Je! Mungu ni yule yule?

Kwanza mtoa mada Nakushauri kama unapenda sheria na kutawadha kuwa huru na hamia dini ya Uislam kama wewe sio muislamu ila ukiwa ni Muslim Jifunze elimu kwa bidii.
 
Wewe mwenye akili unaweza kuthibitisha mungu yupo?
Kwako wewe kuwepo au kutokuwepo kwa mungu hakubadilishi chochote kwako?kwa maana kwamba hata endapo ungepata uthibitisho kuwa mungu yupo je,kusingekuwa na tofauti yeyote kwako?
 
Kwako wewe kuwepo au kutokuwepo kwa mungu hakubadilishi chochote kwako?kwa maana kwamba hata endapo ungepata uthibitisho kuwa mungu yupo je,kusingekuwa na tofauti yeyote kwako?
Tofauti ingekuwa nimeweza kuthibitishiwa mungu yupo.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo? Hujajibu swali hili.
 
Ni hivi yesu alipokuja alishajitoa sadaka ya kuteketezwa pale msalabani ili wanadamu wote wakombelewe . soma kitabu cha yohana 1. 1 , palikuwepo neno naeneno alikuwa mungu wala hakikufanyika chochote bila yeye ukienda chini zaidi , nae neno akavaa mwili akashuka kwetu , kupitia kusulubiwa kwa yesu tulisha kombolewa,
 
Tofauti ingekuwa nimeweza kuthibitishiwa mungu yupo.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo? Hujajibu swali hili.
Kwa hiyo unakubali kuwa kutakuwa na tofauti endapo itathibitishwa kuwepo kwa mungu?
 
Kama tulishakombolewa makanisani tunafuata nini? Si tayari pepo inatusubili? Mnawaona kina Kiranga hamnazo lakini kuna hoja za msingi binadamu anapaswa kuzijuwa badala ya kuongozwa na imani tu, wake zetu tunaamini hawatoki nje ya ndoa lakini wapo wajanja wanaowavuwa chupi ila wewe imani yako unamla peke yako.

Suicide bomber anajazwa imani akijipuwa anakwenda peponi kuna mabikira 100 wanamngoja, lakini anashindwa kutumia logic ndogo tu ya kujihoji je Sheikh anayemjaza uongo huo hapendi pepo?
 
Hujatibitisha kwamba mungu yupo.
Tuanzie hapa, hivi unaamini kwamba kuna mwanzo wa ukoo wako? Kabla ya wazazi wako palikukwa na babu zako ambao pia walikuwa na babu zao na babu zao?
Kama jibu ni ndiyo, nini kinachokufanya uamini kwamba palikuwa na waanzilishi wa ukoo wako ambao hujawahi kuwaona??
Kama jibu siyo, then una logic behind what you believe.
 
Wanadamu huzaliwa kwa sexual reproduction inayohitaji wazazi wawili kukutana na kuzaa mtoto, hivyo ni wazi mimi nina wazazi na wao wana wazazi.

Habari ya mwanzo wa ukoo inabidi iwe defined vizuri zaidi. kwanza, ukoo ni nini, unaanzia wapi na kuishia wapi (scope)?

Unapimaje huyu ni mtu wa ukoo wangu na huyu si mtu wa ukoo wangu?

What is your point?
 
Ni sawa wanadamu tunatokana na hiyo sexual reproduction (kwa mujibu wa science)
Wale wazazi wa kwanza kabisa kabla ya hii sexual reproduction mwanzo wao nini?
 
Ni sawa wanadamu tunatokana na hiyo sexual reproduction (kwa mujibu wa science)
Wale wazazi wa kwanza kabisa kabla ya hii sexual reproduction mwanzo wao nini?
Kwa nini unafikiri kuna wazazi wa kwanza kabisa?
 
Kwa sababu kila kitu kina mwanzo.....
Basi hakuna mungu, kwa sababu naye atakuwa na mwanzo na chanzo chake kitakuwa na mwanzo, na chanzo cha chanzo chake kitakuwa na mwanzo. Ad infinitum, ad absurdia.

Mwanzo wa number line ni namba ngapi?
 
Basi hakuna mungu, kwa sababu naye atakuwa na mwanzo na chanzo chake kitakuwa na mwanzo, na chanzo cha chanzo chake kitakuwa na mwanzo. Ad infinitum, ad absurdia.

Mwanzo wa number line ni namba ngapi?
Tuzungumzie huyu binadamu ambaye tuna uhakika nae ambae uwepo wake hauna shaka,
Swali langu linarudi pale pale..huyu mwanzo wake ni nini?
 
Tuzungumzie huyu binadamu ambaye tuna uhakika nae ambae uwepo wake hauna shaka,
Swali langu linarudi pale pale..huyu mwanzo wake ni nini?

Kwanza kabisa.

Binadamu ni nani?

Unamjuaje huyu ni binadamu na huyu si dinadamu?
 
Kwanza kabisa.

Binadamu ni nani?

Unamjuaje huyu ni binadamu na huyu si dinadamu?
Unamtambua huyu ni binadamu kwa "intelligence power"
Tofauti na wanyama wengine binadamu ana uwezo mkubwa wa kutafakari na kuchambua mambo.
"A human being is an intelligence served by organs." Ralph Waldo Emerson
 
Unapimaje "intelligence power" ? Computer ikimzidi binadamu "intelligence power" computer hiyo itakuwa binadamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…