Je, muungano wa Tanganyika na Zanzibar upo kwa vigezo vipi?

Bora Kurudi kwetu mbona tunaomba kila siku lkn Tanganyika vinganganizi
Tung’ang’anie kwa faida ipi wakati wewe umeshindwa kutaja hata faida moja ambayo Tanganyika inapata, ila mserereko wote wanaupata wala urojo? Hapa suala ni kujadili ili hoja ikionekana kupitia huu mjadala basi wenye maamuzi bungeni na serikali kuu wachukue hatua. Ni bora tuungane tuwe serikali moja au unyonyaji na utegemezi wa wala urojo ukome!
 
Uchaguzi wa mwakani uwe kama Kura ya maoni wasiotaka muungano wachague upinzani wanaotaka muungano wachague CCM
 
Uchaguzi wa mwakani uwe kama Kura ya maoni wasiotaka muungano wachague upinzani wanaotaka muungano wachague CCM

Na atayehesabui kura ni huyo aliyeuweka huo muungano CCM
 
Aliyeipokonya Tanganyika identity yake ni nani ??
 

Ukawaambie wajitoe kutoka wapi na mumuweka majeshi yenu kila mtaa , usalama wa Taifa ulipiga kambi huku wakati wa uchaguzi na wapo kila mtaa mpaka leo. Mlikodi majeshi ya Burundi mkayaleta zanzibar kupiga watu kudhibiti wapinzani kwa nini ??

Si mliondowe jeshio lenu na polisi wenu pamoja na usalama wa taifa wenu , wengine wanavaa rubega za kimasai ??
 

Ndivyo ilivyokuwa kabla ya huu uvamizi wa Nyerere mwaka 1964 aliouita Mapinduzi na akaubatiza jina la MUUNGANO
 

Kwanini Mwinyi Mtanganyika kutoka Mkuranga ni Raisi Zanzibar na aliwahi kuwa Mbunge wa Mkuranga kabla na kwa sheria za uchaguzi hawezi kugombea Zanzibar msikilize huyu Ali Karume



View: https://youtu.be/C8SWv9uxpoo
 

Muungano hauna haja ya kuwepo kila mtu aende mambo yake , kwani huwezi kuunganisha nchi ya watu karibu milioni 60 ukaungana na watu milioni 2 hawafiki ,
 
Muungano hauna haja ya kuwepo kila mtu aende mambo yake , kwani huwezi kuunganisha nchi ya watu karibu milioni 60 ukaungana na watu milioni 2 hawafiki ,
Sawa, ni either hivyo, au tuungane tuwe nchi moja chini ya Serikali na Rais mmoja.
 
Sawa, ni either hivyo, au tuungane tuwe nchi moja chini ya Serikali na Rais mmoja.

Tuwe nchi moja sawa kwa kugeuza Zanzibar kuwa Tanganyika yaani hivi ilivyo Sasa kwa Tanganyika kuvaa jojo la Muungano , Sasa iwe zamu ya Zanzibar kulivaa joho, kwa kuweka makao ya serikali yawe Zanzibar na wizara zote Za muungano ziwe na makao Makuu Zanzibar yaani wizara Za Zanzibar ziwe Za Muungano, bunge la Zanzibar ndio liwe bunge la Muungano na makao yake yaweko Zanzibar. Raisi wa Zanzibar ndio awe Raisi wa Muungano. Tanganyika ipoteze kila kitu Kama ilivyopoteza Zanzibar hivi sasa
 
Utakuwaje na Makao ya Rais wa Muungano sehemu ambapo tayari kuna makao ya Rais mwingine?, utawekaje makao ya wizara ya Muungano sehemu ambapo tayari kuna makao ya wizara nyingine? Utawekaje makao bunge la Muungano sehemu ambapo kuna makao ya bunge lingine?
Utakuwaje na maRais wa Muungano Wawili tena wote wametoka Zanzibar?

Ukifanya hivyo italazimu sasa Tanganyika nayo iwe na serikali yake isiyo ya Muungano, means serikali 3, ambayo itakuwa ni ukichaa..

Suluhisho, Tuwe na nchi moja chini ya Rais mmoja au kila mtu awe kivyake pasiwe na unyonyaji na utegemezi..
 

Kwani mlipoulazimisha huu muungano uliopo Tanganyika ilikuwa Haina Raisi, Haina bunge ??
 
Kiuhalisia hii "Tanganyika" yote iwe ni Zanzibar, kama ilivyokuwa kabla ya wajerumani kuikata na kujigawia hili pande linaloitwa bara.

Hata jina "Tanganyika" hakuna anayejuwa limetokea wapi, hii yote ilikuwa ni Zenj bar, yaani bara la Zenj.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…