Joseph lebai
JF-Expert Member
- Jul 19, 2017
- 8,452
- 8,670
Kila rangi ina Mungu wake, ila Waafrika tunampuuza Mungu wetu na kujikita kwa Mungu wa wazungu. Atakuwaje yuleyule na dini utitiri? Chungana na Mungu wako kulingana na imani yako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja nikupe concept ya kibinadamu tu maana najua wewe mbishani sana,
Mimi ninaamini mungu yupo wewe huamini kama yupo, sasa endapo tukifika kweli uko mbinguni na kumkuta yupo kweli mimi nitapata faida wewe utapata hasara, lakini tukimkuta hayupo kweli sisi wote hakuna atayepata faida wala hasara.
Sasa hii inamaanisha kuwa sisi tuna advantage katika kuamini yupo rakini wewe hakuna faida yoyote ukijiukiza ukichambua concept hii vizuri kama anayo akili timamu utapata jibu
Na Mimi namkubali sana huyu jamaa ila naamini kwamba Mungu muumba mbingu na nchi yupoKiranga anaweza aonekane mkorofi na wengine kumchukia kabisa kwa misimamo yake. Haiendi hivyo, iko hivi, kama Mungu anajulikana na kufahamika kwa imani, tayari imeshapishana na kanuni anazosimamia huyu jamaa, yeye anataka kitu uthibitisho, aone, ashike, aguse, ajiridhishe kabisa. Binafsi sioni kosa lake. Nikimchukia kwa yeye kutokuamini uwepo wa Mungu ni kuonyesha hitilafu kwenye uelewa.
Lakini hata kwenye maandiko ya hiyo Biblia, kuna mtu aliitwa Tomas, yeye licha ya kuambiwa kwamba Yesu amefufuka, alibisha hata baada ya kumuona aligusa alama za makovu ya misumari. Imani ni jambo la mtu binafsi, hakutaka kwenda kwa mkumbo. Kwanini tuone Kiranga ni wa ajabu kwa kutaka uthibitisho.
Binafsi naamini uwepo wa Mungu, narudia tena, Naamini uwepo wa Mungu lakini jaijawahi kunifanya nikorofishane au kuzongana na Kiranga.
Simjui uyo uliyemtaja nasijaipata hii concept kwake ndio kwanza namsika Leo ila sio cha msingi.Hii concept inaitwa "Pascal's Wager". Nimeisomasana, nimeichambua sana, nimeona udhaifu wake sana.
Kimsingi,imejengwa katika uvivu wa kujifikirisha,na kuamua kucheza kamali kizembe.
Kwa nini?
Unacheza kamali maisha yako kwa mambo ambayo hayahitaji kucheza kamali, yanahitaji uchunguzi.
Ujinga wa Pascal's wager ni pale inaposema "tukifikakweli huko mbinguni na kumkuta yupo kweli mimi nitapata faida wewe utapata hasara, lakini tukimkuta hayupo kweli sisi sote hakuna atakayepata faida wala hasara".
Ukweli ni kwamba, ukiamini Mungu ambaye hayupo, wala huhitaji kusubiri mbinguni ili uanze kupata hasara.
Hasara unaipata hapa hapa duniani.
Kivipi?
1. Unaishi kwa kupangiwa na wengine jinsi ya kuishi. Mzungu atataka watumwa kutoka Africa, atatumia mistari ya Biblia kuhalalisha biashara ya utumwa (Biblia imebariki utumwa na kusema watumwa wawe watii kwa bwana zao). Wewe utakubalikuwa mtumwa kwa kuamini hayoni maagizo ya Mungu, na ukifa utaenda peponi kwa sababu umetii maagizoya Mungu. Huuni ujinga. Mtu ambaye haamini ujinga wa kuamini vitabu vya Mungu atapinga unyama wa utumwa na kujikomboa.
2. Kuamini sana Mungu kunajenga utamaduni wa uvivu, alhamdullilah, bwana ametoa bwana ametwaa, kutokuwa na uchunguzi. Mvua zikiacha kunyesha kwa sababu za kiasili tu, watu wanakata miti, watu wanaoendekeza kuamini sana Mungu badala ya kufanya uchunguzi kujua chanzo ni nini, watawahi kwenda misikitini na makanisani kuomba Mungu ambaye hayupo. Matokeo yake muda ambao walitakiwa kupanda mitina kujifunza mazingira wanautumiakanisani na misikitini kuomba Mungu. Wanaendelea kukata miti, nchi inazidi kuwa jangwa. Imani yao ya Mungu inawaponza. Wasioamini kuwepo Mungu wanajua kwamba hakuna Mungu hivyo hawamuombi Mungu, wanasoma mazingira na kuyakabili wao wenyewe.
3. Mtu anaweza kuacha kwenda hospitali na kunywa dawa kwa kuamini kwamba atapona akiombewa na watu wa Mungu. Bilakuangalia matatizo ya afya kiasili zaidi na kutafuta tiba zinazoeleweka za afya. Mtu huyu hata akifariki, hakuna atakayestukana kusema Mungu kashindwa kumponya hata baada ya maombi, watu watasema tu "kazi ya Mungu haina makosa". Hata kufanya post mortem kujua chanzo cha kifo watu wanaoamini Mungu sana ni shida, wanaona nikamakutakakumkosoa Mungu. Hapo maendeleo ya tiba yanadumazwa.
4. Kifusi kilipoanguka Arusha kwenye machimbo ya Tanzanite, alienda rais Kikwete akaishia kusema "kazi ya Mungu haina makosa". Hakuongelea kuhusu kuboresha miundombinu, kuanzisha bima za maisha,kuboresha elimu kwa wachimbaji, kuweka sheria kali kuzuia uchimbaji holela. Huu utamaduni wa "kazi ya Mungu haina makosa" unadumaza maendeleo ya nchi nzima kama watu watauendeleza.
Hiyo mifano michache ya haraka haraka tu jinsi gani imani ya Mungu inavyoweza kuleta hasara hapa hapa duniani kabla hata ya kwenda mbinguni.
Hii concept inaitwa "Pascal's Wager". Nimeisomasana, nimeichambua sana, nimeona udhaifu wake sana.

Mimi ni libertarian.Unachokisema kina ukweli kiasi flani. Kwangu sipo kwenye kundi hata moja kati ya wanaofaidika na hizo hasara mkuu.
Mambo ni mepesi sana, kyamini au kutokuamini kwamba Mungu yupo sio ugonjwa wala sio kasoro, ila pale imani hiyo inapokufanya uanze kuishi maisha yasiyo na maana inakua ujinga na hasara.
Wote tunapata mvua ile ile, hewa ileile, tunakufa, tunaugua, tunaajiriwa kwa vigezo vya elimu na uzoefu wa kazi na taaluma.
Hiyo ndio sababu kubwa inanifanya nisigombane au kubishana kuhusu uwepo wa Mungu.
Mwisho, kama yupo, ni juu yake kujitetea na kuthibitisha uwepo wale. Naheshimu na kuthamini maoni, mitazamo na imani za wengine hata kama sikubaliani nazo.
Mimi ni libertarian.
Napenda uhuru. Watu wawe huru. Kuishi huru. Kufanya biashara huru. Kuamini huru.
Hata mambo yanayosemwa ni ya dini za kishenzi, au za Mu gu ambaye hayupo, yanaweza kuwa na maana sana. Mambo ya dini yamejaa allegory, mutholigy na busara nyingi mahali pengine. Hata kama Mungu hayupo naweza kuelewa kwa nini watu wanahitaji dini. Hiki halinifanyi niseme Mungu yupo.
Mathalani. Kuna dini nyingi sana za asili, hata huku Africa tulikoitwa bara la giza, zenye kanuni nyingi nzuri za kutoua wanyama bila sababu, kutokata miti. Nitatoa mbili hizo tu kama mfano. Sasa Waafrika wamefanya haya mambo kwa miaka na miaka, maelfu kwa maelfu. Mtu anayechukulia dini literary atasema hawa watu washenzi. Wanaabudu miti na wanyama.
Lakini juna upande wa piki wa uchambuzi wa dini kama hizi. Mtu anaweza kusema dinibza kuabudu miti na kukataza usikatwe ovyo zinesaidia ju naibtain ecoligical balance na kuhifadhi mazingira. Siku hizi tumeziacha na hii ni moja ya sababu ukataji miti hilela umeongezeka na mvua zinaweza kukosekana baadhi ya maeneo. Uuaji hokela wa wanyama umeharibu ecological cycle. Watu wanasoma sayansi wanaona hatari za pool of species kuwa reduced, endangered species kuongezeka, au hata unnatural imbalance ya mating populatiin katika wanyama fulan. Mambo haya haya yakisemwa na wazungu/wasomi tunasikliza na kusema yana maana, lakini tukimkuta babu anakataa mti wake usikatwe tunasema mshenzi anaabudu mti.
Kwa hiyo mimi natetea uhuru wa watu kuabudu. Lakini pia, uhuru wa kuabudu kwa kiasi kikubwa ni kitu cha faragha. Ukiabudu kwako, kanisani kwako, msikitinibkwako sawa. Ukianzisha mjadala JF kujadili uwepo wa Mungu, halafu ukaniambia mti wa Mbuyu ni Mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wite na upendo wite, nitakupinga sana.
Kwa maana utakuwa umeshaingilia dini yangu ya kutafuta ukweli kwa uchunguzi.
Kwa hiyo mtu akisema keo Tanzania inepiga marufuku wanaoabudu miti, nitapinga habari hiyo na kusema hawa watu wana haki ya kikatiba Tanzania na pia kimataifa wanatetewa na Universal Deckaration if Human Rights iliyopitishwa December 10 1948 kama sikosei, na Tanzania tumetia sahihi kulikubali Azimio hili zuri sana.
Nitaitetea imani hii. Uburu wa kuabudu si kitu cha kuchezea.
Lakini mtu wa imani hii akija hapa kimujadili na kusema mti wa kwao ni Mungu, nitampinga vikali sana kwa facts.
Sahihisho.Kiranga anaweza aonekane mkorofi na wengine kumchukia kabisa kwa misimamo yake. Haiendi hivyo, iko hivi, kama Mungu anajulikana na kufahamika kwa imani, tayari imeshapishana na kanuni anazosimamia huyu jamaa, yeye anataka kitu uthibitisho, aone, ashike, aguse, ajiridhishe kabisa. Binafsi sioni kosa lake. Nikimchukia kwa yeye kutokuamini uwepo wa Mungu ni kuonyesha hitilafu kwenye uelewa.
Lakini hata kwenye maandiko ya hiyo Biblia, kuna mtu aliitwa Tomas, yeye licha ya kuambiwa kwamba Yesu amefufuka, alibisha hata baada ya kumuona aligusa alama za makovu ya misumari. Imani ni jambo la mtu binafsi, hakutaka kwenda kwa mkumbo. Kwanini tuone Kiranga ni wa ajabu kwa kutaka uthibitisho.
Binafsi naamini uwepo wa Mungu, narudia tena, Naamini uwepo wa Mungu lakini jaijawahi kunifanya nikorofishane au kuzongana na Kiranga.
Samahani mkuu,Tofauti ipo.
Hakuna mjadala kwamba watu wapo. Au unabisha?
Kuna mjadala kama mungu yupo.
Ukisema maneno haya yaameandikwa na watu, hilo halihitaji kuthibitishwa, hatuhitaji kuthibitisha kwamba watu wapo.
Tunahitaji kuthibitisha mungu yupo maana haonekani, haeleweki, wazo la kuwepo kwake linajipinga lenyewe.
Utasemaje mawili haya ni sawa?
Sahihisho.
Square root ya 2 ukiizidisha jwa square roit ya 2 katika base ten math utapata 2.
Square roit ya 2 sijawahi kuiona, kuishika, kuinusa, kuisikia sauti yake wala kuionja ladha yake.
Ninetumia mlango wa akili kuijua.
Na mtu atakayeniambia square root ya 2 ni 10 nitamkatalia. Kwa sababu jibu hilo lina contradiction.
Hata Mungu naye si kazima kumuona, kumsikia, kumgusa, kumuonja au kumnusa ili ujue yupo.
Unaweza kumdadisi kwa mlango wa akili tu, ukaona hili suala la Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuwepo, ni sawa sawa kabisa na like suala la "square root of 2 =10".
Yote ni uongo.
Yote yana contradiction.
Kwa hiyo hapa ni mambo ya kutumia akili tu, si lazima utumie five senses.
Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
Kuna mengi tu umeyapata kutoka kwa watu ambao hata huwajui.Simjui uyo uliyemtaja nasijaipata hii concept kwake ndio kwanza namsika Leo ila sio cha msingi.
Cha msingi kwamba kama umeweza kupinga concept hii ambayo inaihitaji uwelewa wa kibinadamu tu naishia hapa.
Hapa sasa unataka kuchanganya madawa kaka. Anzisha thread tofauti halafu ni tag.Maelezo mujarab Kiranga . Hayo mambo tuyaache kama ambavyo mtu anaamua kuwa shabiki wa timu ya mpira, ilimradi athiathiri wala kubughudhi wengine.
Naomba nipe mtazamo na maoni yako kuhusu ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Stieglers Gorge ambapo kuna makadirio ya kuzalisha 2,100 MW.
Unafahamu logical consistency ni nini?Niliwahi kusema vitu vingi tunaanza kwa kuamini kisha inafuatiwa na kuelewa au uthibitisho. Tatizo kuhusu Mungu, msingi wake mkuu umejikita kwenye imani na tafsiri ya imani iko wazi. Hapo ndio imekua mjadala mzito kuhusu hili kambo mara zote.
Ni kweli hizo squre root haujawahi kuziona lakini kuna watu wametueleza zipo. Hali kadhalika akitokea mtafiti au mtaalamu mwingine akaja na hoja kwamba binadamu alitokana na magome ya miti, akaweza kutetea hoja yake kwa kuthibitisha itaaminika na kufundishwa hivyo.
Kumekuwepo ongezeko la tafiti zinazoendeleza au kuibua mambo mapya kabisa na kubadili uelewa au nadharia zilizokuwepo awali. Hata hizo square root tunaziamini tu.
Linapokuja suala la imani kuhusu Mungu, hauwezi kuingia maabara, hauwezi kuchukua viniti ukavirusha juu ukasema vikiyeyuka yupo, vikirudi chini hayupo.
Hapa sasa unataka kuchanganya madawa kaka. Anzisha thread tofauti halafu ni tag.
Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
Unaelewa kwamba unresolved contradiction inaonesha uongo?Naelewa mkuu. Inategemea unahitajika uelewa wa kuwango gani.
Unaelewa kwamba unresolved contradiction inaonesha uongo?
ukiambiwa umuonyeshe kwa watu bila kutumia biblia/maandiko utaweza?..let assume umeenda sehemu hawajui kusomaSisi tunaoamini kuwa Mungu yupo tunatumia imani.