Kwanza Nikupongeze, Kwa Swali Lako Zuri Sana, Ambalo Linahitaji Ufafanuzi Ili Wengi Wapate Kujua Hukweli Juu ya Mtakatifu Wetu Yehova. Ambaye Tunamwabudu Kwa Ukamilifu Ndani ya Kristo Yesu.
1: MUNGU hajabadilika, ni Yeye Yule Jana Leo na Hata Milele.
2: Katika Taratibu za Agano la Kale Ibada Ilikuwa ni Sheria Katika Mwili. Soma Haya katika Kitabu Cha (Ebania 9🙂(Warumi 8🙂 Utaona Kwamba Watu walikua Wanajitaidi Kuosha Mwili ili Kumwabudu Mungu, Huku wakiacha Mioyo Yao Ikiwa Michafu, Soma (Marko 7:1-16) Ndiyo Maana Watu Wengi Walishindwa Kuwa watakatifu na kwenda Kwa Utakatifu Mbele za Mungu, Maana Utakatifu Utoka Moyoni na Sio Mwilini Kwa Kutawadha na Kuoga Soma (Yeremia 4:14) Mungu Anatuhusia Tuoshe Mioyo Yetu Tupate Kuokoka, na Siyo Mwili.
Sasa Yesu Alikuja Kuondoa Ibada Ya Mwilini Na Kuiamishia Ndani ya Mioyo Yetu, ili Kuleta Utakatifu Ndani Yetu, Ndiyo Maana Akatupa Roho Wake Mtakatifu Mioyoni Mwetu ili Atuongoze, Atufundishe, na Kutusaidia Kwenda Kwa Ukamilifu Mbele Zake. (Warumi 8:8)
Hivyo Basi Imetupasa Kumwabudu Mungu Katika Roho na Siyo Katika Mwili, Ndiyo Maana Mungu Alimtuma Yesu Aje Kulifunua Agano Jipya Ili Kila Atakaye Mwanini Yesu Ahesabiwe Haki Pasipo matendo ya Sheria Bali Katika Roho, na Yesu Ndiye Mwanzilishi wa Ibada Ya Rohoni nasi Katika Mwili (Yoh 4:22-24)
Hivyo Basi ni Lazima Kila Mwanadamu Azaliwe Mara ya Pili Kwa Kumwamini Yesu, na Kumpokea Roho Wake Soma Haya Kwa Undani Kabisa Kwenye Kitabu Cha Warumi 8:
Mbarikiwe sana Nyote Mlio Soma Haya na Mungu Kupitia Roho Mtakatifu Awafunulie Siri Hii ili Kila Asomaye Ahanze Kumwabudu Mungu Katika Roho na Kweli.