Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Huo ndio uongo mkuu zaidi wa Ukatoliki, na ndio unabeba madanganyo yake mengine yote.Mkuu tambua hiyo biblia unayoiamini walio itunza na kuilinda ni wakatoliki ukiristo bila ukatoliki ungekua umepotea siku nyingi.
Kwangu mimi ukatoliki ndio mlizi wa ukristo duniani.
Kwa taarifa yako Ukatoliki ndio umeuchafua Ukristu kuliko kingine chochote duniani!!!
👉Ukatoliki ndio umesababisha hadi leo Ukristu hauwezi kupenya kirahisi Mashariki ya Kati na maeneo mbalimbali mengine.
👉Vile vita vijulikanavyo kama Vita vya Msalaba alivyovianzisha Papa Urban II kunako karne ya 11, vikaendelea hadi karne ya 14, ni donda baya mno lilosababishwa na haohao mapapa wanaojigamba eti ni warithi wa Mtume Petro na wawakilishi wa Kristu duniani.
👉Ukatoliki ulizuia kabisa Biblia zisitafsiriwe wala kusomwa wala kumilikiwa na waumini wa kawaida. Waliokutwa na Biblia waliuawa; waliohubiri misingi ya Biblia waliteswa na kuchomwa moto.
👉Wasiokubali imani ya Ukatoliki waliuawa kikatili mno, wengi walifungwa na kuchomwa moto.
👉Wakati fulani kwa jamii ya Wakristu huko Ufaransa, Papa Innocent III alitoa amri akisema ^waueni wote, Mungu atajichagulia walio Wake huko huko!^
👉Je, hiyo kweli ni kauli na matendo ya Kanisa la Mungu ambalo Yesu alikuja kuwafia watu ili waokolewe?
👉Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. ~Luka 9:56
👉Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. ~Mathayo 7:15
👉Bila kusahau mauaji ya kinyama ya Wakristu 70,000 kwa siku moja Jijini Paris/St Bartholomew's Day Masaccre Agosti 24 1572.
👉Maelfu kwa maelfu waliuawa kwa amri ya yule anayejiita eti ndiye mwakilishi wa Mungu duniani! Fedheha na kufuru ilioje!
👉Wayahudi waliteketezwa kwa maelfu. Nchini Hispania Wayahudi zaidi ya 10,000 walifungwa na kuchomwa moto! Nchini Ufaransa, Hispania na Uingereza Wayahudi wakatimuliwa.
👉Upagani ulioenea makanisani leo ni matokeo ya Ukatoliki kuunajisi Ukristu.
👉Ibada za sanamu ziliingia kwenye makanisa ya Ukristu kupitia mlango wa Ukatoliki.
👉Ukatoliki ulihusika kupindua serikali na tawala za nchi na falme mbalimbali ambazo hazikukubali kuufuata Ukatoliki. Na ndivyo hufanya hadi leo.
👉Ukatoliki umejipatia pesa na utajiri kwa kuuza vitubio na misamaha ya dhambi kwa waumini na hata raia katika nchi.
👉Kuna Daraja la Ombaomba waliokuwa wameidhinishwa na papa, wakajaa Ulaya yote wakiwalaghai watu na kukomba mali zao ili tu kutunisha hazina ya papa.
👉Leo hii Ukatoliki ni tajiri zaidi duniani kwa sababu ya matokeo ya kazi zake chafu kupitia mgongo wa Ukristu, ukisaidiwa na serikali na falme zilizo chini yake, pamoja na Madaraja ya Ukatoliki kama Majesuti, Franciscans, Dominicans, Augustinians, nk
👉 Haya ni mashirika ambayo yameenea karibu kila nchi duniani, lengo lao ni moja kuuneza Ukatoliki kwa namna yoyote ile na kumfanya kila mtu na kila nchi iwe chini ya upapa. Mali, pesa, ardhi kwa sehemu kubwa vinapokwa na kuwekwa chini ya Vatikani. Anayejaribu kupingana nao anakabiliwa na mkono wa chuma na hatimaye umauti.
👉Ukatoliki ndio chanzo cha umaskini wa mataifa mengi duniani; Vatikani imepoka mali na pesa nyingi za nchi na falme mbalimbali, kwa njia ya hila, ulaghai, na kutumia vitisho na nguvu.
👉Ukatoliki ulihusika 100% kughushi nyaraka na maandishi mbalimbali na kujaribu kuviongeza kama sehemu ya vitabu vya Biblia ili tu kuunga mkono mafundisho yake yaendayo kinyume na Biblia.
👉Kuanzishwa kwa dini ya Kiislamu katika karne ya 7 BK ni matokeo ya moja kwa moja ya mbinu chafu za Ukatoliki. Ndiyo maana Ukatoliki na Uislamu vinafanana sana vikitazamwa kwa jicho la 3.
👉Ukatoliki unaeneza dini yake kimabavu. Uislamu vilevile. Ukiasi Ukatoliki wewe ni adui na mdudu unayestahili kuuawa. Vilevile kwa Uislamu. Ushirikina na mambo ya giza ni sehemu ya ibada za Ukatoliki na Uislamu. Ukatoliki na Uislamu wote huabudu sanamu na wafu, huku wakifanya ionekane kwa vile wanatetea dini ya kweli.
👉Muumini wa Ukatoliki anahesabika kama mali halali ya dini hiyo. Anamilikiwa, wala hatakiwi kuwa na maamuzi yake mwenyewe na hapaswi kuwa na utashi na uhuru kifikra. Vilevile kwa Uislamu. Uislamu na Ukatoliki ni binti na mamaye; akiwa amejifunza maovu na ukatili kutoka kwake.
👉Hila na udanganyifu ndizo silaha zao; kwa nje huonekana wamejivika mavazi ya upole na wema na huduma kwa jamii, lakini ndani yao ni mbwa-mwitu wakali. Mathayo 7:15
👉Ukatoliki una hatia ya kurudisha nyuma maendeleo ya sayansi, taaluma, dini na mfumo wa jamii ya mwanadamu. Wanahesabu, wanafalsafa, wananga, wanafizikia na wasomi mahiri kama akina Galileo walifungwa gerezani na kuuawa, kisa tu walifundisha na kueneza mawazo ambayo Ukatoliki haukuyaridhia.
👉Huo ndio Ukatoliki unaoendelea kuwaghilibu watu kwamba Yesu aliwapa ufunguo wa mamlaka duniani, na kwamba Petro ndiye alikuwa papa wa kwanza.
👉[4] Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
[5] Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. ~Ufunuo wa Yohana 18:4-5