Hakuna mjadala kwamba watu wapo.
Sijakataa kwamba ninachosema kimesemwa na watu.
What's your point?
Anayesema mungu yupo katika ulimwengu ambao hatujathibitisha kwamba mungu yupo, ana tatizo la kuthibitisha kwamba mungu yupo.
Anayesema mungu hayupo, ukimwambia maneno yake ni ya watu tu, hujamkanusha. Maana hajawahi kusema mungu yupo.
Unaposema maneno yangu ni ya watu tu, unakanusha nini?
Sijawahi kusema mungu yupo, sasa unaponiambia maneno yangu ni ya watu tu, unakanusha nini?
Tatizo unageza kanusho langu kwangu visivyo.
Mtu anayeamini mungu yupo ukimwambia maneno ya mungu yupo ni ya watu tu, na mungu hayupo, umemkanusha.
Mtu anayesema mungu hayupo, ukimwambia maneno yake ni ya watu tu, hujamkanusha. Inawezekana ukawa umeongezea nguvu hoja yake.