Je, Mungu analo Jina? Jina lake ni lipi?

Bas Mungu wa waislam yuko na Siri sana asee
Ndio maana akaitwa Mungu.

Hata umbile lake hakuna atakayeweza kulikumbuka hata umuone mara elfu 10.

Siku ya qiyama waja watapata bahati ya kumuoma M/Mungu ila hawataweza kumkumbuka akitoweka machoni mwao.
 
Salaam, Shalom!!

Mungu ni Jina la Cheo kikubwa kuliko vyeo na mamlaka yote Mbinguni na duniani.

Swali ni je, Mungu analo Jina lake binafsi?

Jina la Mungu ni nani?

Karibuni [emoji120]
Jina la mungu linatumika afirika mashariki hasa chanzo chake ni pwani sehemu nyingine nchi nyingine hakuna jina hilo
 
Kwa sisi waislamu Mungu ana majina 100.

Majina yanayojulikana na wengi ni majina 99 hilo moja wanalijua mitumie na wale watu wacha Mungu sana.

Ukilijua hilo jina chochote utakachokiomba ni rahisi kukubaliwa ndani ya muda mfupi sana.
Uongo, kwanini wasitwambie na sisi hilo jina ndo kusema kwamba hakuna mitume wa kweli wala wacha Mungu sana?
Kama ni siri kuna ajenda gani wanatuzunguka eeh?
 
Mmh akikuelewa sijui, Niko pale
 
Tunataka kulijua Jina lake Moja linalozama Majina hayo mengine 99!!
Ilah(God) kwa lugha ya Aramaic ambayo ni lugha aliyokuwa akiitumia Yesu(issa) na Arabic ambapo ukiunganisha na Al(The) unapata Al Ilah yani Allah(The God).
 

Mungu mwenye mwanzo na mwisho (mwanzo 1:1,ufunuo 1:8, ufunuo 21:6, ufunuo 22:13) aliekuwa anaabudiwa na wengi hata yeye aliumbwa na Muumba yaani CHANZO HALISI (warumi 11:36) asiye na mwanzo wala mwisho.
 
Ilah(God) kwa lugha ya Aramaic ambayo ni lugha aliyokuwa akiitumia Yesu(issa) na Arabic ambapo ukiunganisha na Al(The) unapata Al Ilah yani Allah(The God).
Bado God Si Jina personal la Mungu.
 
Unalazimiaha ambacho hata ukijibiwa hukijui.

Shika Neno lake
Amini Neno lake
Tafuta USO wake.

Hayo ndo ya msingi sana. Safari ya Mbinguni haina ujuaji bali kuomba rehema na neema zake aliye mkuu wa wakuu wote
Jikite kwenye mada,

Jina la Mungu hulijui?

Kama hulijui Sema sijui, kama walijua, litaje.
 
Ana jina moja tu alilotupa kumtambulisha, jina la YESU.

Mapokeo yamefanya wengi wasisome na kuelewa kitabu (biblia) maana kila jambo liliandikwa litimie kwa majira na wakati sahihi.

Hata Yesu aliposema ufalme utaondolewa israel na kupewa taifa lingine (mathayo 21:43) wengine ukiwaambia watabisha kwakuwa dini na mifumo imelificha hilo, lakini limeandikwa na limeshatimia.

Hata Muumba anaposema itafika wakati atakuwa mmoja na jina lake moja maana miungu isiyoumba mbingu na nchi itaangamizwa (yeremia 10:11) wengine wanabisha ila imeandikwa

zekaria 14:9,
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.


1korintho 15:24-28

24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana (Yesu) mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
 
Uliyoyaandika,

Maji na Damu na akili ya kibinadamu haiwezi kuyaelewa Hadi yawe yamefunuliwa na Mungu kupitia Roho MTAKATIFU.

UBARIKIWE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…