Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?

Unadha ujumbe wa Mungu ungefika vipi bila kutumia binadamu wenzetu?
Ungejiuliza kwanza Binadamu wa Kwanza Kuumbwa alipataje Ujumbe Wa Mungu. Na wakati alikuwa Mwenyewe.

Na kama Hao Manabii ni wa Mungu kweli inakuwaje Kuna Wakristo(Yesu) Waislamu(Mohamed) wayahudi(Musa) n.k

Je huoni hapo Si Mungu ila Ni Viumbe Wengine tu
 
Binadamu wa kwanza ambaye NI Adam alipata ujumbe kupitia kwa malaika.
Lakini pia inasemekana alikuwa anaongea na Mungu.
kuhusu mitume na manabii kuwa tofauti sio kweli maana wote walikuwa na ujumbe mmoja wa kumuabudu Mungu mmoja.
Tofauti inakuja kwenye mapokeo ya vitabu
Ungejiuliza kwanza Binadamu wa Kwanza Kuumbwa alipataje Ujumbe Wa Mungu. Na wakati alikuwa Mwenyewe.

Na kama Hao Manabii ni wa Mungu kweli inakuwaje Kuna Wakristo(Yesu) Waislamu(Mohamed) wayahudi(Musa) n.k

Je huoni hapo Si Mungu ila Ni Viumbe Wengine tu
 
Mungu anasehemu yake na Viumbe wake wanasehemu yake ya Kuishi.

Hakuna anayejua Mungu anakaa wapi wala anaishi wapi.

Kwahiyo huwezi Jua Alikuwa wapi kipindi anaumba Chochote.
Hapo anapokaa, kabla hajaumba chochote, paliumbwa na nani wakati alikuwa hajaumba kitu bado
 
Mungu hawezi kuumba wala kufanya chochote.

Mungu hayupo.

Binadamu ndiye alimuumba Mungu kwenye fikra zake.
Then where did the universe came from?,
actually it takes a lot of faith to be an atheist, is like telling me your house came from physiochemical reactions, without any work of a mason.
 
What about the materials which God used to create whatever that exists....je alitoa wapi hizo materials?

Some questions are beyond human comprehension. Hauwezi kuelewa kwa sasa kuhusiana na swali lako. Ni sawa na swali na Mungu alitoka wapi? No mortal being can fathom the truths thereof.

All i know ni kuwa mazingira yananipa ushahidi madhubuti wa uwepo wa Mungu. Na whatever alichokisema Mungu kwenye Scriptures kuhusu namna alivyoumba ndiyo information pekee tuliyonayo kwa sasa. Beyond that hakuna majibu.

Mungu ndiye ajuaye wakati anaumba aliumbaje umbaje...na haku reveal hiyo information kwetu. When we get to heaven utamuuliza hili swali na mengine mengi...bila shaka utajibiwa.
God created all things from nothing, the only material he used to create was only his Word.
 
Hapo anapokaa, kabla hajaumba chochote, paliumbwa na nani wakati alikuwa hajaumba kitu bado
Wewe unachohoji ni Infinity thing. Maana Yake Hutopata Jibu. Na Mungu Hakai Maana Hana Makalio Kama Uliyonayo wewe. Wewe ndio unakaa maana Una Mwili wenye makalio

Unachoka Maana una Mwili. Kwahiyo Usimfananishe kama Ulivyo wewe kwamba Eti ana Sehemu amejenga ana Kaa.

Eti aliumba halafu akapumzika siku ya 7. Kupumzika maana Yake alichoka Manaa Yake Mungu anachoka Kama Wewe na Mimi ,kitu ambacho Akiingii akilini ila Ni Binadamu Tunamtungia Hadithi Mungu
 
Mimi sijakataa, hapo kabla ya kabla, ambapo alikuwa hajaumba chochote, ndio alikuwa wapi? Au hapo alipokuwepo paliumbwa na nani? Maana alikuwa hajaumba kitu bado. Pia hatumpo specific location, tunaulizia generality ya uwepo wake, hata kama ni yupo sehemu zote mida wote, kabla hajaumba kitu, ni wapi alikiwepo, na hapo alipokuwepo , paliumbwa na nani wakati alikuwa hajaumba kitu bado?
Husimfananishe na chochoteeee
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Kwani sasa hivi Yuko wapi? Najua kuwa kiroho yupo kila mahali, lakini je, Kiti chake cha Enzi kiko wapi? Ukijua mahali kilipo muda huu Kiti chake cha Enzi, basi ndiyo huko ambako amekuwepo milele yote
 
Hadith na nadharia za Mungu Zina utata na contradictions kibao,Watu was kwanza kuanza kuanzisha nadharia za Mungu ni wa accient civilization za kale kama Sumerians, Assyrian, Babylon, Egyptian, Kush, Aztec, Maya, Peru, Indus, valley nk
Hawa walianza Hizo nadharia baada ya Dunia kutembelewa na viumbe kutoka nje ya mfumo wetu wa Nyota yaani
ANNUNAK
Hao ndio waliomproject maabara Mwanadamu na kumpa ujuzi wote lengo atumike kama nguvu KAZI ya kuchimba dhahabu,dhahabu ilihitajika na hao viumbe kuizirudisha Sayari zao katika Hali ya kawaida baada ya kuharibiwa na vita vya
Nuclear reactors baada ya viumbe wale kumaliza mission na kuondoka Watu wakaanza waabudu kama Miungu na hata mwanzilishi wa Imani za Abrahamic alitokea Uru ya Ukaldayo Mesopotamia alikua akimuabudu Mungu El au Elohim (YHW)
Huyo alikua ni Moja kati ya Miungu wa Annunak na mapokeo mengi ya wayahudi Yana masimulizi ya sifa za huyo Mungu wao El mpaka pale zilipokuja zaliwa dini zenye mlengo wa huyu El kama Judaism, Christianity and Islamic
Na sio Kwamba El alikua ndie Mungu pekee hapana kulikua na Miungu wengi sana ukienda Kwa wahindi Wana Mungu wao Rama mwenye sifa kama za El
Ukienda misri Kuna Ra
Mesopotamia Kuna Anu
Kuna Enki
Na wengine wengi sana wote Wana mapokeo tofauti tofauti ila asili Yao ni Moja na Hao Miungu baadhi Yao walikua na bifu Kali sana mfano
Elohim YHW aliingia mkataba na agano na Abraham Kwamba uzao wake wote Watakua Watu wake na ni Marufuku kujihusisha na miungu mingine lengo lake awe na Watu wa kukamilisha mission zake Kwa urahisi na lengo la huyo Annunak El ni gold na dio maana mmoja wa uzao wa Abraham yaani Suleiman alikua na uwezo mkubwa sana na akili nyingi aliweza kukusanya gold Kwa maelfu ya matani na baadae zikapotea ghafla tu hata hatujui zilienda wapi hao ndio ANNUNAK na mission zao duniani

Nahitimisha ya Kwamba Hizo Hadith za Mungu mkuu muumbaji wa ulimwengu ni uongo na huyo Mungu hayupo na hajawahi kuwepo ila tu Watu waliamua kuwaita accient ANNUNAK miungu ila walikua Alliens tu!
We utakua mweu wewe
 
Mungu hawezi kuumba wala kufanya chochote.

Mungu hayupo.

Binadamu ndiye alimuumba Mungu kwenye fikra zake.
Na hii ni mara baada ya kula kushiba hadi kuvimbiwa na kuishia kuandika utopolo huu
 
Namaanisha kabla ya ulimwengu kuumbwa, Mungu aliumba ulimwengu na kila kilichomo akiwa wapi? Je, alikuwa Mbinguni? Na wakati anaumba mbingu, alikuwa anaiumba akiwa wapi?
Takujibu kwa ninachofahamu kutoka katika Biblia,
Mwanzo moja, inasema "hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi,"

Kabla ya yote kuwepo Mungu alikuwepo,

ALIUMBA AKIWA WAPI??
Kitabu cha ufunuo kinaonesha
Mungu aliumba malaika kabla ya kumuumba mwanadamu, so shetani alianguka kabla ya uumbaji wa mwanadamu
Alianguka kukutoka wapi HEAVEN,
SO MUNGU ALIUMBA ULIMWENGU FROM HEAVEN, Ila Roho yake ilikua juu ya vilindi vya maji vya dunia
 
Binadamu wa kwanza ambaye NI Adam alipata ujumbe kupitia kwa malaika.

Malaika Wapo Wabaya..Wazuri na Waovu Unajuaje Kwamba Alikuwa anaongea na Malaika Mzuri au Mbaya.. Kama Mungu amekamilika Inakuwaje Tena Anatuma Viumbe wengine kwenda Kuongea na Wengine

Mbona Wewe Hujawahi Kutumwa Kwenda kuongea na Malaika au Viumbe wengine kama jini na Mashetani. Yaani wao tu ndio wanakuja Kwako. Huwezi jiuliza Hata Kutumia Tu Akili hapo kwamba Unapumbazwa

Lakini pia inasemekana alikuwa anaongea na Mungu.

Kwanza Mungu Haongei na Viumbe wake. Maana Kuongea Ni mpaka Mtu apate Mwili na Mdomo na Ulimi. Mungu akiongea Basi Ujue Hapo Ana Mwili kama Wewe au Viumbe unavyo-viona vinatembea. Na Kama Angekuwa anaongea Mpka Leo hii angekuwa anaongea

Ukiona Ameandika Aliongea mwanzo halafu Leo hii Haongei Jua Umepumbazwa na Maandiko



Kuhusu mitume na manabii kuwa tofauti sio kweli maana wote walikuwa na ujumbe mmoja wa kumuabudu Mungu mmoja.
Tofauti inakuja kwenye mapokeo ya vitabu

Kwanza Hawakuja na Ujumbe Mmoja. Musa Alikuja Na Yake..
🟢Mambo ya Sabato n.k
🟢Torati

Yesu akaja na Yake..
🟢Mambo ya Mwana Wa Mungu
🟢Roho Mtakatifu

Mohamed akaja na Yake
🟢 Kuabudu Mecca
🟢Mungu hana Mshirika

Maana Leo Kuna Msikiti..Kanisa na Sinagogi. Kama Hawa Wangekuwa Wote wametumwa Na Mungu Basi Wasingepishana Hivyo. Leo hii Muislam anaabudu tofauti na Mkristo... Leo hii Wayahudi wanaabudu Tofauti na Waislamu na Wakristo. Sasa Hapo Mungu Mmoja Yupo wapi


[emoji1630]POLE KWA KUPIGWA BAN
 
Kwani sasa hivi Yuko wapi? Najua kuwa kiroho yupo kila mahali, lakini je, Kiti chake cha Enzi kiko wapi? Ukijua mahali kilipo muda huu Kiti chake cha Enzi, basi ndiyo huko ambako amekuwepo milele yote
Hamna Cha kiti Cha Enzi Wala Nini. Hapo ndo Mna mfananisha na binadamuuu...
 
Si mmesema ni beyond comprehension? Sasa inakuwaje tena unataka nimfahamu? Kikubwa swali ndio nimeuliza hilo, nipate majibu
Sisi ni viumbe ambao hatuna uwezo wa kuwepo sisi wenyewe. Uwezo wetu unaathiriwa na nguvu basi ingebaki katika hali ya kutokuwepo isingiwezekana sisi kutokea. Uwezo wa binadamu kufikiri unaathiriwa na uwepo wa mazingira. Imma yawe mazingira ya ndani ya sayari yetu au nje ya sayari yetu mifumo ya anga na kanuni na nidhamu yake.

Hivyo ndivyo tunavyofikiri kwa sababu ndiyo yaliyotuzunguka. Ikiwa kuna nguvu ipo nje ya huu mwenendo ama mazingira yaliyotuzunguka kwenye akili zetu inakuwa imetoka kwenye hali ya ufahamu wa ukawaida wa akili zetu. Ishara zitakufahamisha kuwa kipo lakini unaweza usikielewe kwa namna gani. Kinachohitajika kwako ni kuelewa tu kipo basi inatosha kwa sababu ukitaka kuelewa zaidi ya hapo kwa kutumia kanuni na nidhamu za kimazingira yaliyokuzunguka wewe utajisumbua. Hapa ndipo tunaposema haya mambo yapo juu ya ufahamu wetu. Tuyazungumzie haya masuala ni ni ambalo ulilouliza "Je, Mungu aliumba ulimwengu akiwa wapi?"

Kwanza inakubidi ufahamu Mungu hana mwanzo. Maana yake kuwepo kwake hakujatoka kwenye kitu kingine isipokuwa ni yeye mwenyewe. Kama ametokana na yeye mwenyewe maana yake hakuna nguvu kutoka pengine iliyoathiri na kufanya uwepo wake kwa maana kuwepo kwake hakujatoka kwenye kitu chengine bali kitu chenyewe (yaani yeye mwenyewe). Na kama ikiwa hivi inammanisha muda wote tokea na tokea yupo na hakuumbwa na kitu kingine. Hivyo yeye daima yupo.

Aliumba ulimwengu akiwa wapi?
Hili swali linamaanisha eneo ama mahali. Uwepo wake hautegemei chochote. Yeye ni wa daima wa tangu kabla ya chochote. Hivyo, alikuwepo Mungu pasipo na kitu chochote kuwepo na hapa ndipo inapokuja tafsiri yeye ndiye wa mwanzo kwa maana kabla ya chochote yeye yupo! Mbingu inaingia kwenye kitu. Sayari zinaingia kwetu kitu. The universe inaingia kwenye kitu. Space inaingia kwenye kitu. Giza inaingia kwenye kitu, Nuru zinaingia kwenye kitu. Na kama hakukuwa na kitu ina maana hakuna kilichomfunga, yaani ameepukana na pande 6. Hayupo juu(1) wala chini(2), hana kwake kuwa hapa itakuwa mbele(3) kwake hapa itakuwa nyuma(4). Na kwa kuwa hakuna kitu hutoweza kusema hapa ni juu(5) na hapa ni chini (6).

Jawabu swali lako: Mungu alikuwepo kabla ya chochote, kama alivyokuwepo kabla ya chochote kisha ndipo akauumba ulimwengu akiwa kwenye hali isiyokuwa na chochote.

Huyu ndiye ambaye unayemuulizia na ndiye ambaye aliyetuumba mimi na wewe.
 
Back
Top Bottom