Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Roho ni habari nyingine ya uzushi.

Haipo. Kama ipo thibitisha.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa roho, nitakwambia unatumia uzushi mmoja (roho) kutetea uzushi mwingine (kuwepo kwa Mungu).
Watu wa rohoni Ndio wanaomjua roho, huwezi thibitisha kwa mtu asiyekuwa na roho, Mungu ni roho na huwezi mwelezea kimwili, na bila kuamini huwezi jua habari za Mungu, cha muhimu amini kwamba Mungu yupo ndipo utakapojiliwa na huyo roho,na roho atakusaidia kumwona Mungu katika maisha yako, kumbuka vitu hivi sio vya kimwili, unapotaka uthibitisho wa kimwili siku zote utakuwa mshindi mkuu
 
Kama kitu hakipo. Unaanzia wapi kuthibitisha kwamba hakipo?

Uthibitisho wa aina gani utakufaa kuonesha kwamba kitu hakipo?

Nikikwambia pembetatu yenye pembe sita ipo, ila wewe huijui na huna akili za kuiona tu (wakati kwa kweli haipo), utanithibitishiaje kwamba haipo?

Aliyeua kwa kisu unaweza kutoa ushahidi wa alama za vidole zake ukasema huyu kaua kwa kisu, kisu kimepatikana eneo la mauaji kina damu, kina alama zake za vidole, jeraha lililoua limetokana na kisu hiki, huyu ambaye alama zake za vidole zipo kwenye kisu hana alibi.Zaidi kuna video imemrekodi akiua. Zaidi, nyumba ina alarm na ikajifunga milango, polisi wakaja wakamkuta muuaji ndani. Jirani walimuona dirishani akiua.

Overwhelming evidence. Huyu kaua.

Sasa kama hakuna aliyeua kwa kisu, utathibitishaje kwamba hakuna aliyeua kwa kisu wakati hakuna maiti, hakuna kisu, hakuna alama za vidole?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kama alivyoandikwa katika vitabu vya Biblia na Quran, hayupo.

Hayupo kwa sababu, dhana nzima ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.Contradiction.

Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, kwa sababu, kwa upande mmoja, Mungu huyu ni mtakatifu sana kiasi kwamba kibaya chochote hakiwezi kutoka kwake. Kwa maana hiyo, angekuwepo, dunia isingewezekana kuwa na mabaya. Ukisema aliumba dunia isiwe na mabaya ila Shetani ndiye akaleta mabaya, nitakuambia hata huo uwezo wa Shetani kuweza kuleta mabaya ni ubaya ambao Mungu mwenye utakatifu unaosemwa hatakiwi kuwa nao.

Kwa hiyo, utaona kwamba, kuwepo kwa mabaya, na zaidi, kuwezekana kuwepo kwa mabaya katika dunia hii, ni uthibitisho kwamba Mungu huyu hayupo.

Wengine wamejaribu kujibu kwa kusema Mungu kaachia mabaya ila katupa uwezo wa kuchagua mabaya na mazuri. Hili ni jibu lisilo na mantiki. Ukiwa na mtoto wako mchanga ambaye uelewa wake ni mdogo sana, na wewe una helewa mkubwa sana kujilinganisha naye, unampenda, utampa chupa ya maziwa na pembeni umuwekee chupa ya sumu ili tu aweze kuchagua anachotaka? Hapana. Utahakikisha nyumba nzima haina sumu anayoweza kuifikia. Utampa maziwa tu.

Sasa kama binadamu mwenye uwezo mdogo, upendo mdogo na ujuzi mdogo anakataa kumpa mtoto wake mchanga maziwa na sumu ili mtoto awe na uhuru wa kuchagua, imekuwaje Mungu huyu mnayemsema mwenye uwezo usio na mwisho, ujuzi usio na mwisho na upendo usio na mwisho ameruhusu ulimwengu uwe na mazuri na mabaya ili watu wawe na uhuru wa kuchagua tu?

Watu kama wangeumbwa katika dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya na mabaya hata hayajulikani, in fact hayapo kabisa hata kidhana, wangekosaje uhuru wa kitu ambacho hakijulikani wala kufikirika wala kuwepo kidhana tu?

Huyu Mungu yupo kweli au hadithi tu?

Kaachia dunia yenye magonjwa, vita, matetemeko, mafuriko, njaa, umasikini, kuteseka etc, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hivyo vyote haviwezekani watu wakaishibraha mustarehe.

Kwa nini?

Sijajibiwa jibu la kueleweka kwenye swali hili.
Je una amini Shetani yupo? Je unaamini kuna nguvu (super power, somewhere)? Labda tuanzie hapo.
 
Kuamini uwepo wa mungu ni utumwa wa mawazo na fikra ikiwa ni pamoja na uvivu wa kuuhangaisha ubongo. Kuna maswali mengi juu ya uwepo wa mungu kiasi kwamba vitabu vya dini havina majibu yake mpaka wanafikiria kuviandika upya. Fungukeni nyie bibadamu hakuna mdudu yeyote anayeitwa mungu
hebu niambie hilo swali ambalo halina majibu?
 
Kuliko kusema ww ni Muislim (unaamin ktk Mungu) hafu huku unamkana na kusema hayupo/una mashaka nae kua hayupo bora uache tu Kua Muislam
mkuu malizana na kiranga kwanza ...mimi mambo ya dini hayo nimewaachia wenye interest zenu ...mimi wala siwaelewi ..kuna yule zito junior aliwahi kusema kuwa kabla adamu na hawa hawajala. tunda walidanganywa na Nyoka nawakati huo Nyoka alikuwa na miguu ...aiseee nikajiuliza ilinyoka apate kuwa Nyoka nilazima asiwe na miguu..sasa Nyoka ana miguu tena halafu bado anaitwa Nyoka ...au alikuwa anamaanisha kenge ila kakosea ..haaahaaa

mimi nimechoka kulishwa matango pori mkuu
 
kiranga katoa hoja anatka uthibitishe kwanza kama Mungu yupo wewe waanza blaaahaa blaaaahh mahubiri kibao ..hivi ndivyo mlivyo fundishwa namna ya kujibu hoja....huyu Jamaa sio size yko mkuu utakimbia bure ..sio kila hoja nilazime muwe mnajibu nyingine kimo chake cha kufikiri hamkiwezi zina kina kirefu ....
Skeptics kama hao hatupotezi muda. Tunawaelekeza kwenye hoja ya msingi. Mambo ya Mungu hayajulikani kwa kuona, kutazama, kuchunguza na mengineyo bali kwa imani. Biblia ibasema wazj ni *********** tu anayesema hakuna Mungu. Yaani "common sense" itakueleza tu Mungu yupo. Philosophy of Religion inadeal na maswali ambayo Kiranga hagusii sasa nipoteze muda wa nini. Aamini tu asisumbue watu humu JF.
 
mkuu malizana na kiranga kwanza ...mimi mambo ya dini hayo nimewaachia wenye interest zenu ...mimi wala siwaelewi ..kuna yule zito junior aliwahi kusema kuwa kabla adamu na hawajala. tunda walidanganywa na Nyoka nawakati huo Nyoka alikuwa na miguu ...aiseee nikajiuliza ilinyoka apate kuwa Nyoka nilazima asiwe na miguu..sasa Nyoka ana miguu tena halafu bado anaitwa Nyoka ...au alikuwa anamaanisha kenge ila kakosea ..haaahaaa

mimi nimechoka kulishwa matango pori mkuu
Kwa hii post yako umenifanya niamini una ubongo ila huna Akili...
 
Skeptics kama hao hatupotezi muda. Tunawaelekeza kwenye hoja ya msingi. Mambo ya Mungu hayajulikani kwa kuona, kutazama, kuchunguza na mengineyo bali kwa imani. Biblia ibasema wazj ni *********** tu anayesema hakuna Mungu. Yaani "common sense" itakueleza tu Mungu yupo. Philosophy of Religion inadeal na maswali ambayo Kiranga hagusii sasa nipoteze muda wa nini. Aamini tu asisumbue watu humu JF.
Biblia inajipinga yenyewe katika mambo mengi sana na hivyo haiwezi kuchukuliwa kama kitabu cha kukikubali kama neno la Mungu.

Vivyo hivyo Quran.

Utasemaje Philosophy of Religion inagusia mambo ambayo mimi sigusii wakati naongelea the problem of evil, a central problem in Philosophy of Religion kina Aquinas, Anselm, Russell mpaka Plantinga wameishindwa kuijibu?
 
Huu si uthibitisho. Haya ni mahubiri.

Sijasema nataka mahubiri.

Nimeomba uthibitisho.
nini kilifanyaka mpaka binadamu akaitwa binadamu??
nini kilifanyika mpaka ikawa dunia??
nini chanzo chake?? ur thought plz
 
Nikisoma Vitabu Vya Dini Hasa Biblia... Mungu wa Kuanzia Kitabu Cha Mwanzo Au Vitabu Vya Kale Ni Tofauti Sana kitabia na Mungu wa Agano Jipya.

Tabia za KiMungu Alizokuwa nazo Katika agano la Kale Nikilinganisha Na Agano jipya naona Tofauti Kubwa Sana

Mfano AGANO LA KALE
Mungu Alikuwa ni Wa Hasira Sana na Anayependa Sana Waumini wake Wafuate Sheria ... Kulikuwa na Sheria Za Kitakatifu Mfano Kujiosha Mwili... mavazi.. Kuhudumia Sehemu ya Kuabudia kwa usafi wa hali ya juu... kuvukisha Ubani... kujitawaza... n.k n.k

Sasa Nitapokuja Kusoma Agano jipya Mungu anakuwa Amebadilika Sana Hasa Katika Kuabudiwa.. .. Yale Mambo ya kale aliyotaka hayapo tena.. Je Mungu amebadilika Hataki Tena Ubani... Zawadi za kuteketezwa Alizosema zinamvutia?

Je Kuna Ubaya Gani Kutoa Sadaka Za hivyo.. kuna Ubaya Gani Kurudia Kule kwa Kale.. Kujisafisha Uendapo Kuabudu..... Kuwa Msafi Au kujitawaza kama kale...
labda mimi nikuulize swali unaelewa nini kuhusu maana ya neno "AGANO"
 
HAHAAAA ..MKUU HAPO HAWEZI KUJIBU KITU ATAKUCHOSHA TU ...NIMEPENDA HUO UFAFANUZI ULIOUTOA HAP KWENYE HZO AYA ZA JUU ..JAMAA WEWE NI MTU HATARI SANA ...HIVI KWANINI MIMI SINA AKILI KAMA ZAKO ...MY FOOT
kaka changamsha nondo
 
nini kilifanyaka mpaka binadamu akaitwa binadamu??
nini kilifanyika mpaka ikawa dunia??
nini chanzo chake?? ur thought plz
Hata kama nikikwambia sijui jibu, ila ukiniambia jibu lake ni Mungu nitajua jibu si sahihi.

Kama ambavyo unaweza kuniuliza "nini square root ya 2?" nikakwambia sijui.

Lakini nikajua jibu lake si 10.

Kwa sababu square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa kuliko 2. Hiyo itakuwa contradiction.

Hivyo hivyo, jibu la Mungu kwa maswali yako si sahihi. Kwa sababu lina contradiction.

The problem of evil contradicts the existence of God.

Sijui kama umeelewa.

Ukisema Mungu ndiye chanzo cha maisha haya ni sawa sawa na anayesema square root ya 2 ni 10.
 
Mungu atajithibitisha mwenyewe kwa Kiranga naye atakuja humuhumu akipata neema hiyo kuja kukiri. Mtu hawezi kumtetea Mungu. Mungu hujitetea mwenyewe na hujithibitisha mwenyewe. Watumishi wa Mungu kazi yao ni kuhubiri tu Injili. Wapo watakaoamini na huenda wakawepo wasioamini kama Kiranga. Sasa huwezi kumlazimisha. Mwacheni na muombeeni kwa Mungu ampe kuamini.
Mungu hawezi kujithibitisha kwangu.

Kwa sababu hayupo.

Na hii ndiyobsababu hata wewe huwezi kuthibitisha yupo.

Unajificha kwenye chaka la "Mungu atajithibitisha".
 
Deadbody, Biblia inasema kuwa "mpumbavu amesema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu.".

Sasa unataka huyo mtu athibitishiwe vipi kuwa kuna Mungu wakati Biblia inamwita mtu wa namna hiyo kuwa ni mpumbavu? Unathubutu vipi kubishana na 'mpumbavu '?

Vv
 
Back
Top Bottom