.
Tena mayahudi linapo kuja suala la kuzaa nje ya ndoa ni wakali mno na wakigundua wanakutenga.
Mkuu Mungu ni mmoja Tu naye ni Allah,Mitume wote tangu Zama na zama walikuja kumlingania Mungu mmoja Tu basi.Kuna miungu mingi sana duniani, au hujui hilo? Au unafikiri mungu ni Alah peke yake?
Wachina hawamuamini Alah wako, wao wana mungu wao budha na wanamuamini.
Wakristo Mungu wao anaitwa Jehovah ni tofauti na mungu wako anayeitwa Alah.
Wewe mungu wako wa Uarabuni amekuambia Umtenge mtoto wa damu yako kwa sababu umemzaa nje ya ndoa...
Mungu wa wazungu (Mungu wa Israel) yeye hajatoa maagizo ya aina hiyo... Kila mtoto ni mtoto na anastahili treatment sawa.
NAKAZIA HII [emoji116]Basi tu ndio dini zetu na sisi wanadamu tunatofautiana katika mapokeo ya hizi dini zetu.
Yaani mimi nifanye uzinzi na mwanamke tukiwa hatujaoana kwa raha zetu, halafu tukioana ama kutubu dhambi hiyo basi tunafutiwa lakini mtoto aliyetokana na starehe zetu yaani hajui chochote kuhusu starehe yangu na mama yake ndio hiyo dhambi inamuhuku hadi kifo chake nadhani huyo mnayemwabjdu is very unfair.
Yaani nyie wazazi mzini halafu atokee mtoto wewe mwanaume umkatae na kumpachika jina eti MWANAHARAMU ni kwa nini hilo jina lisiwe MZAZI HARAMU? Yaani ukipita popote baba uitwe hivyo lakini mnampa mzigo mtoto ambaye wakati mimba inatungwa hata hakuwa na habari ya uharamu maana sperms na ovules za wazazi hazina tofauti na zile za walio kwenye ndoa hamuoni hii ni unfair.
1. Huyo mnayemwabudu kwa nini asingejwwka mzigo huu kwenu wazazi?
2. Kwamba mnayemwabudu hakujua kuww kuna madhalimu na wabaya huwa wanabaka?
3. Hakujua kuww huu ni unyanyapaa kwa kiumbe ambacho hakikuwa na habari juu ya huo uzinzi?
4. Kwa nini kufanya uzinzi kuonekana ni dhambi ya muda mfupi lakini zao la uzinzi kuwa na adhabu ya milele?
5. Kwa nini hajawaagiza kukazia juu ya watoto wa Ibrahim mjifunze?
6. Huyo mnayemwabudu anawaza sawasawa?
7. Je hajui kuwa kuna wengine wanaanza kumwabudu pia baada ya kuwa wamemaliza kuzaa halafu leo unalazmishwa uwaite wanao haramu?
8. Mbona naona huyu mnayemwabudu ni mfarakanishi? Yaani leo mimi na mke wangu tulikua tukiishi kwa kufuata imani tofauti na hii tukajaaliwa kupata watoto 6, leo nikiamua kuja kwenye imani hii mpya naambiwa hao wanangu wote 6 ni haramu na hawatambuliwi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
MSIMAMO WANGU:
"HAKUNA MTOTO HARAMU BALI KUNA WAZAZI HARAMU"
Chief nimejua tatizo lako wapiHuyo Mungu unayedai amekuambia Umtenge mwanao wa damu, amewahi kukuambia wewe hayo maneno AU ni umesoma na kukariri maandiko yaliyoandikwa na waarabu ambao walidai yanatoka kwa mungu???!!
Nikikuambia uthibithshe kuwa hayo maandiko yaliyoandikwa na hao waarabu kuwa ni kweli yalitoka kwa Mungu aliyeumba Dunia utaweza kunithibitishia??
Sijui kwanini watu wanapenda kujenga hoja za kibabe kwenye swala ambalo liko wazi kabisa. Sasa yeye amezaliwa amekuta kanuni. Basi anaanza kupingana nazo anaamini akizijengea hoja itahalalisha uovu anaofanya. Haramu ni haramu tuAfadhali madam nawe umeliona hili
Huyo Alah ni mungu wako wewe kwa imani yako. Elewa kwanza hili, usiendelee kukaririshwa msikitini.Mkuu Mungu ni mmoja Tu naye ni Allah,Mitume wote tangu Zama na zama walikuja kumlingania Mungu mmoja Tu basi.
Sasa hao miungi wengine sijui wanatoka wapi kwakweli?
Siku ya mwisho ambao watafaulu na kuuona uzima WA milele au kuingia peponi ni Wale ambao hawamshirikishi Mungu na chochote kile.
Na wale ambao wanamshirikisha Mungu vitendo vyao vitaangukia patupu Kwa maana hata ufanye amali njema au vitendo kiasi gani hakuna utakacho kichuma huko siku ya hukumu.
Okoa nafsi yako kabla siku ya mwisho haijafika chief
Hakuna mahali nimesema Waarabu na Wazungu wameanzisha dini. Usiniwekee maneno ambayo sijayasema.Chief nimejua tatizo lako wapi
Unaamini kuwa waarabu na wazungu ndio wameleta au kuanzisha Dini.
Sidhani hata kama kuna haja ya kujadili haya maswala kwasabubu ni watu wawili wenye mitazamo tofauti kabisa