Je, Mungu wa walokole hasikii hadi apigiwe makelele Makubwa?

Je, Mungu wa walokole hasikii hadi apigiwe makelele Makubwa?

LUKA 19:40 - "Nawaambia kwamba hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele"

By choosing understanding over judgment, listening over condemnation, and respect over fear, we foster harmony among all faiths

NB: EMBRACE TOLERANCE
Asante but this is out of context and you know it 😅
 
Naomba nikujibu. I declare mimi siyo mlokole ila najua details nyingi sana za hayo mambo. In fact walokole ibada yao haijajikita kwenye kusoma biblia na kumwelewa Mungu. Badala yake Ibada zao zimejikita katika kuamsha hisia (to arouse emotions). Yaani mtu anakujaza upepo kitu ambacho ukitumia akili vizuri kufikiria huwezi kukubaliana nacho, ila unatengenezewa muamsho wa kihisia ambazo ili ukubaliane nazo lazima uwezo wako wa kuchambua mambo uushushe kwanza alafu upandishe uwezo wa emotions zaidi. Imagine kwenye maombi mtu unaambiwa pokea gari, pokea nyumba, pokea ajira n.k. na wewe unajua kabisa hujafanya chochote ili hilo gari ulipate. Akili yenye kufikiria inakuambia je utaliokota? Unatakiwa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya fedha. Lakini kwa sababu ya emotions unaaminishwa kwamba unapokea kimiujiza. Na hapo hapo unaaminishwa utoe sadaka ili upokee huo muujiza. Huyo anayekujaza upepo huo anataka sadaka yako ili akanunue gari ila wewe anakuambia utapokea muujiza.
Asante umeelezea vizuri kabisa. Nilikuwa mlokole hivyo haya unayoyaelezea nayaelewa kabisa lakini katika ulokole wangu hiki kipengele cha kusali kwa kelele kilikuwa sikipendi kabisa, kabisa. Why shout?
 
Issue yako ilikuwa ni Makelele huko kupayukapayuka umetoa wapi? Au kwako wewe kupiga kelele ndiyo kupayuka?. Pia umesema Ibada zinaanza saa mbili asubuhi Mpaka saa sita Usiku, Sijui hao watu wanne wa familia moja wanakula saa ngapi au wewe unawapelekea chakula?. Na Kelele za spika kwenye Misikiti wewe hizo huzisikii? na mungu wao yeye ana masikio kwa sababu wanapiga kelele za kiarabu?
Jibu hoja punguza mihemko. Isitoshe kuhusu Waislam, huwa wanafanya adhana kuwakumbusha waumini muda wa ibada lakini ibada zao hazina kelele kabisa. Hata Wakatoliki na Waluteri husikii kelele za kukwaza
 
Wakatoliki huwa hatuna makelele! Hata kwenye mahubiri yetu (homilia) huwezi kumkuta Katekista/ Shemasi/Padre/Askofu ametokwa na mishipa ya shingo, macho yamemtoka, na mate yamejaa mdomoni; huku akipiga makelele [emoji2788][emoji441] pepoo tookaa! Mbengo zemefongoka! Sharaghabar tashasha! [emoji16]
Wakatoliki wanajua wafanyalo, huwezi kumuomba Mungu kama unamfokea. Kama Baba mzazi tu huwezi kumuomba pesa au hitaji lolote kwa kupayuka je inakuwaje kwa Mungu? Wakatoliki nawaelewa, hawa wengine sijui huo mtindo wa kupayuka waliutoa wapi!!!???
 
LUKA 19:40 - "Nawaambia kwamba hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele"

By choosing understanding over judgment, listening over condemnation, and respect over fear, we foster harmony among all faiths

NB: EMBRACE TOLERANCE
Zaburi 100:1
[1]Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
(A Psalm of praise.) Make a joyful noise unto the LORD, all ye lands.
 
Jibu hoja punguza mihemko. Isitoshe kuhusu Waislam, huwa wanafanya adhana kuwakumbusha waumini muda wa ibada lakini ibada zao hazina kelele kabisa. Hata Wakatoliki na Waluteri husikii kelele za kukwaza
Swala swala swala...
Nyani.... Nyani.... Nyani...
 
Siwashangai wao bali serikali tulivu hii inayokubali mpaka kunguni watangazwe kwa maspika
Upumbavu mtupu

Halafu hawa jamaa wa kanisa hili kuna wakati usiku wanaomba mpaka wanazima taa wanakaa kimya huwa natamani kunyata 😄 🤣
 
Kwanza fahamu hakuna kitu kinaitwa mungu wa walokole na neno walokole si neno rasmi bali ni kejeli na mzaha tu kwa watu waliojitenga na uovu. Kuna kalele za shangwe, kuna kuomba kwa kupaza sauti ni namna tu ya kufanya ibada. Mbona hushangai adhana kwenye loud speaker?
Neno Ulokole /Walokole ni neno rasmi, hutumiwa na waamini wa makanisa ya wokovu na hujiita walokole yaani waliookolewa.
 
Ibada za walokole ukihudhuria lazima uumwe kichwa. Kuna manzi mmoja nilikuwa nafukuzia akanialika kanisani kwao.. ikabidi niende jpili moja kwa mara ya kwanza kwenye kanisa la kilokole. Yaani ile ibada kama 70% ilikuwa ni kelele za kuimba. Maspika makubwa na bado watu mnaimba. Nilijuta kwenda. Sema maumivu yalipoa baada ya kumtafuna yule manzi.
 
Jibu hoja punguza mihemko. Isitoshe kuhusu Waislam, huwa wanafanya adhana kuwakumbusha waumini muda wa ibada lakini ibada zao hazina kelele kabisa. Hata Wakatoliki na Waluteri husikii kelele za kukwaza
Wewe ndiyo Una mihemko kuamini Horn-Speaker misikiti si tatizo bali speaker makanisani ni tatizo. Na si kweli kuwa horn-speaker ni adhana tu kuwakumbusha waislamu. Ningekuelewa sana kama ungeona vyote ni kelele
 
Wakisali ni makelele makubwa sana, mpaka unashangaa, hivi haiwezekani wakiomba waombe kwa Sauti za kawaida tu na sio kupayukapayuka?

Wakianza kuabudu sasa, muziki utawekwa full blast, buzuki kubwa sana halafu ndani ya kanisa unakuta wako watu wanne tu wa familia Moja, hapo watapiga makelele kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa SITA usiku.

Kwa ibada ndefu za makelele zinasababisha maswali mengi sana, huenda Mungu wao Yuko mbali sana. Huenda haelewi Kiswahili hivyo inabidi wampigie makelele mazito ili aweze kubahatisha baadhi ya maneno.
Labda Yuko busy sana hivyo wanamahtua ili awakumbuke...
Maswali ni mengi majibu ni haba.
Najibu kutokana na heading, sijasoma content ndani.

Jibu ni NDIO. Sababu wanaomuomba ni wengi bas inabidi upaze sauti ili yako isikike zaidi kuliko za wengine. Ukiomba kipole pole atawasikia wengine zaidi kuliko wewe
 
Back
Top Bottom