Je! Mungu ni yule yule?

Samahani mkuu,
Kwahiyo kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba kila ambacho hakionekani hakipo.
Muziki hauonekani na upo.

Dhana ya Mungu kuwapo inapingwa kwa sababu haina logical consistency, ina contradiction.

Sio kwa sababu Mungu haonekani.
 
Kiranga na ujanja wako wote...nimekutupa kwny shimo kwa iyo avatar yako ivi nawewe unaamini kweli mifumo ya garax(planet)...


Unakula MATANGO PORI YA CGI..@[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwa kuongezea tu atheist tunaamini ya kuwa dini ni kipimo cha ufikiri,na pia dini ni dhana ya kuwaweka watu mahala salama(tulivu),...


ninyi endapo kila mmoja wenu atajitambu(ni ngumu kuwezekanadunia itagubikwa na fujo sana na matendo machafu zaidi kutawala....AMINI HIVI WEWE NI WW AKUNA KAMA WW.....mtu ni OWN UNIVERSAL....


dunia ni mithili ya nyumba ghorofa tunavyoamini sisi...PIA TUNAAMINI HAKUNA DHAMI NA HAKUNA MUNGU WALA MIUNGU.....


mungu kama ni mwenye utukufu na mwema ilikuwa vigumu yeye kuumba ubaya duniani....bibilia ni kitabu cha majaribio ya fikira zenu naweza ita,ama nadiliki taja ni ulaghai...(hamtanielewa wala sitaeleweka)...


Tunachopaswa kuweza fanya ni kuwa na utayar wa ww kuwa na mapokeo tofaut na uliyokuzwa na au sumu uliyokuzwa nayo kuitemaa eee KUITEMAA[emoji23] [emoji23] [emoji23] nacheka kama mazuri...eee uiteme maana hapo ulipo ni kama robot vile wanavyolicontroll...


Wewe kiranga nawe huna tofaut na unaobishana nao tena bora ya wenzako kuliko ww unaeamini uwepo wa garax....,ni hayo tu wakuu ila si kila mtu na IMANI YAKE?,wacha tusonge...
 

A proposition can be logically true but not sound. Unaposema "pembe Sita kwenye tatu" nilikuambia ni sawa na kutaka nikuoneshe mwanamke anayetaga mayai.

Biblia inapotaja habari za shetani haitaji asilia kwamba alikuwa malaika mwovu. Neno shetani ni sawa na neno "mpinzani" au "adversary," hata Petro aliambiwa hivo pia alipopinga shauri la Mungu (Math. 16:23).

Unachanganya mada nyingi ktk sefuria moja; wakati mwingine inakuwa vigumu kukujibu. Labda hiyo ndiyo akili nyingi au what is called "because you don't know it might be true."
 
Mungu aliweza au alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na shetani au uovu wowote?
 
Binaadamu ni waoga. Wana hofu kuhusu hatima yao baada ya maisha ya hapa duniani. Hawajui ni kipi kitafuata baada ya hapo. Pia wanastaajabu kila kitu kilichopo. Mipangilio ya galaxy na kila kitu kilichoo, mifumo mbali mbali ya miili yao, namna dunia inasapoti maisha, kila kitu kipo katika mpangilio ambao ukibadirika tu huenda maisha yasiwezekane tena.

Binaadamu anatazama mifumo yote iliyopo na kustaajabu sana maana imepangiliwa katika namna ya pekee hivyo anahitimisha kuwa lazima yupo au kipo kilichoiweka hiyo mifumo katika umakini huo.

Na kutokana na hilo binaadamu anaamini kuwa huyo au hicho kilichoweka mifumo hiyo ndicho chenye mamlaka ya kila kitu. Hii ni imani sasa. Na binaadamu anahisi ana deni kwa huyo/hicho kilichoweka mifumo hii. Binaadamu anajaribu kumuelewa huyo/hicho kilichoweka hii mifumo na ndio idea ya mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote, mwenye upendo wote inapokuja! Hii idea kazitengeneza mwanadamu mwenyewe na ndio maana zinajichanganya sana. Binaadamu kaandika vitabu vinavyojipinga vyenyewe kujaribu kuelezea hiyo idea ya mungu. Uongo uongo umekuwa mwingi sana. Watu wanajazana hofu (mfano kuhusu moto wa milele) wanasema hiyo mamlaka (kujaza watu hofu) wamepewa na mungu sasa huyo mungu kweli anapata maslahi gani kwa kuchoma watu wake moto? Maana yeye alikuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu asiyetenda dhambi (maana yeye ana uwezo wote) ila kwa mapenzi yake akamuumba mwanadamu ambaye anaweza kutenda dhambi. Sasa katika hili unaona idea ya moto ni uonevu kwa mwanadamu, Je mungu ni muonevu?

Ila atakuwa muonevu maana pia ni mbaguzi anasema taifa teule ni Israeli. Huyu mungu ana sifa za kibinaadamu nyingi sana maana katokana na idea ya mwanadamu.

Naamini kuna nguvu fulani (mungu?) iliyoumba kila kitu ila bado hatujafanikiwa kuijua. Mungu yupo ila si huyu anayeelezewa kwenye vitabu maana huyu haeleweki. Mungu hatumjui, hatujui anataka nini, hatujui lolote maana yeye hajataka tumjue. Angetaka wala kusingekuwa na mjadala kuwa yupo au hayupo bali angejidhihirisha pasina shaka yoyote kwetu. Kwani kuna mjadala kuwa jua lipo au halipo? Ni kwa kuwa limedhihirika, na mungu naye angejidhihirisha basi tusingekuwa na akina Kiranga
 
Nimejifunza mengi sana kupitia hili bandiko Pongezi kwa wakuu wote kwa michango yenu yenye tija kulingana na mada husika,ila mkuu Kiranga heshima kwako bado najifunza mengi kupitia wewe.
 
Hongera sana mleta mada nimejitahi kufatilia hii mada kwasababu kuna maswali mengi huwa najiuliza bila kupata jibu lakini sasa kidogo nimeanza kupata mwanga kidogo naendelea kufatilia labda nitapata jibu huko mbele heshima kwako Kiranga.
 


Unaongea ujinga soon utakua mpumbavu! Me sijawai kumuona Mungu ktk sura yake na hii ni kutokana na matokeo ya dhambi ila nakuhakikishia nimemuona Mungu kupitia matendo yake! wapo watu wanashuhuda mbalimbali ila kwa mtizamo wako huo wa kijinga utataka mabishano. Ukitaka nithibitishe juu ya uwepo wa Mungu nitafute, historia yangu tu inadhihirisha uwepo wa Mungu.
 
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao dhambi inawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani?

Hujajibu swali hili.

Ujinga ni kukubali kuwepo kwa huyo Mungu bila kuweza kujibu swali hili.
 
Anataka umthibitishie uwepo wa MUNGU kwa jinsi anavyotaka yeye, sio kwa jinsi ambavyo Mungu anataka. Watu wa namna hiyo ni vigumu sana kupokea uthibitisho wa uwepo wa Mungu, na kila kitu utakachomwambia ataona ni ujinga na upuuzi. Ukimwambia umemuona Mungu kupitia matendo Yake, ujue anakuona unaongea vitu visivyo na maana kabisaaaa.

1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Zaburi 14 :1

Science will never disprove God's existence:, He is the best scientist and all sciences are His.
Anataka umthibitishie uwepo wa MUNGU kwa jinsi anavyotaka yeye, sio kwa jinsi ambavyo Mungu anataka. Watu wa namna hiyo ni vigumu sana kupokea uthibitisho wa uwepo wa Mungu, na kila kitu utakachomwambia ataona ni ujinga na upuuzi. Ukimwambia umemuona Mungu kupitia matendo Yake, ujue anakuona unaongea vitu visivyo na maana kabisaaaa.

Mpumbavu huese
 

Swali gani hujajibiwa? Umewahi kuuona upepo? Je upepo upo ama haupo na unajuaje huu ni upepo ilihali hauna umbile wala sura? Hacha maswali ya kijinga kwa mambo ya maaana!
 
Si lazima jambo/ama kitu kionekane kwa sura ndo uwepo wake uthibitishwe. Huko ni kukosa akili.
 

Sa skia kama hujui jambo uliza, usije hitimisha na maneno yako ya kipuuzi eti hakuna Mungu! Mungu hakuwai kuumba ulimwengu wenye dhambi. Ila aliumba utashi wa kujua jema na mabaya, na katika hilo uchague mwenyewe kutenda jema ama baya. Sas dhanbi ni matokeo ya chaguzi zetu mbovu. Kudhihirisha utashi wa jema na baya, hatia uweka wazi juu ya baya husilo stahili kulitenda. Robot hutengenezwa ku-perfom a certain task, robot hana utashi. Mungu angeumba robots kusingalikuwepo dhambi.
 
Mleta mada muda ndo unazungumziwa hapo, ukitaka kujua soma kisa ni kwanini azungumzie kusimamisha jua. Joshua hakua

Yoshua hakua mwana sayansi, hawakuwa na elimu ya mfumo wa jua kama ambavyo ilivyo leo. Sisi pia tunazungumzia sun rising/set wakati tayari tunajua, jua halina movement (Nazungumzia kauli ilo zoeleka jua kuzama ama kuchomoza). Kama una uelewa utagundua Yoshua hakumaanisha jua kusimama (yaani jua simama ili iwe nini?) bali Muda! Jambo jingine ni kwamba Joshua aliamuru lkn ukweli ni kwamba MUngu ndiye alitenda na sio Joshua.
 
Sitaki kuthibitishiwa Mungu alivyokwa ninavyotaka mimi.

Natakakuthibitishiwa Mungu yupokwa logical consistency.

Mnavyomuelezea Mungu huyu mwenye uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote halafu akaumba ulimwengu huu wenye kuweza kuwa na mabaya mengi,maelezo yake yana contradiction.

Contradiction inaonesha habari ya kuwepo Mungu wenu huyo ni ya uongo.
 
Kwa nini Mungu aliumba ulimwengu unaowezekana kuchagua mema na mabaya?

Kwa nini hakuumba ulimwengu wenye utashi wa kuchagua mema na mema tu, mabaya yasijulikane wala kuwezekana?

Hujajibu swali hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…