Je, Mungu wa walokole hasikii hadi apigiwe makelele Makubwa?

Je, Mungu wa walokole hasikii hadi apigiwe makelele Makubwa?

Wakisali ni makelele makubwa sana, mpaka unashangaa, hivi haiwezekani wakiomba waombe kwa Sauti za kawaida tu na sio kupayukapayuka?

Wakianza kuabudu sasa, muziki utawekwa full blast, buzuki kubwa sana halafu ndani ya kanisa unakuta wako watu wanne tu wa familia Moja, hapo watapiga makelele kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa SITA usiku.

Kwa ibada ndefu za makelele zinasababisha maswali mengi sana, huenda Mungu wao Yuko mbali sana. Huenda haelewi Kiswahili hivyo inabidi wampigie makelele mazito ili aweze kubahatisha baadhi ya maneno.
Labda Yuko busy sana hivyo wanamahtua ili awakumbuke...
Maswali ni mengi majibu ni haba.
na wakianza kuongea kile kizigua kilichochanganywa na kikurya na kingoni mixa kisenegali hapa ndio utawataka haswaa.
 
Wakisali ni makelele makubwa sana, mpaka unashangaa, hivi haiwezekani wakiomba waombe kwa Sauti za kawaida tu na sio kupayukapayuka?

Wakianza kuabudu sasa, muziki utawekwa full blast, buzuki kubwa sana halafu ndani ya kanisa unakuta wako watu wanne tu wa familia Moja, hapo watapiga makelele kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa SITA usiku.

Kwa ibada ndefu za makelele zinasababisha maswali mengi sana, huenda Mungu wao Yuko mbali sana. Huenda haelewi Kiswahili hivyo inabidi wampigie makelele mazito ili aweze kubahatisha baadhi ya maneno.
Labda Yuko busy sana hivyo wanamahtua ili awakumbuke...
Maswali ni mengi majibu ni haba.
Zaburi 5:11 Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
 
Hivi makanisa ya kikatoliki hayana spika za nje kweli?!
Baadhi yanazo. Ila zinatumika wakati wa ibada/misa tu. Na siyo kwa kupiga disco au kuwaamsha watu alfajiri na kuanza kukemea mapepo.
 
Kuna kanisa hapa la Mungu wa bendera hizo kelele ni Siri yetu tu sisi majirani asee.
Mbaya zaidiwenyekiti wa mtaa ni mwimba kwaya aseee... Tuhurumieni sisi
 
Mathayo 6:7
[7]Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi
.
But when ye pray, use not vain repetitions, as the heathen do: for they think that they shall be heard for their much speaking.
Habari za wakati huu mkuu.
Naona umeweka na mstari kabisa hapa mkuu 😁😁. By the way unafahamu mstari unamaanisha nini kuhusu kupayuka katika muktadha huo hapo?
Ni hivi,tafsiri ya kiingereza umeiweka hapo mwenyewe inaongelea "vain repetitions" ambayo kwa kiswahili tumeichukulia kama kupayuka tunayoijua ya kupiga kelele.
Lakini katika mstari huo huo maneno kupayuka payuka imetumika kumaanisha kurudia rudia maneno na sio kupiga kelele kama watu wengi wanavyoitafsiri.
Hivyo unapoona watu wanasali wanaongea kwa sauti ya juu usikwazike ndugu.Mbona ukiishi karibu na vibanda vya mpira huwezi kulalamika wanapiga kelele ,jibu ni kwa sababu unafurahia mpira na hivyo huoni kama ni kero.
Usikasirikie watu wakifanya ibada yao.
 
Unajua kaka, ibada ni jambo la moyo na kila mtu ana njia yake ya kujieleza mbele za Mungu. Wengine wanapenda utulivu, wengine wanafurahia kumwimbia na kumsifu Mungu kwa nguvu na sauti, si kwa sababu Mungu hasikii bali kwa sababu ndivyo mioyo yao inavyopata pumziko. Kama wewe unapendelea utulivu, hiyo pia ni njia halali kabisa ya kuabudu. Sidhani kama kuna njia moja sahihi—cha muhimu ni moyo wa mtu na nia yake mbele za Mungu.
 
Back
Top Bottom