Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Sasa kama habadiliki iweje nisome Agano Jipya Wakati la Kale Linatosha
Kama unaona linatosha usisome ila swali ni Linatosha kivipi??,linakutosheleza nini ,linakutosheleza kwa wakati gani,kitabu gani kinatosha na kinatosheleza nini........................................fafanua zaidi maswali yanayotokana na jibu lako ni mengi mno! Na kama linatosha unauliza ili iweje??
 
Nibaki namfano wangu wa kusafiri kwenda Mwanza kwakupitia Dodoma.

Unachouliza hapo ni kama vile umuulize mtu, wewe unataka kwenda Mwanza, unaanzaje kujadili kwamba ukiwa Dodomauelekee muelekeo gani?

Usipokadili uelekee muelekeo gani kutokaDodoma ili ufike Mwanza, unaweza kujikuta unazunguka Dodoma hapohapo Mwanza hufiki, au unarudiulikotoka Dar.

Kama natafuta fact, na kuna imani nyingi tofauti, nazichuja imani kutafuta ipiya ukweli.

Ntest ya kwanza ni logical consistency.

Kama naenda Mwanza kutoka Dodoma kwa barabara nyoofu (for simplicity's sake), Mwanza ni magharibi ya Dodoma, kurudi mashariki ni kurudi DAR.

Sasa kwa nini unaniambia niende Mwanza kutoka Dodoma bila kuangalia naelekea muelekeo upi?

Kwa nini unataka nitafute fact kutoka imani bila kuhoji imani tofauti?

Ni nani anayekwambia utafute fact kutoka kwenye imani?

Wewe mwenyewe ulisema haupo hapa kujadili imani bali fact na ndiyo maana unadai uthibitisho kwa mtu mwenye kusema mungu yupo kama fact na si imani,maana imani mtu anaweza kuamini vyovyote anavyotaka huna tatizo na unatetea haki yake hiyo.

Tatizo lako unaandika tu unachojisikia bila kuzingatia unachokisimamia.
 
Ni nani anayekwambia utafute fact kutoka kwenye imani?

Kwa nini swali liwe nani? Nikikuuliza "bendera ya taifa ya Tanzania ni ya aina gani ya rangi nyekundu?", utanijibu vipi?

Wewe mwenyewe ulisema haupo hapa kujadili imani bali fact na ndiyo maana unadai uthibitisho kwa mtu mwenye kusema mungu yupo kama fact na si imani,maana imani mtu anaweza kuamini vyovyote anavyotaka huna tatizo na unatetea haki yake hiyo.

Nikisema sitaki kukaa Dodoma, nataka kukaa Mwanza, nikiwa Dodoma njiani kwenye gari naelekea Mwanza utaniuliza vipi "mbona umekaa Dodoma?" wakati sijakaa Dodoma, nipo kwenye gari napita kuelekea Mwanza?

Nimekuuliza hili swali, umeliruka hujalijibu kama hujaliona.

Tatizo lako unaandika tu unachojisikia bila kuzingatia unachokisimamia.

Tatizo lako ama hujui kusoma, ama unataka kupinda maneno, inawezekana kabisa yote mawili yanahusika.
 
Je Mungu anabadilika
Kwangu mimi, swali la Mungu kubadilika hata halipo mpaka nithibitishiwe kwamba yupo kwanza.

Kwa sababu kama hakuna anayeweza kuthibitisha Mungu yupo at all, tutajadili vipi habari za kubadilika?

Kama hayupo, atabadilikaje?

Kuna mtu anaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Kwa nini swali liwe nani? Nikikuuliza "bendera ya taifa ya Tanzania ni ya aina gani ya rangi nyekundu?", utanijibu vipi?

Nikisema sitaki kukaa Dodoma, nataka kukaa Mwanza, nikiwa Dodoma njiani kwenye gari naelekea Mwanza utaniuliza vipi "mbona umekaa Dodoma?" wakati sijakaa Dodoma, nipo kwenye gari napita kuelekea Mwanza?

Nimekuuliza hili swali, umeliruka hujalijibu kama hujaliona.

Tatizo lako ama hujui kusoma, ama unataka kupinda maneno, inawezekana kabisa yote mawili yanahusika.

Tatizo lako unafikiri mie niko hapa kushindana na kwa ubishi,mie siwezi kushindana ubishi na mtu ambaye hata hajui anchokisimamia alichokiandika jana na leo ni tofauti. Muda wote hapa nina kazi ya kukuonesha jinsi unavyojichanganya kwa sababu yakutojua unachosimamia.

Halafu suala la sijui dodoma na mwanza tulishajadili na comment yangu ndiyo ya mwisho katika huo mjadala ila nashangaa kuambiwa skujibu swali.

Kwanza umetunga swali mwenyewe kwa mtazamo wako na kuchukulia kama mie ndiye niliyeuliza swali hilo kisha hapohapo unanitandika swali lenye kutokana na swali la kufikirika kisha unalazimisha nijibu!!!

Kukaa kuna maana mbili,inaweza kuwa kuka kitako au kuishi .Sasa sijui hapo dodoma ulikaa kitako au uliweka makazi sijui hata nashindwa kuelewa.
 
Tatizo lako unafikiri mie niko hapa kushindana na kwa ubishi,mie siwezi kushindana ubishi

Ubishi ninini? Mbona watu wengine wanaweza kusemaukinijibu tu umeshaingia katikaubishi na wasiotakaubishi hata kujibu hawajibu?

Kwa niniubishi uwe kitu kibaya kama umejikita katikakutafuta ukweli?

Umeshasoma habari zozote za mahojiano ya Socrates ukaona jinsi ubishi unavyotumiwa kufungua macho?

Umeshasoma kitabu cha Galileo Galilei "The Dialogue Concerning The Two Chief World Systems" ukaona ubishiulivyopangiliwa na kuelimisha watu kwamba jua halizunguki dunia kamawalivyofikiri, na inaonekana zaidi kwamba duniandiyoinazunguka jua?

Dialogue Concerning the Two Chief World Systems - Wikipedia

na mtu ambaye hata hajui anchokisimamia

Mtu yupo kwenye gari hayupo Dodoma, anakwenda Mwanza, kwa niniunasema hajui aliposimamia kwa sababu yupo kwenye gari Dodoma anakwenda Mwanza na amaesema hataki kukaa Dodoma? Kwa niniunaona hajui aliposimamia wakati kasemahatakikukaa Dodoma anapita njia tu kuelekea Mwanza? Hujanijibu swali hili

alichokiandika jana na leo ni tofauti. Muda wote hapa nina kazi ya kukuonesha jinsi unavyojichanganya kwa sababu yakutojua unachosimamia.

Nilichoandikatofauti ni kipi?

Kusema sitaki kujikita kujadili imani, nataka kujua ukweli, ambao unapatikana kwa kujadili imanikwa niaya kujua ukweli, hapo kujichanganya kuko wapi?

Kusema kwamba sitakikukaa Dodoma, nataka kupita njia tu kwenda Mwanza,ukinikuta njianikwenye gari napita Dodoma utasemaje najichanganya, nimekaa Dodoma, wakati nilisemasikai Dodoma, wakati Dodoma sijakaa, napita kwenye gari?

Unaelewa wewe ndiye unayetaka kulazimishakujichanganya ambako hakupo?

Unaelewa wewe unayemuamini Mungu mwenye contradiction ndiye unayejichanganya?

Mungu wako, upande mmoja ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, upande mwingine, kaumba ulimwengu wenye maovu mengi yasiyomithilika.

How do you reconcile this? Hujaondoa contradiction hii, umejichanganya. Halafu unaona mimi najichanganya pale ambapo hakuna kujichanganya.

Halafu suala la sijui dodoma na mwanza tulishajadili na comment yangu ndiyo ya mwisho katika huo mjadala ila nashangaa kuambiwa skujibu swali.

Tumejadili wapi? Post iko wapi? Swali ambalo hujajibiwa ni lipi?

Wewe hujajibu swali langu, je, mtu anayetaka kwenda Mwanza kwakupitia Dodoma, akisema hataki kukaa Dodoma, ukimkuta kwenye gari njiani Dodoma, anaelekea Mwanza, utasema kakaa Dodoma kinyume na matamshi yake ya awali?

Kwanza umetunga swali mwenyewe kwa mtazamo wako na kuchukulia kama mie ndiye niliyeuliza swali hilo kisha hapohapo unanitandika swali lenye kutokana na swali la kufikirika kisha unalazimisha nijibu!!!

You either can't see the analogy, or you are pretending to not see it.

Mwanza ni ujuzi, Dodoma ni imani.

Mimi sitaki kujikita katika imani, nataka kupita tu imani, nielekee ujuzi.

Nataka kupita Dodoma, nielekee Mwanza.

Ukinikuta Dodoma nafuata direction ya Mwanza kwenye GPS huku naendesha gari,utasema nimekaa Dodoma kinyumena matamshi yangu ya awali?
Kukaa kuna maana mbili,inaweza kuwa kuka kitako au kuishi .Sasa sijui hapo dodoma ulikaa kitako au uliweka makazi sijui hata nashindwa kuelewa.

Una hakika hata ukieleweshwa uwezo wa kuelewa unao?

Kushindwa kwakokuelewa pia ni ushahidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, hakuna mtu ambaye angeshindwa kumuelewa yeye huyo Mungu wala mtum wingine yeyote.
 
Haijalishi kuchomoza jua lini, kitendo cha kusema unaamini jua litachomoza iwe kesho au kesho kutwa hiyo ni imani. Na wewe mwenyewe ulisema kuwa hiyo imani ina ushahidi tofauti na imani ya uwepo wa mungu.

Na dodoma ni sawa na imani, na ndiyo nilipohusisha imani ya kuchomoza jua na dodoma.

Kama bado haujaridhika endelea kuuliza.
Kiranga

Hii ndiyo comment ya mwisho kujadili mfano wa wako wa dodoma na mwanz, kwa mara ya kwanza.

Post#1367
 
Kiranga

Hii ndiyo comment ya mwisho kujadili mfano wa wako wa dodoma na mwanz, kwa mara ya kwanza.

Post#1367
Comment ya mwisho kujadili kwa mara ya kwanza?

Wakati naendelea kujadili mpaka sasa!

Does that make sense to you?
 
Mkuu, nadhani wote tunaamini kua BIBLIA Takatifu imeandikwa na watu wa Mungu walioongozwa na ROHO wa Mungu.
Agano la kale lina vitabu ambayo vingi ni torati za Musa na habari za Waamuzi, Wafalme na Manabii...
Agano jipya lina vitabu vya Injili vilivyoandikwa na Wainjilisti (wanafunzi wa Yesu) pamona na Mitume (Mf Paulo).

Ujio wa Agano jipya ni utimilifu wa yaliyoandikwa katika vitabu vya Agano la kale....
Ndio maana mwenyewe Yesu alisema "Siajaja kuibadilisha torati bali kuitimiza" (Sikumbuki kutabu gani nikipata ntaweka)

Agano la kale Mungu alikua anaongea na Manabii ndio Nabii alete ujumbe and vice versa....
Agano jipya baada ya Yesu kusulubiwa na pazia la Hekaluni kupasuka, hii inamaanisha mlango wa kufikisha maombi yako na ibada zako moja kwa moja bila kupitia kwa Manabii kama ilivyokuwa awali.....

Yapo mengi sana ambayo kuandika sitoweza maana mimi sio muandishi mzuri...
Umesema ujio wa Agano jipya ni utimilifu wa Agano la kale je lilikuwa na kasoro na kama lilikiwa na kasoro kwa nini kutumika wakati likiwa na kasoro huoni kabla ya kurekebishwa limewapoteza wengi?
 
Umesema ujio wa Agano jipya ni utimilifu wa Agano la kale je lilikuwa na kasoro na kama lilikiwa na kasoro kwa nini kutumika wakati likiwa na kasoro huoni kabla ya kurekebishwa limewapoteza wengi?
Hebu niiweke hii sawa

Anaposema ujio wa agano jipya ni utimilifu wa agano la kale haimaanishi agano la kale linakasoro hapana
Labda nikupe mfano uelewe

Tuseme watu watatu wanakunywa maji Lita 3 (Kila mmoja Lita Moja) kwa siku wakiwa kivulini hii inamaana wakiongezeka watu Wawili na watu hawa wakihamia juani hawatatosheka tena na zile Lita 3 kwasababu kwanza wamebadili mazingira na wameongezeka idadi.

Vivyo hivyo agano lakale liliwafaa na kuwatosheleza Kama zile chupa 3 za maji kwa walio kivulini Haina maana kuwa agano la kale halifai tena linafaa maana wale watu 3 na walioongezeka na kwenda juani hawatakataa kunywa zile Lita 3 wanakunywa ingawa hawata tosheka kutokana na mabadiliko inabidi wapate ndoo ya Lita 10 ili watosheke

Agano la kale = maji Lita 3
Agano jipya = maji Lita 10
 
Watu wanakufuru humu doh.. Bora uamini Mungu yupo hata siku ukifa ukakuta hayupo inakua sio mbaya..

Kimbembe unaamini hayupo halafu siku unakufa unakutana nae uso kwa uso huyu hapa[emoji16][emoji16][emoji16]
Hapo Ndo utakapocheza sindimba na roho yako[emoji23]
 
Comment ya mwisho kujadili kwa mara ya kwanza?

Wakati naendelea kujadili mpaka sasa!

Does that make sense to you?
"Tumejadili wapi? Post iko wapi? Swali ambalo hujajibiwa ni lipi?"

Uliniuliza hivyo.

Unaona tatizo lako nililokwambia? Sasa kama hata hukuwa ukikumbuka kama tuliwahi kujadili mfano wako wa mwanza na dodoma unadhani hata utajua tuliishia vp katika huo mjadala?

Na ndiyo maana kila siku umekuwa mtu wa kuuliza maswali yaleyale na kudai haujajibiwa wakati mtu mwenyewe huna hata kumbukumbu.
 
let us say tunaishi kwenye era ambayo hatujui kuhusu hewa,likatokea kundi flani likaamini katika hewa,likasema hewa IPO kwasababu inatusaidia kupumua,mazao yanakua kwasababu ya hewa hivo ni muhimu sana kwa maisha yetu na wakaandika na kitabu kinachoelezea sifa nzuri za hewa.Baadae akaja mtu akakakataa akasema hewa HAIPO kwasababu kwenye kitabu wameandika hewa ni muhimu kwa maisha yetu ili hali ni hewa inayosababisha vimbunga,miti kuanguka na maafa makubwa na isitoshe hewa yenyewe haionekani.hiyo inaweza kuondoa ukweli kwamba hewa ipo?unaposema Mungu hayupo kwasababu tuu ya sifa zake zilizotajwa kwenye maandiko haukubaliani nazo,vipi ukikutana na mtu anayeamini Mungu yupo sio kwasababu ya maandiko ila kwasababu sayansi imeshindwa kutoa majibu kamili kuhusu source of life and the universe utamshawishi vipi mtu kama huyo kwamba Mungu hayupo?kuna thread humu inazungumzia mikanganyiko inayochanganya iliyopo kwenye biblia,sina tatizo na thread hizo na nafikiri kwa ukomo wa uelewa wetu tunaweza tukajadili,lakini kujadili Mungu yupo au hayupo thats beyond our knowledge.and a wise man yupo tayari kusema sijui kuliko ku jump on conclusion kwamb hayupo.
 
Kwa nini unafikiri mtu akikuuliza "tumejadili wapi?" basi ni lazima hakumbuki kama mliwahi kujadili?

Yesu alivyoshika sarafu na kuwauliza Wayahudi "Sarafu hii ina picha ya nani?" alikuwa anajua sarafu ile ina picha ya nani au haina?

Tatizo una assume sana.

Mtu akitaka kujenga hoja kwa kutumia "Socrates Method" unaona kila swali analokuuliza ni kwa sababu hajui jibu.

This is a logical non sequitur.

Unaonesha ufinyu wa mawazo yako uki assume kwamba kila swali mtu analokuuliza ni kwa sababu hajui jibu.
 
Umesema ujio wa Agano jipya ni utimilifu wa Agano la kale je lilikuwa na kasoro na kama lilikiwa na kasoro kwa nini kutumika wakati likiwa na kasoro huoni kabla ya kurekebishwa limewapoteza wengi?
Mkuu soma uelewe au uombe ufafanuzi... UTIMILIFI = KUTIMIZA au UTIMIZO
 
let us say tunaishi kwenye era ambayo hatujui kuhusu hewa,likatokea kundi flani likaamini katika hewa,likasema hewa IPO kwasababu inatusaidia kupumua,mazao yanakua kwasababu ya hewa hivo ni muhimu sana kwa maisha yetu na wakaandika na kitabu kinachoelezea sifa nzuri za hewa.Baadae akaja mtu akakakataa akasema hewa HAIPO kwasababu kwenye kitabu wameandika hewa ni muhimu kwa maisha yetu ili hali ni hewa inayosababisha vimbunga,miti kuanguka na maafa makubwa na isitoshe hewa yenyewe haionekani.hiyo inaweza kuondoa ukweli kwamba hewa ipo?unaposema Mungu hayupo kwasababu tuu ya sifa zake zilizotajwa kwenye maandiko haukubaliani nazo,vipi ukikutana na mtu anayeamini Mungu yupo sio kwasababu ya maandiko ila kwasababu sayansi imeshindwa kutoa majibu kamili kuhusu source of life and the universe utamshawishi vipi mtu kama huyo kwamba Mungu hayupo?kuna thread humu inazungumzia mikanganyiko inayochanganya iliyopo kwenye biblia,sina tatizo na thread hizo na nafikiri kwa ukomo wa uelewa wetu tunaweza tukajadili,lakini kujadili Mungu yupo au hayupo thats beyond our knowledge.and a wise man yupo tayari kusema sijui kuliko ku jump on conclusion kwamb hayupo.
Jibu zuri..
Ningependa wanaopinga uwepo wa mungu wapite hapa kidogo
 
Mkuuu umeelewekaaa....
 
Jibu zuri..
Ningependa wanaopinga uwepo wa mungu wapite hapa kidogo
mkuu watu kama hao unakuta hoja zao ni zile zile hawana jipya,kama unaweza kuprove kitu fulani KIPO inamaanisha unaweza pia kuprove kitu hicho HAKIPO(kama hakipo).atakulazimisha wewe u prove,ukimwambie yeye a prove atakimbilia kujificha kwenye maandiko,hiyo hai prove kwamba Mungu hayupo,na haitakuja kuprove kamwe.ni bora kusema sijui kuliko kujivimbisha humu kila siku.
 
Nikisoma Vitabu Vya Dini Hasa Biblia... Mungu wa Kuanzia Kitabu Cha Mwanzo Au Vitabu Vya Kale Ni Tofauti Sana kitabia na Mungu wa Agano Jipya.

Tabia za KiMungu Alizokuwa nazo Katika agano la Kale Nikilinganisha Na Agano jipya naona Tofauti Kubwa Sana

Mfano AGANO LA KALE
Mungu Alikuwa ni Wa Hasira Sana na Anayependa Sana Waumini wake Wafuate Sheria ... Kulikuwa na Sheria Za Kitakatifu Mfano Kujiosha Mwili... mavazi.. Kuhudumia Sehemu ya Kuabudia kwa usafi wa hali ya juu... kuvukisha Ubani... kujitawaza... n.k n.k

Sasa Nitapokuja Kusoma Agano jipya Mungu anakuwa Amebadilika Sana Hasa Katika Kuabudiwa.. .. Yale Mambo ya kale aliyotaka hayapo tena.. Je Mungu amebadilika Hataki Tena Ubani... Zawadi za kuteketezwa Alizosema zinamvutia?

Je Kuna Ubaya Gani Kutoa Sadaka Za hivyo.. kuna Ubaya Gani Kurudia Kule kwa Kale.. Kujisafisha Uendapo Kuabudu..... Kuwa Msafi Au kujitawaza kama kale...
MUNGU hajabadilika, ni Yule Yule, jana, leo, na kesho. Kilichobadilika ni Sheria za MUNGU na siyo AMRI za MUNGU. Kuna tofauti kubwa kati ya Sheria na Amri.

Wakati ule wa Agano la Kale, MUNGU alikuwa analiandaa taifa la Israeli ili kupitia taifa hili, Mwokozi wa ulimwengu mzima azaliwe. Ifahamike kwamba wakati ule wanadamu walikuwa kwenye ujinga wa hali ya juu sana wa kutomtambua wala kumkubali MUNGU. Hivyo basi hata yeye ilibidi awe mkali zaidi ili watu waweze kufahamu uwepo wake na ndiyo maana akaweka Sheria kali ili kila anayevunja sheria hizo, kama ni kufa na afe ili wengine wajifunze. Na ndiyo maana utaona hata wakati anawatoa wana wa Israeli pale Misri, alitumia nguvu kubwa na maajabu makubwa ili wanadamu wafahamu kuwa yupo MUNGU WA KWELI. Hata baadhi ya Waisraeli walipokosea wakati wakiwa jangwani, wakati mwingine alikuwa anawazamisha chini ya ardhi na kuwafukia wakiwa hai ili wale wanaobakia watambue kuwa yupo na wasirudie makosa kama yale. Tena akaweka Sheria kali na kuwakabidhi Makuhani Walawi wazisimamie na kuwaadhibu wale wote watakaozivunja Sheria hizi kwa namna Sheria inavyotaka.

Sasa basi utaona baada ya kuzaliwa kwa YESU KRISTO, sheria zilibadilishwa na MUNGU mwenyewe kupitia YESU KRISTO sababu mpaka wakati wa Agano Jipya tayari MUNGU wa KWELI alikuwa anajulikana isipokuwa tu baadhi ya watu walikuwa hawamtii, lakini kujua kama MUNGU yupo, walikuwa wanajua sana. Lengo la MUNGU lilikuwa ni kumleta Mwanawe duniani ili aje aikomboe dunia kutoka kwenye dhambi na hilo lilipofanikiwa, basi MUNGU akawaacha wanadamu wote na Waisraeli wachague wenyewe njia ya Wokovu au njia ya Upotevu. Akawaacha pasipo kuwaadhibu kwa kutumia Sheria kama ilivyokuwa enzi za Agano la Kale ambapo walikuwa wanaadhibiwa kwa kutumia Sheria.

Ndiyo maana ukisoma kwenye Biblia utaona kuna mahali YESU anasema; "sijaja kuitangua torati wala manabii, bali kuitimiliza". Na tena kuna mahali YESU anasema "maneno yangu siyo yangu bali ni yake Yeye aliyenituma". Hivyo basi tunaona kwamba MUNGU alimtuma YESU aje awafundishe wanadamu wasihukumiane tena, bali wawe wenye upendo na wenye kusameheana wao kwa wao na kuvumiliana mpaka siku ile atakapoleta hukumu kwa watu wote. Na ndiyo maana YESU aliwaambia Mafarisayo maneno haya; "enendeni mkajifunze maana ya maneno haya; nataka Rehema na siyo Sadaka". Hapa alikuwa anamaanisha kuwa anataka Mafarisayo na watu wote wawe na "huruma" zaidi kuliko kutoa Sadaka.

Ukitizama kijuu juu kwa macho ya kibinadamu, unaweza ukasema MUNGU amebadilika, lakini siyo kweli, MUNGU ni yule yule, isipokuwa tu amebadili Sheria na kuzifanya kuwa Neema yenye Upendo ili huruma yake kwa wanadamu aliyokuwa nayo tokea mwanzo ijidhihirishe kwa watu wa mataifa yote. Na ndiyo maana hata Mitume walisema kuwa "tunaokolewa kwa Neema tu", yaani, ni kama Zawadi tu, hatukustahili kuokolewa. Mfano mzuri ni enzi zile mtu akizini, alikuwa akikamatwa anazini, ilikuwa ni lazima auawe kwa kupigwa na mawe. Na hivi ndivyo sheria ilikuwa inataka iwe. Lakini utaona kwenye Agano Jipya, yule mwanamke mzinzi anapokamatwa na kuletwa mbele ya BWANA YESU, mwanamke yule anasamehewa na kuachiwa huru. Hii ndiyo "neema", yaani kwa neema tu anasamehewa ingawa Sheria inamuhukumu. Maana yake ni kwamba wale wasioipokea neema hii kwa kuacha dhambi zao, basi siku ya mwisho watahukumiwa kwa kutupwa kwenye moto kama Sheria inavyosema kuwa kila mzinzi, kama ni kufa na afe. Hivyo basi utaona "neema na rehema" zimepewa nafasi kipindi hichi ili watu wengi waokolewe, lakini wale watakaokataa kuzipokea rehema na neema hizi, hukumu ya moto inakuja juu yao.

MUNGU ni yule yule, MUNGU ni mkali sana, isipokuwa ni mvumilivu sana, tena anavumilia tu ili tuweze kujirudi na kuacha maovu yetu sababu hapendi hata mmoja wetu apotee. Hata yeye alisema kwa kinywa cha Nabii Isaya kuwa; "nimenyamaza kimya kwa muda mrefu, lakini sasa nitapiga kelele na kupaza sauti kama mwanamke aliye kwenye utungu wa kuzaa". Na kweli kabisa, sasa hivi MUNGU amenyamaza kimya, siyo kama zamani zile za Agano la Kale, lakini siku inakuja ambapo atapaza sauti yake, na hapo ndipo wanadamu na viumbe vyote watakapotambua hasira za MUNGU. Biblia inasema kuwa siku hiyo milima itakimbia na visiwa vitatoweka na mbingu zitafunguka kama vile mtu afunuavyo ukurasa wa kitabu. Siku ya ghadhabu na hasira ya BWANA MUNGU hakika inakuja.

Ndugu yangu RGforever MUNGU ni yule yule, jana, leo na kesho.
 
Back
Top Bottom