Naomba nikujibu. I declare mimi siyo mlokole ila najua details nyingi sana za hayo mambo. In fact walokole ibada yao haijajikita kwenye kusoma biblia na kumwelewa Mungu. Badala yake Ibada zao zimejikita katika kuamsha hisia (to arouse emotions). Yaani mtu anakujaza upepo kitu ambacho ukitumia akili vizuri kufikiria huwezi kukubaliana nacho, ila unatengenezewa muamsho wa kihisia ambazo ili ukubaliane nazo lazima uwezo wako wa kuchambua mambo uushushe kwanza alafu upandishe uwezo wa emotions zaidi. Imagine kwenye maombi mtu unaambiwa pokea gari, pokea nyumba, pokea ajira n.k. na wewe unajua kabisa hujafanya chochote ili hilo gari ulipate. Akili yenye kufikiria inakuambia je utaliokota? Unatakiwa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya fedha. Lakini kwa sababu ya emotions unaaminishwa kwamba unapokea kimiujiza. Na hapo hapo unaaminishwa utoe sadaka ili upokee huo muujiza. Huyo anayekujaza upepo huo anataka sadaka yako ili akanunue gari ila wewe anakuambia utapokea muujiza.Wakisali ni makelele makubwa sana, mpaka unashangaa, hivi haiwezekani wakiomba waombe kwa Sauti za kawaida tu na sio kupayukapayuka?
Wakianza kuabudu sasa, muziki utawekwa full blast, buzuki kubwa sana halafu ndani ya kanisa unakuta wako watu wanne tu wa familia Moja, hapo watapiga makelele kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa SITA usiku.
Kwa ibada ndefu za makelele zinasababisha maswali mengi sana, huenda Mungu wao Yuko mbali sana. Huenda haelewi Kiswahili hivyo inabidi wampigie makelele mazito ili aweze kubahatisha baadhi ya maneno.
Labda Yuko busy sana hivyo wanamahtua ili awakumbuke...
Maswali ni mengi majibu ni haba.