Je, mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya urithi?

Je, mtoto wa nje ya ndoa ana haki ya urithi?

Habari za asubuhi, mchana na jioni. Hapa mtaani kuna sekeseke limetokea, mzee mmoja Mangi wa Rombo ameowa mwanamke wa kidogo kutoka mkinga huko Tanga.

Katika maisha yao ya ndoa wamejaaliwa watoto 3 ila katika hao watoto mmoja wa kiume sio wa Mangi na alimpima DNA huko kenya ikaonesha kweli sio wake na mwanamke akathibitisha hilo.

Sasa huyo Mangi aliugua sana kidogo afe kauguzwa kapata nafuu kaamua kugawa urithi kwa watoto wake wawili kamuacha yule mmoja.

Ndipo timbwili lilipoanzia mama mtu akidai huyo mwanawe nae ana haki ya urithi kama nduguze.

Mangi amegoma katakata na kesi imeenda kwa wazee, wazee wakaamua kitanda hakizai haramu maana maadamu alizaliwa ndani ya ndoa basi ana haki kweli.

Mangi kagoma katakata nakusema huyo mtoto ana baba yake na ndipo haki yake ya urithi ilipo na sio kwake.

Mwanamke ameamua kwenda mahakamani kwa sasa kesi iko mahakamani mwanamke anataka apewe talaka yake na mumewe!

Katika mali za Mangi alikuwa na nyumba 2 hapo dar, lodge za kulala wageni 2 hapo dar, bar moja hapo dar.

Huko Rombo alikuwa na nyumba 1 na shamba la takribani heka 3. Na mwanza ananyumba 1 na lodge 2 za kulala wageni.

Swali langu ni je! Huyo mtoto ana haki yakupata urithi kama wazee walivyoamua wapande zote mbili wa huko Rombo na Tanga au hana haki kama Mangi anavyodai.

Kwa wataalamu wa kijamii hili swala limekaaje maana kwa sasa Mangi amehama nyumba kabisa kutokana na maelewano kuwa madogo baina yake na mke.
Huyu si mtoto wa nje ya ndoa.
Angekua mtoto wa nje ya ndoa iwapo angezaliwa na baba huyu mtoa mirathi lakini kwa mwanamke mwingine nje ya ndoa.
Huyu ni mtoto asiezaliwa na baba mtoa mirathi, Ana haki zote kupata mirathi kwa baba yake mzazi, aidha Ana haki ya kupata mirathi na akaitwa mtoto wa nje ya ndoa kwa mirathi ya mama.
 
Acheni kutesa watoto kwa kuwanyanyapaa na kuwaita majina ya ajabu kama watoto wa nje ya ndoa au watoto haramu na kuwanyima haki zao kwa kizingizio za imagination iitwayo ndoa. Wototo wotw ni sawa na wana haki sawa, tena watoto wa hivyo ndio wamekuwa msingi wa ukomboziwa ukoo na familia .Tuwaheshimu hili suala la ndani ya ndoa au nje ya ndoa ni ideology za kigeni na zilizopitwa na wakati
Akili ndogo
 
Back
Top Bottom