Je! Mungu ni yule yule?

Kila rangi ina Mungu wake, ila Waafrika tunampuuza Mungu wetu na kujikita kwa Mungu wa wazungu. Atakuwaje yuleyule na dini utitiri? Chungana na Mungu wako kulingana na imani yako
 

Hii concept inaitwa "Pascal's Wager". Nimeisoma sana, nimeichambua sana, nimeona udhaifu wake sana.

Kimsingi, imejengwa katika uvivu wa kujifikirisha, na kuamua kucheza kamali kizembe.

Kwa nini?

Unacheza kamali maisha yako kwa mambo ambayo hayahitaji kucheza kamali, yanahitaji uchunguzi.

Ujinga wa Pascal's wager ni pale inaposema "tukifika kweli huko mbinguni na kumkuta yupo kweli mimi nitapata faida wewe utapata hasara, lakini tukimkuta hayupo kweli sisi sote hakuna atakayepata faida wala hasara".

Ukweli ni kwamba, ukiamini Mungu ambaye hayupo, wala huhitaji kusubiri mbinguni ili uanze kupata hasara.

Hasara unaipata hapa hapa duniani.

Kivipi?

1. Unaishi kwa kupangiwa na wengine jinsi ya kuishi. Mzungu atataka watumwa kutoka Africa, atatumia mistari ya Biblia kuhalalisha biashara ya utumwa (Biblia imebariki utumwa na kusema watumwa wawe watii kwa bwana zao). Wewe utakubali kuwa mtumwa kwa kuamini hayo ni maagizo ya Mungu, na ukifa utaenda peponi kwa sababu umetii maagizo ya Mungu. Huuni ujinga. Mtu ambaye haamini ujinga wa kuamini vitabu vya Mungu atapinga unyama wa utumwa na kujikomboa.

2. Kuamini sana Mungu kunajenga utamaduni wa uvivu, alhamdullilah, bwana ametoa bwana ametwaa, kutokuwa na uchunguzi. Mvua zikiacha kunyesha kwa sababu za kiasili tu, watu wanakata miti, watu wanaoendekeza kuamini sana Mungu badala ya kufanya uchunguzi kujua chanzo ni nini, watawahi kwenda misikitini na makanisani kuomba Mungu ambaye hayupo. Matokeo yake muda ambao walitakiwa kupanda miti na kujifunza mazingira wanautumia kanisani na misikitini kuomba Mungu. Wanaendelea kukata miti, nchi inazidi kuwa jangwa. Imani yao ya Mungu inawaponza. Wasioamini kuwepo Mungu wanajua kwamba hakuna Mungu hivyo hawamuombi Mungu, wanasoma mazingira na kuyakabili wao wenyewe.

3. Mtu anaweza kuacha kwenda hospitali na kunywa dawa kwa kuamini kwamba atapona akiombewa na watu wa Mungu. Bila kuangalia matatizo ya afya kiasili zaidi na kutafuta tiba zinazoeleweka za afya. Mtu huyu hata akifariki, hakuna atakayestuka na kusema Mungu kashindwa kumponya hata baada ya maombi, watu watasema tu "kazi ya Mungu haina makosa". Hata kufanya post mortem kujua chanzo cha kifo watu wanaoamini Mungu sana ni shida, wanaona ni kama kutaka kumkosoa Mungu. Hapo maendeleo ya tiba yanadumazwa.

4. Kifusi kilipoanguka Arusha kwenye machimbo ya Tanzanite, alienda rais Kikwete akaishia kusema "kazi ya Mungu haina makosa". Hakuongelea kuhusu kuboresha miundombinu, kuanzisha bima za maisha, kuboresha elimu kwa wachimbaji, kuweka sheria kali kuzuia uchimbaji holela. Huu utamaduni wa "kazi ya Mungu haina makosa" unadumaza maendeleo ya nchi nzima kama watu watauendeleza.

Hiyo mifano michache ya haraka haraka tu jinsi gani imani ya Mungu inavyoweza kuleta hasara hapa hapa duniani kabla hata ya kwenda mbinguni.
 
Na Mimi namkubali sana huyu jamaa ila naamini kwamba Mungu muumba mbingu na nchi yupo
Siwezi kumchukia kiranga kwa kile akiaminicho
 
Simjui uyo uliyemtaja nasijaipata hii concept kwake ndio kwanza namsika Leo ila sio cha msingi.

Cha msingi kwamba kama umeweza kupinga concept hii ambayo inaihitaji uwelewa wa kibinadamu tu naishia hapa.
 

Unachokisema kina ukweli kiasi flani. Kwangu sipo kwenye kundi hata moja kati ya wanaofaidika na hizo hasara mkuu.

Mambo ni mepesi sana, kyamini au kutokuamini kwamba Mungu yupo sio ugonjwa wala sio kasoro, ila pale imani hiyo inapokufanya uanze kuishi maisha yasiyo na maana inakua ujinga na hasara.

Wote tunapata mvua ile ile, hewa ileile, tunakufa, tunaugua, tunaajiriwa kwa vigezo vya elimu na uzoefu wa kazi na taaluma.

Hiyo ndio sababu kubwa inanifanya nisigombane au kubishana kuhusu uwepo wa Mungu.

Mwisho, kama yupo, ni juu yake kujitetea na kuthibitisha uwepo wale. Naheshimu na kuthamini maoni, mitazamo na imani za wengine hata kama sikubaliani nazo.
 
Mimi ni libertarian.

Napenda uhuru. Watu wawe huru. Kuishi huru. Kufanya biashara huru. Kuamini huru.

Hata mambo yanayosemwa ni ya dini za kishenzi, au za Mungu ambaye hayupo, yanaweza kuwa na maana sana. Mambo ya dini yamejaa allegory, mythology na busara nyingi mahali pengine. Hata kama Mungu hayupo naweza kuelewa kwa nini watu wanahitaji dini. Hili halinifanyi niseme Mungu yupo.

Mathalani. Kuna dini nyingi sana za asili, hata huku Africa tulikoitwa bara la giza, zenye kanuni nyingi nzuri za kutoua wanyama bila sababu, kutokata miti. Nitatoa mbili hizo tu kama mfano. Sasa Waafrika wamefanya haya mambo kwa miaka na miaka, maelfu kwa maelfu. Mtu anayechukulia dini literary atasema hawa watu washenzi. Wanaabudu miti na wanyama.

Lakini kuna upande wa pili wa uchambuzi wa dini kama hizi. Mtu anaweza kusema dini za kuabudu miti na kukataza usikatwe ovyo zimesaidia jk maintain ecological balance na kuhifadhi mazingira. Siku hizi tumeziacha na hii ni moja ya sababu ukataji miti holela umeongezeka na mvua zinaweza kukosekana baadhi ya maeneo. Uuaji holela wa wanyama umeharibu ecological cycle. Watu wanasoma sayansi wanaona hatari za pool of species kuwa reduced, endangered species kuongezeka, au hata unnatural imbalance ya mating population katika wanyama fulani. Mambo haya haya yakisemwa na wazungu/wasomi tunasikliza na kusema yana maana, lakini tukimkuta babu anakataa mti wake usikatwe tunasema mshenzi anaabudu mti.

Kwa hiyo mimi natetea uhuru wa watu kuabudu. Lakini pia, uhuru wa kuabudu kwa kiasi kikubwa ni kitu cha faragha. Ukiabudu kwako, kanisani kwako, msikitini kwako sawa. Ukianzisha mjadala JF kujadili uwepo wa Mungu, halafu ukaniambia mti wa Mbuyu ni Mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wote na upendo wote, nitakupinga sana.

Kwa maana utakuwa umeshaingilia dini yangu ya kutafuta ukweli kwa uchunguzi.

Kwa hiyo mtu akisema leo Tanzania imepiga marufuku wanaoabudu miti, nitapinga habari hiyo na kusema hawa watu wana haki ya kikatiba Tanzania na pia kimataifa wanatetewa na Universal Declaration of Human Rights iliyopitishwa December 10 1948 kama sikosei, na Tanzania tumetia sahihi kulikubali Azimio hili zuri sana.

Nitaitetea imani hii. Uhuru wa kuabudu si kitu cha kuchezea.

Lakini mtu wa imani hii akija hapa kujadili na kusema mti wa kwao ni Mungu, nitampinga vikali sana kwa facts.
 

Karibu tena tuwaelimishe hawa watu kuhusu uhalisia
 
Maelezo mujarab Kiranga . Hayo mambo tuyaache kama ambavyo mtu anaamua kuwa shabiki wa timu ya mpira, ilimradi athiathiri wala kubughudhi wengine.

Naomba nipe mtazamo na maoni yako kuhusu ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Stieglers Gorge ambapo kuna makadirio ya kuzalisha 2,100 MW.
 
Sahihisho.

Square root ya 2 ukiizidisha kwa square root ya 2 katika base ten math utapata 2.

Square root ya 2 sijawahi kuiona, kuishika, kuinusa, kuisikia sauti yake wala kuionja ladha yake.

Nimetumia mlango wa akili kuijua.

Na mtu atakayeniambia square root ya 2 ni 10 nitamkatalia. Kwa sababu jibu hilo lina contradiction.

Hata Mungu naye si kazima kumuona, kumsikia, kumgusa, kumuonja au kumnusa ili ujue yupo.

Unaweza kumdadisi kwa mlango wa akili tu, ukaona hili suala la Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuwepo, ni sawa sawa kabisa na like suala la "square root of 2 =10".

Yote ni uongo.

Yote yana contradiction.

Kwa hiyo hapa ni mambo ya kutumia akili tu, si lazima utumie five senses.
 
Samahani mkuu,
Kwahiyo kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba kila ambacho hakionekani hakipo.
 

Niliwahi kusema vitu vingi tunaanza kwa kuamini kisha inafuatiwa na kuelewa au uthibitisho. Tatizo kuhusu Mungu, msingi wake mkuu umejikita kwenye imani na tafsiri ya imani iko wazi. Hapo ndio imekua mjadala mzito kuhusu hili kambo mara zote.

Ni kweli hizo squre root haujawahi kuziona lakini kuna watu wametueleza zipo. Hali kadhalika akitokea mtafiti au mtaalamu mwingine akaja na hoja kwamba binadamu alitokana na magome ya miti, akaweza kutetea hoja yake kwa kuthibitisha itaaminika na kufundishwa hivyo.

Kumekuwepo ongezeko la tafiti zinazoendeleza au kuibua mambo mapya kabisa na kubadili uelewa au nadharia zilizokuwepo awali. Hata hizo square root tunaziamini tu.

Linapokuja suala la imani kuhusu Mungu, hauwezi kuingia maabara, hauwezi kuchukua viniti ukavirusha juu ukasema vikiyeyuka yupo, vikirudi chini hayupo.
 
Simjui uyo uliyemtaja nasijaipata hii concept kwake ndio kwanza namsika Leo ila sio cha msingi.

Cha msingi kwamba kama umeweza kupinga concept hii ambayo inaihitaji uwelewa wa kibinadamu tu naishia hapa.
Kuna mengi tu umeyapata kutoka kwa watu ambao hata huwajui.

Unaweza kubaa cheni ya dhahabu ukafikiri umeioenda wewe dhahabu, kumbe dhahabu imechaguliwa kuwa kitu cha thamani tangu enzi za Wasumaria.

Kwa habari zaidi kuhusu Pascal's Wager, Wikipedia page yake hii hapa.

Pascal's Wager - Wikipedia

Tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba tunajadiliana vitu kwa kutofautiana upeo.

Wewe unataja Pascal Wagwr hata huijui kama hii ni Pascal Wager.

Mimi nishaisoma kipindi kirefu sana, nimesoma watetezi wake, nimesoma walioonyesha udhaifu wake, nimesoma mpaka hesabu za Pascal. Miaka 24 iliyopita.

Halafu keo unanidharau eti sinaielewa Pascal's Wager, wakati hata criticism yangu hujaijibu.

Nikikwambia mimi ni Mungu, nioe mshahara wako wote kila mwezi, na ukifa ukienda mbinguni ukakuta mimi si Mungu utakuwa hujapata hasara, lakini ukikuta mimi ni Mungu utapata faida sana, utakubali?

Kwanza Pascal's Wager hata hau address tatuzo la kwamba, hata ukikubali Mungu yupo, hujajihakikishia utapata faida mbinguni.

Unaweza kumkubali Mungu wa Wakristo, ukaenda mbinguni ukakuta Mungu wa Wakristo ni wa uongo. Mungu wa ukweli ni wa Mayan Civilization.

Hapo hata hiyo Pascal Wager yako haikusaidii.

Ndiyo maana mimi naona badala ya kucheza kamali ya kizembe, shuvhukisha kichwa chako ujue ukweli.

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
 
Hapa sasa unataka kuchanganya madawa kaka. Anzisha thread tofauti halafu ni tag.
 
Unafahamu logical consistency ni nini?

Sent from my LGLS992 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…