Je, Mungu anapokupa jaribu anakuacha upambane nalo au anakuletea na usaidizi wake? Mjamzito anataka msaada wangu, hatujawahi kuwa na mahusiano

Je, Mungu anapokupa jaribu anakuacha upambane nalo au anakuletea na usaidizi wake? Mjamzito anataka msaada wangu, hatujawahi kuwa na mahusiano

Msaidie naona anakufanyia interview. Ukifanikiwa kuonesha utu anaweza kubali kukupa mimba na mtoto umleleee. So anza kumsaidia
 
Nina miezi sita sina ajira wala kazi na hali yangu ya uchumi ni mbaya mno, sina hata pa kuhemea.

Juzi nimekutana na mdogo wa rafiki yangu, tuliishi wote huko Arusha, dada ni mjamzito anasema amefukuzwa na bwanake, na bwanake karudisha na nyumba waliyokuwa wakiishi.

Nimemwambia urudi kijijini, anasema bora afe kuliko kurudi kijijini na hali ile. Ndugu zake niliachana nao siku nyingi sina namba zao za simu.

Kwa hali ya huyu dada anatakiwa kukaa chini ya uangalizi, sio ghetto.

Je namsaidiaje? Kwanini Mungu huu mtihani kanidondoshea mimi?

Kama unaweza msaidie wakati mwengine mungu hupima imani za watu na ukishinda umefanikiwa, mimi nililelewa na baba mwingine lakini sasa hivi huyu baba mwingine yupo proud sana kuwa na kijana kama mimi maana anakula bata sio za kawaida na maisha nimemnyooshea anakola kivulini,

Yule mzee wangu snitch ndo kajitokeza sasa anataka niwe mwanae ila nimempiga chini sitaki mazoea.... unaweza ukachelewa kuona return ya wema lakini inaweza kuja kukufaa baadae sana ukiwa umechoka, kama unaweza msaidie kama huwezi mpe nauli aende om
 
Je namsaidiaje? Kwanini Mungu huu mtihani kanidondoshea mimi?
Yakobo 1:13-14
[13]Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
Let no man say when he is tempted, I am tempted of God: for God cannot be tempted with evil, neither tempteth he any man:
[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
But every man is tempted, when he is drawn away of his own lust, and enticed.
 
Jiulize Kwanini bwanake amfukuze akiwa kwenye hali hiyo,, huyo atakua na shida sio bure....anyway kama umewiwa msaidie tu
Hata kama ana shida ila maadam anahitaji msaada basi asaidiwe tuu hiO shida zinawahusu yy na mumewe wewe toa msaada kama una uwezo
 
Lakini kwenye Biblia hiyo hiyo kuna story ambapo Mungu na shetani walikubaliana wamjaribu mtu fulani baada ya Mungu kusema hawezi tingishwa na shetani kusema akipata majanga atakengeuka tu.

Huyo ni mtumishi wa Mungu Ayubu, Mungu na shetani walicoraborate kumsurubisha jamaa ili kuipima imani ya Ayubu kwa Mungu wake, kifupi ni Kama walibet jamaa alisurubika ipasavyo Nenda kasome kitabu cha Ayubu utaenjoy Imani aliyokuwa nayo mwamba. Back to the topic, mkuu kwa namna yoyote whatever the chance you get to be helpful be awesome the world is full of disappointments be the hero.
 
Jiulize Kwanini bwanake amfukuze akiwa kwenye hali hiyo,, huyo atakua na shida sio bure....anyway kama umewiwa msaidie tu
Yaani kwenye mahusiano ya awali hakuiona shida, akaja kuìna baada ya kuishi na mwanamke kwa zaidi ya miezi saba?
 
Back
Top Bottom