Je, Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo??

Je, Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo??

Nimefuatilia kidogo mjadali huu ili nijifunze,Ila nimegundua watu hawaonyeshi mistari kutetea hoja zao wanaleta story nyingi sana kichwani mwao,wacha niendelee kujifunza
 
Nakubaliana na hoja yako, na hii inatokana uelewa wa watu, si kweli kwamba Musa aliandika kitabu kinaitwa mwanzo la hasha, ni jina lilopewa na waliofanya collections ya maaandashi hayo ya neno la Mungu.
Nimekuelewa mkuu kuwa kimeandikwa na wanafunzi wake.... Je hao wanafunzi wake waliandika kipindi Musa akiwa hai bado maana mfano hiyo Issue ya wakaldayo walianza kuwepo miaka zaidi ya 400 baada ya Musa kufa je hao wanafunzi wake bado walikuwepo?? Hilo ndio nalotaka kufahamu kwamba final copy ya genesis ilitengenzwa na musa mwenyewe au kuna watu walimtumia musa tu kama moja ya chanzo cha taarifa zao ndio wakaja na final copy ya kitabu cha Mwanzo??
 
kuielewa biblia unahitaji KARAMA NA UJAZO WA ROHO MT.
Na Wala SIYO machapisho ya maproffersor
ni ajabu MTU kama wewe na mwanaume kuamin maproffersor ZAIDI kuliko ROHO MTAKATIFU.
na wengi wamekuwa wagumu kuelwa/kutambua
kuhusu ROHO MTAKATIFU
Kuna mawili hapa.

Kuna imani. Kuna fact.

Imani siwezi kubisha. Una haki ya kuamini unavyotaka.


Kwa fact. Roho Mtakatifu hujaweza kuthibitisha yupo.

Kama unaweza, thibitisha.
 
Kuna mawili hapa.

Kuna imani. Kuna fact.

Imani siwezi kubisha. Una haki ya kuamini unavyotaka.


Kwa fact. Roho Mtakatifu hujaweza kuthibitisha yupo.

Kama unaweza, thibitisha.
sasa hapo Mr kiranga utataka mabishano.
hata nikikupa Verse za kwenye Bible bado hutokaa uamini kuwa huyo roho yupo.
kuelwa ufalme wa mbinguni/mambo ya rohoni inaitaji Sanaa uwe MTU wa rohoni wengi huwa wanashindwa kuelwa mambo ya rohoni coz huyachukulia ki mwili.ndipo hapo mnaanza kusema kuwa fact/mkanganyiko upo HAPANA.
 
Kuna mawili hapa.

Kuna imani. Kuna fact.

Imani siwezi kubisha. Una haki ya kuamini unavyotaka.


Kwa fact. Roho Mtakatifu hujaweza kuthibitisha yupo.

Kama unaweza, thibitisha.
Swali la Roho Mtakatifu ni la kiimani kwa maelezo yako umekubali uwezi kubisha

Sasa swali la kutaka kuthibitishiwa la Nini?
 
Musa alipokuwa mlima Sinai siku 40 Mungu alimweleza habari zote tangu mwanzo. Yaani alimweleza asili ya mwanadamu ilianzia kwa Adamu! Alimpa mtiririko wote jinsi mambo yalivyokuwa. Musa aliandika kile alicho ambiwa.
Una ushahidi wa kimaandiko ku support hoja yako?
 
Kwanza maana halisi ya Mtume ni nini ? Kumbuka Yesu aliongelea mambo yaliyopita na yajayo. kwa hiyo Musa kipindi anawasilina na Mungu sio kwamba alipewa maagizo tu, fahamu kwamba Kuna vitu vingine alihitaji kufahamu hivyo alipewa nafasi ya kuuliza na akaelezwa. katika dhana kama hiyo Kama unatafakari kwa undani enzi hizo asingekua na cha zaidi ya kuuliza historia ya kufahamu chimbuko la wana Israel. pili, muda aliokaa mlima Sinai ni muda mrefu mpaka wafuasi wake waka kata tamaa, jiulize utakua ni muda gani watu wakate tamaa baada ya kutolewa kwenye vizuizi vya hatari na maajabu dhahiri na walikuwa wana msujudia Mungu wao kwa ukuu wake na miujiza mingi. hapa inaonyesha kwamba alichukua muda mrefu sana akiwa mlimani. pia kumbuka kwamba hawa Mitume walikua wanachaguliwa na mungu mwenyewe kuanzia utungaji wa mimba mpaka ukubwani, kwa hiyo karma waliyo kua nayo ilikua ni yake yeye mwenyewe Mungu kwa ajili ya kazi yake.
Ni kwa fikra zangu tuu.
Bora zibaki tu kuwa firka zako..Maana tuna ambiwa Musa alipotoka kuonana na Mungu alikuja akiwa amebeba zile mbao mbili zenye amri za Mungu tu na sio kingine
 
wewe nawe stori yako bila kuweka deuterenomy 34(kumbukumbu la torati 34) inakuwa haijakamilika
hivi umeshindwa kuona kuwa sio tu kitabu cha mwanzo isipokuwa vitabu vyote vinavyosemwa vimeandikwa na musa ni feki?
musa hakuandika kitabu chochote,stori zake zimejaa third person narrations
 
Kitabu cha Mwanzo ndiyo kitabu cha kwanza cha Agano la Kale na kiliandikwa na Nabii Musa.

Kinatoa historia ya mianzo mingi ya mambo, kama vile uumbaji wa dunia, kuwekwa kwa wanyama na mwanadamu juu ya dunia, anguko la Adamu na Hawa, kufunuliwa kwa injili kwa Adamu, mwanzo wa makabila na jamii, asili ya lugha mbalimbali katika Babeli, na mwanzo wa familia ya Ibrahimu inayoongoza kuanzishwa kwa nyumba ya Israeli.

Nafasi ya Yusufu kama mhifadhi wa Israeli inadhihirishwa katika Mwanzo.

Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha na kubainisha taarifa iliyoandikwa katika Mwanzo (1 Ne. 5; Eth. 1; Musa 1–8; Ibr. 1–5).

Katika Kitabu cha Mwanzo, mlango wa 1–4 inahusisha uumbaji wa ulimwengu na kukua kwa familia ya Adamu.

Mlango wa 5–10 inaandika historia ya Nuhu. Mlango wa 11–20 inamtaja Ibrahimu na familia yake hadi wakati wa Isaka.

Mlango wa 21–35 inafuatilia familia ya Isaka. Mlango wa 36 unasimulia juu ya Esau na familia yake.

Mlango wa 37–50 inasimulia juu ya familia ya Yakobo na kutoa historia ya Yusufu kuuzwa Misri na nafasi yake katika kuiokoa nyumba ya Israeli.
jua,nyota na mwezi viliumbwa siku ya nne(kwa mujibu wa biblia)
siku tatu kabla mungu wako wa israeli alikuwa anaonaje wakati kulikuwa na giza?
 
jua,nyota na mwezi viliumbwa siku ya nne(kwa mujibu wa biblia)
siku tatu kabla mungu wako wa israeli alikuwa anaonaje wakati kulikuwa na giza?
Wewe mungu wako aliumba nini? Na kabla ya hilo giza mungu wako alikuwa wapi?
 
Wewe mungu wako aliumba nini? Na kabla ya hilo giza mungu wako alikuwa wapi?
wewe ndio umtetee mungu wako hapa
alionaje wakati kulikuwa na giza?
watu weusi acheni kujidhalilisha na vitabu visivyowahusu,unaona unavyoshindwa kumtetea mungu wa wayahudi ambaye hakuhusu!!!!!!!
 
Back
Top Bottom