Je, mwaka 1993 Simba ilicheza fainali za michuano ipi Afrika na Stella ya Ivory Coast?

Je, mwaka 1993 Simba ilicheza fainali za michuano ipi Afrika na Stella ya Ivory Coast?

Huwa nadhani unajuwa mpira kumbe magumashi tu, mwaka 1993 Pamba ya Mwanza ndio ilishiriki kombe la washindi na Malindi walishiriki club bingwa.

Hivi MNA matatizo gani kichwani?
mbumbumbu wanatafuta faraja isiyokuwepo wasameheni bure
 
Mashabiki wengi wa simba wamepaniki Yanga kufuzu hatua ya nusu fainali.
Hata humo kwenye dalala ukiongea habari za mpira hasa Yanga kufuzu na wao kuishia mikononi mwa waarabu,Simba wanapanick lugha yao wanaiga ya ya yule mlopokaji wao ile sizitaki mbichi hizi kwa Yanga kuingia nusu fainal ya shirikisho.
 
Simba ilifika fainali ya kombe la CAF cup

Hapo zamani kulikuwa na michuano miwili Africa cup of champions club ambayo kwasasa inaitwa CAF champions league na shindano la pili ilikuwa ni Africa cup winner's cup ambayo kwasasa ni CAF confederation cup. Lakini mwaka 1992 Caf wakaanzia mashindano mengine ambayo yalikuwa kwa timu ambazo hazifuzu mashindano ya CAF interclub championship ( klabu bingwa na shirikisho) na mashindano hayo yalidumu kwa miaka 12 tu (1992-2003)

Wakati Simba anacheza fainali ya CAF cup mwaka 1993 dhidi ya Stella club, timu ya Zamalek alikuwa ndio bingwa wa klabu bingwa mwaka huo 1993 huku Al Ahly akiwa ndio bingwa wa kombe la shirikisho mwaka 1993 na hivyo wakakutana kwenye CAF super cup na Zamalek kuwa bingwa wa jumla.

Kwahiyo CAF cup aliyocheza Simba sio sawasawa na kombe la shirikisho kwasasa. View attachment 2605466
Asante saaana kwa majibu mazuri mkuu. Japo hili kwa mikia yoyote hatataka kuipitia. Hata mlete mada ataikimbia hii
 
The 1993 CAF Cup was the second football club tournament season that took place for the runners-up of each African country's domestic league. It was won by Stella Adjamé in two-legged final victory against Simba SC.

Sasa kwa maelezo hayo, mbona hiyo ndio Kombe la Shirikisho la CAF?

Na Simba alifika hadi fainali? Kwanini mseme Tz haijawahi kufikisha timu fainali? Malishusha CV taifa letu, mimi sio Simba, ila Tz lazima ijivunie kwamba iliwahi kufikisha timu fainali
Sasa unabishana na CAF wenye kombe lao?

Wao ndio wanasema hayo maneno na wala sio Yanga.
 
Simba ina historia ya kuchezà mara nyingi robo fainali za mashindano mbalimbali ya CAF.

Mwaka 1993 kuna mashindano ambayo Simba ilifika fainali, je yale yalikuwa ni mashindano gani?

Kwanini Yanga itajwe kwamba ni nchi ya kwanza Afrika Mashariki kufika hatua ya Nusu fainali ya mashindano ya CAF?
√ . Hiyo ilikuwa Karne ya 20
√. Karne hii ya 21 ni YANGA.
√. CAF waliubadili mfumo na kuachana na huo mfumo wa Karne ya 20
 
Kwenye mashindano ambayo Simba na Stella wakicheza fainali, je nchi gani za Afrika ya Kaskazini zilishiriki?
Simba kwenye nusu fainali ya kombe la CAF mwaka huo ilikutana na USM El Harach ya Algeria na kuitoa kwa jumla ya magoli 3-1,hii tu inaonesha timu za Kaskazini mwa Afrika zilishiriki tofauti na uongo anaoeneza ndugu Manara
 
nchi hii ina wajinga wengi sana,
kwaio kagame cup sio kombe kwa sababu kagame ndio anafadhili?
hata hii total caf cl nalo sio kombe kisa total wanafadhili?
nadhani manara alikua sahihi, kule wenye akili ni wawili tu
kuna vitu havihitaj ushabiki, mwaka 1993 bingwa wa clab bingwa alikua zamalek na shirikisho alikua al ahly, mpaka hapo ushajua simba hakucheza fainali ya shirikisho
 
Wewe huna akili, NBC wanadhamini ligi ya Tanzania na siyo wao ndio wametowa kombe lisimamiwe na TFF, pumbavu kabisa.
 
The 1993 CAF Cup was the second football club tournament season that took place for the runners-up of each African country's domestic league. It was won by Stella Adjamé in two-legged final victory against Simba SC.

Sasa kwa maelezo hayo, mbona hiyo ndio Kombe la Shirikisho la CAF?

Na Simba alifika hadi fainali? Kwanini mseme Tz haijawahi kufikisha timu fainali? Malishusha CV taifa letu, mimi sio Simba, ila Tz lazima ijivunie kwamba iliwahi kufikisha timu fainali
Swali langu ni kwanini Stella hakucheza mechi ya CAF super cup katika ufunguzi wa pazia jipya la mashindano ya CAF? kama ingekuwa ni mashindano yenye hadhi kwa CAF baada ya klabu bingwa basi bingwa wa CAF cup angeshiriki kwenye CAF super cup lakoni badala yake CAF super cup ilikuwa ikishirikisha bingwa wa Africa cup winner's cup VS Africa cup of champions club. Swali langu ni kwanini?

Halafu hilo neno second lisikuchanganye ukachukulia kama walimaanisha ukubwa wa michuano bali walimaanisha ni msimu wa pili kwa maana msimu wa kwanza ilikuwa mwaka 1992 na ndio mwaka ambao yalianzishwa hayo mashindano
 
kuna vitu havihitaj ushabiki, mwaka 1993 bingwa wa clab bingwa alikua zamalek na shirikisho alikua al ahly, mpaka hapo ushajua simba hakucheza fainali ya shirikisho
Onesha ushahidi kuwa Bingwa wa Shirikisho alikuwa Al Ahly sio kuleta maneno matupu
 
Onesha ushahidi kuwa Bingwa wa Shirikisho alikuwa Al Ahly sio kuleta maneno matupu
Huu hapa,
JamiiForums-1088565506.jpg
 
Back
Top Bottom