Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Hao viumbe kutoka sayari nyengine mwisho wa hii project yao juu yetu ni nini?
Project iliyowaleta kwenye Accient civilization ilikua ni Gold,
Dhahabu ilikua ni lengo kuu kwao
Inadaiwa Dhahabu ni ufunguo wa maisha kwao maana hapo kale ulitokea mtafuruku kwenye Sayari Zao uliokuja kuzalisha vita Kali Sana iliyohusisha Nuclear reactors power kutokana na ujuzi mkubwa wa kiteknolkjia walikuta wameharibu mifumo ya kawaida wa Sayari za Orion's
Wakajikuta Kuna material wanazihitaji Ili kurecover Moja wapo ni dhahabu basi ndio waakanza kuzunguka Sayari mbali mbali wakizitafuta ndio wakajipata wapo duniani na hapa walikuta mfumo tofauti wa kimazingira kama ilivyo Sasa,
Katika maandiko ya kale ya Sumerian wanadai waliwakuta duniani viumbe mithili ya primitive wakiishi kama wanyama wengine wa kawaida na changamoto kubwa kwao licha ya technology kubwa ila walihitaji man power wa kusaidia kazi na ndipo walipoanza majaribio ya kisayansi ya kumproject primitive Kwa kuchanganya DNA tests mara ya kwanza walianza kupata viumbe vingi kama
marmeids
viumbe kichwa Cha mbuzi kiwili wili Cha Binadamu na miguu yenye kwako,
Wakatengeneza nusu
Mtu nusu nyani
Wakatengeneza nusu farasi nusu Mtu
Wakatengeneza nusu nyoka nusu Mtu
Tatizo lilikuja Hawa viumbe walio wa project walifeli kwenye uzalishaji yaani hao viumbe wote walikua hawana uwezo wa kuzalisha Zaidi na walichukua kipindi kichache kusurvive
Annunaki wakaona wanaingia hasara kutengeza sample Kila siku kuongeza nguvu KAZI ndio walipokaa na kuamua
Kutoa DNA Za miili Yao na kuunganisha na ya primitive
Wakabahatika kumtoa Homo sapiens Sapiens kamili ambae ndie super human na akawa na uwezo wa kuzalisha na ana life span ndefu,mwenye akili,ujuzi na kutambua Nini anafanya
Humanoids waliweza kufanya Kazi wakiongozwa na akili Zao timamu na ANUNNAK wakawapa ujuzi mkubwa sana wa kuchimba gold na kuanzisha ustaarabu wa kwanza wa kale na ndio historia ya Mwanadamu na Watu ikaanzia hapo,

Hapo tunaona lengo ni Gold tu na Ndio maana jiulize Toka Hapo kale walikua wanachimba dhahabu Kwa mamillion ya Tani na zikaja kupotea ghafla tu zilienda wapi na hua haziozi?
Jibu utapata mataifa makubwa yanajua Siri za Gold na ndio maana inazalishwa Kwa wingi ila hua haieleweki inakopotelea hata utafiti wa Hivi majuzi unadai Kuna upotevu wa kutatanisha wa dhahabu yaani kiwango kinachozalishwa ni kikubwa ila kinachoingia kwenye rekodi ni kidogo Sana

Secrets a.k.a secreto!
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Swali lako linaweza jibiwa endapo tutakonsider kwamba huenda Mungu alitoka kwenye ulimwengu mwingine nje na huu ambao tunaujua.

**** theory inasema huenda kukawa na ulimwengu to infinity na zote zina tabia tofauti: utakuta kuna ulimwengu mda unarudi nyuma, utakuta kuna ulimwengu hakuna mda, utakuta kuna ulimwengu ambao ni 2 dimension, ulimwengu ambao kuna binadamu ambqo hawafi. Nimesema ulimwengu msije chanyanya na sayari kwani ni vitu viwili tofauti.

Sasa huyu mungu kaumba ulimwengu ambao una time. Na chochote chenye time lazima kiwe na mwisho na mwanzo. Hapo sasa ndo mwanadamu anataka apate gate pas ya kuingia ulimwengu mwingine ambao ni time less. Maam kifo chatisha.

Na saa ivi technology inatupeleka kwa kitu kinaitwa Metaverse Facebook wanatengeneza ulimwengu wao kwenye computer, na magame nyingine tayari wana ulimwengu wao tayari, sasa waona mfanano wa hizi verse ambazo mwanadamu anazitengeneza kwenye mifumo ya kompyuta na analogy y muumba anayeumba ulimwengu na kuweka sheria zake.

Pia kuna utata mkubwa sasa kwenye huu tunaoona ni uhalisia, kuna uwezekano hivi vyote tunavyodhani ni maisha yetu ni computer simulation iliyotengenezwa hapo kalee. Dunia yaenda kasi sana
 
Kwani sasa hivi Yuko wapi? Najua kuwa kiroho yupo kila mahali, lakini je, Kiti chake cha Enzi kiko wapi? Ukijua mahali kilipo muda huu Kiti chake cha Enzi, basi ndiyo huko ambako amekuwepo milele yote
Paliumbwa na nani hapo kilipo kiti? Kama alipaumba yeye, alipaumba akiwa wapi wakati alikuwa hajaumba kitu bado?
 
Nani aliumba Heaven? Mungu? Aliumba Heaven akiwa wapi?
 
Kwa maelezo yako ni kwamba hata yeye hakuwepo, kama ni absolute nothingness, in every sense of the word (unayoijua na usiyoijua) , means hakuwepo, hata consiousness yake, haikuwepo, ili kitu kiwepo, inabidi kiwepo. Haiwezekani kitu hakipo halafu useme kipo, how?!
 
 
Na Je Waandishi wa Hivyo Vitabu nitakavyosoma Ni Sisi Binadamu au ni Hao Viumbe.?

If ni Sisi Binadamu basi Hakuna Tofauti na Vitabu vyetu vya Biblia na Quran maana Ukweli hauwezi Kuandikwa na Anayetafuta Ukweli wenyewe
 
Kama Binadamu wa Kwanza Aliumbwa Kisa Gold [emoji1628] How Come Binadamu wa Kwanza Hakujua Kuhusu Gold [emoji1628]ila alikuwa anajua Kuhusu Stone zama Za Mawe ndipo zilianza Huko hakukuwa na Binadamu aliyejua Kuhusu Dhahabu mpaka Pale Zama za Mbele sana Na Civilization kuanza.

Binadamu wengi waliishi kwa Kutumia Mawe.. baadae wakagundua Silver [emoji1627] baadae ndio Dhahabu ikaja

Je huoni kwamba Unapotea Ndugu yangu kwa Story za Kutungwa Tu. Maana Hao Viumbe Umesema tena Waliwakuta Viumbe wanaishi kama Wanyama Hao Viumbe Walitokea Wapi Kama Wao waliwakuta ??
 
mkuu tunawaheshimu wazazi coz kibaiolojia wanahusika na existence yetu, kwa nini hatujawahi/wala hatuwezi kuwahoji kua game ya kupatikana kwetu ilichezwaje au ilichezwa wakati gani?

kama tumeshindwa kuwahoji wazazi, mamlaka ya kumhoji mungu tunayapata wapi?
tuoneshe heshima kwa muumba wetu madam anahusishwa na existence ya kila kitu.
 
Mbinguni kwanza ni wapi waislamu wanatuambia kuna mbingu ya saba hizo mbigu zipo wapi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ulimwengu ni ni kila kinachoweza kuwepo combined. Ni totality ya everthing that is.
Ongea kiswahili na sisi waswahili tucahngie.

Ukisema combined unakusudia nini ?

Ukisema "totally ya everything that is" unakusudia nini ?

Huu mjadala mzito sana usichanganye lugha
 
Kiufupi Mungu ni mwanzo asiyekuwa na mwanzo ,na mwisho asiyekuwa na mwisho.
Alikuwepo,atakuwepo,na atabakia
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hakujua hata DNA ni nini
 
waliokua wanatumia zana za Mawe ni Homo Elactus
Ambao walikua Bado Wana u primitive
Baada ya Annunak kufika ndio wakamfanyia cloning project akawa homo sapiens Sapiens aliekamilika na super intelligent

Hata wanasayansi wanakili kwamba kulikua na mabadiliko ya ghafla Sana ya kimazingira maana homo Elactus walibadilika ndani ya Muda mfupi na kua homo sapiens kitendo kinachodaiwa kulikua na mwingiliano wa ghafla wa kitu kisicho Cha kawaida katika DNA zao
Yaani wanadai Homo Elactus Alikua kawaida tu ila baadaye ikaonekana ana DNA zilizopandikizwa kutoka Nje ya mfumo wetu wa Nyota na kumfanya awe modern Man na hapo hapo anaanza ustaarabu mkubwa wenye ujuzi wa kushangaza
Hivyo nadharia za Annunak kumproject Zina mashiko!
 
Ulichokiandika hakina tofauti na wanaoandika kwa mlengo imani ya dini. Umekielezea ulichokiamini nao wanaelezea wanachokiamini.

Unajua katika race zote ulimwenguni mzungu ndiye race ya mwisho kupata elimu na kuendelea mpaka leo hii. Kwa kila zama ziliendelea kielimu, kiuchumi, kitabibu na kiteknolojia kulingana na zama husika. Mzungu ndiye akawa race ya mwisho kurithi haya.

Lakini mzungu alichokifanya ni kuzima vumbuzi za nyuma kwa kuzinyanyua kuzifanya za kwake husika na kwa mlengo huo zama zilizopita akazifanya ni dark ages, ndilo jina alilolipa. Na kama nilivyoelezea hapo awali; asili ya mzungu kupata elimu ni Misri ya kale. Anachokifanya mzungu ni kupoteza ushahidi wa maendeleo ya kiujumla ya zama zilizopita kwa kupachika ANUNAKI, na kama ukihitaji kulifahamu hili zaidi angalia documentaries zinazoelezea maendeleo ya Misri ya kale, wazungu wanakataa wanasema kwa karne hizo binadamuasingekuwa na ujuzi huo bali kuna msaada wa waziunaonekana aliupata. Kutoka kwa nani? Jawabu wanakupatia ni ANUNAKI.

Hivyo, hili suala la ANUNAKI usiliangalie kwa upande mmoja wa chapa ya sarafu, liangalie kwa pande zote mbili. Jawabu utakalolipata ni suala si ANUNAKI, suala ni kuna kitu wanajaribu kukifanya.

Imani yako juu ya ANUNAKI naiona haina tofauti na imani ya wale wanaosema wanaoamini vitabu vitakatifu vya Mungu.
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Ya Ngoswe tumwachie Ngoswe
 
Kwahiyo unataka kunambia kabila la Dogon kule nchini Mali waliohifadhi kumbukumbu za mababu zao ni Wazungu mpaka wadanganye kwamba mababu zao wa kale huko misri walitembelewa na Miungu kutoka Orion mpaka wadanganye?
Think twice Broo Hata hao Wazungu waliambiwa na wamesoma text za kale ya kwamba wamisri wa kale waliweza cooperate na viumbe kutoka nyota za mbali kitu ambacho hata wao kinawashangaza iliwezekanaje?

Ukweli utabaki kua ukweli tu daima ya kwamba mababu wa kale huko misri walifikia maendeleo makubwa mpaka kuweza kushirikiana na viumbe kutoka Orion's!

Acha kubeza ukweli mchungu!
 
Paliumbwa na nani hapo kilipo kiti? Kama alipaumba yeye, alipaumba akiwa wapi wakati alikuwa hajaumba kitu bado?
Swali lako hapa linaelekea kuwa na mfanano wa NINI KILIANZA KATI YA KUKU NA YAI
Asili ya Mungu ni kwamba hajaanza; alikuwepo siku zote na pia vile vile hana mwisho. Hiyo ni ASILI yake ambapo katika hali ya kawaida, ASILI huwa haihojiwi. Huwezi kwa mfano ukauliza kwa nini binadamu hafanani na ng'ombe au the vice versa, kwamba ng'ombe naye hafanani na binadamu. Au ukahoji kwamba kwa nini ng'ombe nao wapo, possibly baada ya kuwa umepata mawazo kuwa ni binadamu tu ndiyo alitakiwa kuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…