Ukiniambia hujui majibu ya maswali haya, unaniambia humjui huyo mungu.
Unamuamini mungu ambaye humjui.
Na kwa sababu unaamini kitu ambacho hukijui, kuna nafasi kubwa sana unaamini kitu ambacho hakipo. Mungu ambaye hayupo, katungwa tu na watu kama hadithi.
Mimi sijajua mwanadamu katoka wapi, bado nachunguza.Lakini hawezi kuwa kaumbwa na mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Maana ana mapungufu mengi sana ambayo kama kweli angekuwa kaumbwa na mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, asingekuwa nayo.
Njia moja ya kutafuta jibu ni "elimination process". Unapewa theory, unaipima, inapita au kutopita mitihani Fulani.
Mathalani, naweza kuwa sijui square root ya 2 ni nini. Lakini najua square root ta 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Mtu akiniambia kwamba square root ya 2 ni 10, nitamwambia kakosea, hilo jibu si sahihi. Hata kama sijui square root ya mbili ni nini. Najua ni lazima itakuwa ndogo kuliko mbili, si kubwa zaidi.
Wewe unachoniambia hapa, logically, ni kama uansema square root ya mbili ni 10. Mimi nakwambia si 10, ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Wewe unaniuliza square root ya mbili ni ipi.
Hata kama siijui, jibu lake haliwezi kuwa 10.
Hata kama sijui mtu katokea vipi, jibu lake si kwamba kaumbwa na mungu wako mjua yote, mwenye upendo wote na muweza yote.