Je, mtu unaweza kufunga ndoa kanisani bila kusaini lile karatasi?

Je, mtu unaweza kufunga ndoa kanisani bila kusaini lile karatasi?

Naona kama unataka kuichenga nafsi yako mwenyewe, unataka kuwaridhisha watu. Ndio maana nawasisitiza vijana kila siku tuwajengee watoto wetu wa kike confidence, tuwape elimu waweze kusimama na kuamua maisha yao. Wewe ndugu yetu unataka kumfanya mwanamke kama zuzu yaani uingie nae mkataba feki wa ndoa ambayo mahakama wala dini haitambui.
Sasa lengo si kuepuka kile wanchoita kuzaa nje ya ndoa na kuzini.., sasa mimi nimechoka hayo masimango, nimechoka kabisa.., nataka niende huko kanisani sasa, kwani kitu gani? Ila sitaki kusainishwa, kwani nauza nini au nanunua nini?! Kwanini mnatupa wakati mgumu hivi hapa duniani?! Tuacheni tuishi bhanaa.., pelekeni utaahira wenu huko!
 
Sasa lengo si kuepuka kile wanchoita kuzaa nje ya ndoa na kuzini.., sasa mimi nimechoka hayo masimango, nimechoka kabisa.., nataka niende huko kanisani sasa, kwani kitu gani? Ila sitaka kusainishwa, kwani nauza nini au nanunua nini?! Kwanini mnatuoa wakati mgumu hivi hapa duniani?! Tuacheni tuiwhi bhanaa.., pelekeni utaahira wenu huko!
Sasa kama sisi mataahira nenda kafunge ndoa bila kutia wino kila la heri ndugu yetu. Ila Ujue huyo utakayemuita mke wako atakuwa huru kuolewa na mwanaume mwingine sababu wewe na yeye hamna ndoa.
 
Wachungaji/mashehe/manabii ....etc wanaofungisha ndoa ni mawakala wa serikali - RITA. Wanatekeleza Sheria, hivyo uwazalo haliwezekani
 
Utakuwa hujafunga ndoa bali maonyesho ya ndoa.
Ndoa ni jambo la kisheria na ndoa inafungwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ile karatasi ni ya kiserikali isipokuwa inafungwa kwa mujibu wa imami yako ya kikristo
Ni mkataba wa kisheria kama ilivo mikataba mingine
 
Sahihi, huyu mleta uzi anataka kufanya igizo la ndoa
Igizo kwa msingi upi wakati natekeleza kile mnachoita agizo la Mungu? Kwani alisema tuweke saini ndio iwe ndoa? Biblia ndio imesema hivyo?
 
Tunaambiwa kwamba kuendelea kuishi pamoja na kuzaa watoto bila kufunga ndoa kanisani ni uzinzi
Huu ni uongo mkubwa ambao watu wengi hawajaugundua. Chukua biblia yako ipekue yote kila mahali ukipata sehemu inayosema tufunge ndoa kanisani na kusaini cheti uje nayo hapa ntakupa chochote unachokitaka
 
Tunaambiwa kwamba kuendelea kuishi pamoja na kuzaa watoto bila kufunga ndoa kanisani ni uzinzi na kumchukiza Mungu.

Sasa na mimi nauliza, naweza kwenda kanisani kufunga ndoa bila kusaini chochote? Yaani taratibu zoote za kanisa na mashahidi wawepo kushuhudia ndoa, ila sitaki kusaini chochote, inawezekana?
ile kusaini makaratasi ni utaratibu kiserikali. Kwa lugha rahisi pale ni mikataba miwili mmoja wa kiimani/kidini na kiserikali
 
ile kusaini makaratasi ni utaratibu kiserikali. Kwa lugha rahisi pale ni mikataba miwili mmoja wa kiimani/kidini na kiserikali
Sasa mimi nataka ule mkataba wa kiimani tu ili niache kuzini na kumzalisha mtoto wa watu nje ya ndoa kama wanavyonisimanga.., sitaki huo wa serikali sasa...!
 
Back
Top Bottom