Je, mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya urithi?

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Habari za asubuhi, mchana na jioni. Hapa mtaani kuna sekeseke limetokea, mzee mmoja Mangi wa Rombo ameowa mwanamke wa kidogo kutoka mkinga huko Tanga.

Katika maisha yao ya ndoa wamejaaliwa watoto 3 ila katika hao watoto mmoja wa kiume sio wa Mangi na alimpima DNA huko kenya ikaonesha kweli sio wake na mwanamke akathibitisha hilo.

Sasa huyo Mangi aliugua sana kidogo afe kauguzwa kapata nafuu kaamua kugawa urithi kwa watoto wake wawili kamuacha yule mmoja.

Ndipo timbwili lilipoanzia mama mtu akidai huyo mwanawe nae ana haki ya urithi kama nduguze.

Mangi amegoma katakata na kesi imeenda kwa wazee, wazee wakaamua kitanda hakizai haramu maana maadamu alizaliwa ndani ya ndoa basi ana haki kweli.

Mangi kagoma katakata nakusema huyo mtoto ana baba yake na ndipo haki yake ya urithi ilipo na sio kwake.

Mwanamke ameamua kwenda mahakamani kwa sasa kesi iko mahakamani mwanamke anataka apewe talaka yake na mumewe!

Katika mali za Mangi alikuwa na nyumba 2 hapo dar, lodge za kulala wageni 2 hapo dar, bar moja hapo dar.

Huko Rombo alikuwa na nyumba 1 na shamba la takribani heka 3. Na mwanza ananyumba 1 na lodge 2 za kulala wageni.

Swali langu ni je! Huyo mtoto ana haki yakupata urithi kama wazee walivyoamua wapande zote mbili wa huko Rombo na Tanga au hana haki kama Mangi anavyodai.

Kwa wataalamu wa kijamii hili swala limekaaje maana kwa sasa Mangi amehama nyumba kabisa kutokana na maelewano kuwa madogo baina yake na mke.
 
Vijana acheni kuoa kama uwezo wenu wa kupambana na matukio ni mdogo.
Wanawake= watoto wake
Sasa haijasemwa ni watoto wake nani. Akili kichwani
 
Kwani wewe ukimrishisha utafungwa au kuuwawa
 
Anampaje urithi mtoto wa Baba mwingine.

Na tokea ajue huyo sio mtoto wake alikuwa bado anafanya nini na huyo mwanamke.

Halafu kama ni wosia alianzaje kumuonesha Mke wake?
 
Kanuni za urithi:
1. Moto hurithi Mali za baba yake tu.
2. Moto wa Kambo Hana urithi
3. Kwa huruma ya mwenye Mali, anaweza kumrithisha Mali mtoto asiye wake sehemu tu ya Mali zake. Na hii SI lazima na Wala haidaiwi mahakamani. Kwahiyo hiyo Mzee yupo sahihi kukataa kumrithisha Mali mtoto asiye wake.
 
Anampaje urithi mtoto wa Baba mwingine.

Na tokea ajue huyo sio mtoto wake alikuwa bado anafanya nini na huyo mwanamke.

Halafu kama ni wosia alianzaje kumuonesha Mke wake?
Mzee amegawa kwa watoto kwasababu hali yake kiafya sio nzuri ulitaka afanye siri ilhali anajua vita atakayoiacha akifa!
 
Habari za asubuhi, mchana na jioni. Hapa mtaani kuna sekeseke limetokea, mzee mmoja Mangi wa Rombo ameowa mwanamke wa kidogo kutoka mkinga huko Tanga.

Katika maisha yao ya ndoa wamejaaliwa watoto 3 ila katika hao watoto mmoja wa kiume sio wa Mangi na alimpima DNA huko kenya ikaonesha kweli sio wake na mwanamke akathibitisha hilo.

Sasa huyo Mangi aliugua sana kidogo afe kauguzwa kapata nafuu kaamua kugawa urithi kwa watoto wake wawili kamuacha yule mmoja.

Ndipo timbwili lilipoanzia mama mtu akidai huyo mwanawe nae ana haki ya urithi kama nduguze.

Mangi amegoma katakata na kesi imeenda kwa wazee, wazee wakaamua kitanda hakizai haramu maana maadamu alizaliwa ndani ya ndoa basi ana haki kweli.

Mangi kagoma katakata nakusema huyo mtoto ana baba yake na ndipo haki yake ya urithi ilipo na sio kwake.

Mwanamke ameamua kwenda mahakamani kwa sasa kesi iko mahakamani mwanamke anataka apewe talaka yake na mumewe!

Katika mali za Mangi alikuwa na nyumba 2 hapo dar, lodge za kulala wageni 2 hapo dar, bar moja hapo dar.

Huko Rombo alikuwa na nyumba 1 na shamba la takribani heka 3. Na mwanza ananyumba 1 na lodge 2 za kulala wageni.

Swali langu ni je! Huyo mtoto ana haki yakupata urithi kama wazee walivyoamua wapande zote mbili wa huko Rombo na Tanga au hana haki kama Mangi anavyodai.

Kwa wataalamu wa kijamii hili swala limekaaje maana kwa sasa Mangi amehama nyumba kabisa kutokana na maelewano kuwa madogo baina yake na mke.
Acheni kutesa watoto kwa kuwanyanyapaa na kuwaita majina ya ajabu kama watoto wa nje ya ndoa au watoto haramu na kuwanyima haki zao kwa kizingizio za imagination iitwayo ndoa. Wototo wotw ni sawa na wana haki sawa, tena watoto wa hivyo ndio wamekuwa msingi wa ukomboziwa ukoo na familia .Tuwaheshimu hili suala la ndani ya ndoa au nje ya ndoa ni ideology za kigeni na zilizopitwa na wakati
 
Wakati huyo mama anachepuka mpaka anapata mimba hakuyajua haya yote? avogadro
 
Mzee amegawa kwa watoto kwasababu hali yake kiafya sio nzuri ulitaka afanye siri ilhali anajua vita atakayoiacha akifa!
Sasa ameanzisha vita akiwa hai na ndio maana inatakiwa iwe Siri.

Na huo wosia ilitakiwa uende mahakamani, kanisani, au mwanasheria kama anae.

Sasa akifa ndio mzigo unaletwa mezani inakuwa haina mjadala mke angepambana na Jamuhuri.
 
Ana mwanasheria na huo urithi ameuweka kisheria ndio maana mwanamke anataka apewe talaka ili iwe rahisi kumpatia huyo haramu!
 
Duuuuh, inaumiza Sana.

Ndio maana wale wazee wa kampeni za kutooa wana hoja.
 
Sababu yao ni kuwa mtoto kazaliwa ndani ya ndoa hivyo sio haramu ni wake na pamoja kwamba anatumia jina la huyo Mangi.

Basi ishu iliyokua apo inaonekana mangi hakuwatarifu wazee kua uyoo mtt sio wake ndo maana hazi mamb zinatokea
 
Wazee wanafahamu wa pande zote mbili. Na ndio maana wanasema kitanda hakizai haramu na maadamu kazaliwa ndani ya ndoa ni wake. Kwa mila zetu za kiafrika mtoto akizaliwa ndani ya ndoa ana haki zote za urithi kutoka kwa baba yake.
 
Back
Top Bottom