Mheshimiwa
Kiranga,
Naomba kwanza nikusalimu kisha nianze kuzua hoja.
Swali langu la kwanza ni kwanini wasema kuwa Mungu hayupo maana ili uweze kusema kuwa kitu hakipo lazima uwe umekitafuta na kukikosa kwa mfano una box na ndani ya hilo box palitakiwa pawe na pipi ukija na kuchungulia ndani ya box na ukakuta hamna pipi hata moja utasema kuwa hamna pipi ndani ya box yaani pipi
hazipo. Vivyo hivyo kwenye nyumba ili tuseme kuwa panya hayupo kwenye hii nyumba inatubidi tuwe tumeshakagua nyumba nzima na kuthibitisha kuwa hamna panya.
Swali kwako ni
je umeshakagua dunia yote na kuthibitisha kuwa Muumba hayupo?
Na kama la basi waweza vipi kusema hayupo?
Swali lako nimelijibu mara kadhaa hapo juu na kama ningekuwa katika hali ya kuku dismiss, ningekwambia tu soma hapo juu.
Ila kwa kuwa umenionesha taadhima kubwa, na mimi nina tabia ya kurudisha taadhima kwa taadhima, nitachukua muda kujibu tena.
Sihitaji kukagua magunia yote ya mchele kujua kwamba punje moja ya mcheleukiijumlisha na punje nyingine ya mchele unapata punje mbili za mchele.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo na wala sihitaji kukagua dunia nzima ili kujua hayupo.
Nahitaji kukagua mantiki ya kuwepo kwake.
Mantiki ya kuwepo kwake ina contradiction. Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe kabla haijapingwa na mtu.
Upande mmoja tunaambiwa Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote.
Upande wa pili, tunaona Mungu huyu anasemwa kaumba ulimwengu huu unaoruhusumaovu mengi kuwezekana, kinyume na asili za Mungu huyo aliyetajwa za uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Kujipinga huku kunakuja na habari ya kwamba, imekuwaje Mungu mwenye kila sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani (ana uwezo wote, kwahiyo suala lakukosa uwezo halipo, ana ujuzi wote, kwa hiyo suala la kukosa ujuzi halipo, ana upendo wote, kwa hiyo sualala kukosa upendo halipo) hakuumba ulimwengu huo?
Sijajibiwa swalihili.
Swali linaonesha Mungu huyu hana logical consistency. Ana contradiction.
Contradiction inaonesha uongo katika dhana ya kuwepo kwa Mungu huyu.
Mungu huyu hayupo.