Dumas the terrible
JF-Expert Member
- Jan 20, 2021
- 4,779
- 9,999
Project iliyowaleta kwenye Accient civilization ilikua ni Gold,Hao viumbe kutoka sayari nyengine mwisho wa hii project yao juu yetu ni nini?
Dhahabu ilikua ni lengo kuu kwao
Inadaiwa Dhahabu ni ufunguo wa maisha kwao maana hapo kale ulitokea mtafuruku kwenye Sayari Zao uliokuja kuzalisha vita Kali Sana iliyohusisha Nuclear reactors power kutokana na ujuzi mkubwa wa kiteknolkjia walikuta wameharibu mifumo ya kawaida wa Sayari za Orion's
Wakajikuta Kuna material wanazihitaji Ili kurecover Moja wapo ni dhahabu basi ndio waakanza kuzunguka Sayari mbali mbali wakizitafuta ndio wakajipata wapo duniani na hapa walikuta mfumo tofauti wa kimazingira kama ilivyo Sasa,
Katika maandiko ya kale ya Sumerian wanadai waliwakuta duniani viumbe mithili ya primitive wakiishi kama wanyama wengine wa kawaida na changamoto kubwa kwao licha ya technology kubwa ila walihitaji man power wa kusaidia kazi na ndipo walipoanza majaribio ya kisayansi ya kumproject primitive Kwa kuchanganya DNA tests mara ya kwanza walianza kupata viumbe vingi kama
marmeids
viumbe kichwa Cha mbuzi kiwili wili Cha Binadamu na miguu yenye kwako,
Wakatengeneza nusu
Mtu nusu nyani
Wakatengeneza nusu farasi nusu Mtu
Wakatengeneza nusu nyoka nusu Mtu
Tatizo lilikuja Hawa viumbe walio wa project walifeli kwenye uzalishaji yaani hao viumbe wote walikua hawana uwezo wa kuzalisha Zaidi na walichukua kipindi kichache kusurvive
Annunaki wakaona wanaingia hasara kutengeza sample Kila siku kuongeza nguvu KAZI ndio walipokaa na kuamua
Kutoa DNA Za miili Yao na kuunganisha na ya primitive
Wakabahatika kumtoa Homo sapiens Sapiens kamili ambae ndie super human na akawa na uwezo wa kuzalisha na ana life span ndefu,mwenye akili,ujuzi na kutambua Nini anafanya
Humanoids waliweza kufanya Kazi wakiongozwa na akili Zao timamu na ANUNNAK wakawapa ujuzi mkubwa sana wa kuchimba gold na kuanzisha ustaarabu wa kwanza wa kale na ndio historia ya Mwanadamu na Watu ikaanzia hapo,
Hapo tunaona lengo ni Gold tu na Ndio maana jiulize Toka Hapo kale walikua wanachimba dhahabu Kwa mamillion ya Tani na zikaja kupotea ghafla tu zilienda wapi na hua haziozi?
Jibu utapata mataifa makubwa yanajua Siri za Gold na ndio maana inazalishwa Kwa wingi ila hua haieleweki inakopotelea hata utafiti wa Hivi majuzi unadai Kuna upotevu wa kutatanisha wa dhahabu yaani kiwango kinachozalishwa ni kikubwa ila kinachoingia kwenye rekodi ni kidogo Sana
Secrets a.k.a secreto!