Strong and Fearless
JF-Expert Member
- Apr 24, 2017
- 895
- 2,218
Waishi ndani ya uwezo waoInategemea na kipato Cha mume wake.
Hakika,Waishi ndani ya uwezo wao
Kama mwanamke lazima achangie kifedha ili ndoa ifanye kazi, basi mume naye lazima ashiriki sawa kwenye majukumu ya nyumbani na malezi. Ndoa siyo biashara ya kugawana gharama, ni kushirikiana katika maisha kwa kila hali.Kama mke ana uwezo wa fedha, kama vile kufanya biashara au kufanya kazi ya kuajiriwa, ni vizuri akishirikiana na mme wake katika maendeleo na matumizi ya nyumbani.
Sahihi kabisa, mimi binafsi siwezi kukaa na amani ninapo chukua au kupewa hela na mwanamke.Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Ninakubaliana kabisa na wewe. Hasa katika ndoa, ni muhimu kwa mke na mume kushirikiana na kusaidiana katika kupanga matumizi ya fedha na kutunza familia. Mke anaweza kutoa msaada mkubwa kwa mume kwa kumsaidia kupanga matumizi, kuhakikisha fedha zinatumika vizuri, na kuleta usawa ndani ya nyumba. Ushirikiano huu unasaidia kudumisha amani na mafanikio ya kifamilia.Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Haya ndio mambo ya kuangalia kabla ya kuoa, mwanamme asije akaona anadharauliwa sababu mwanamke hana muda kupika yupo anatafuta shilingiHakika,
Changamoto inakuja mwanamke anapokuwa na kipato kikubwa kuliko mume wake.. huo uwezo wao utabalance vipi wakati mwanaume ndio inatakiwa uwe na mchango mkubwa kuzidi mwanamke
Kama mwanamke anafanya kazi au biashara inayo muingizia kipato ni nirazima kipato chake kichangie maendeleo ya familia tofauti na hapo hiyo kazi na biashara hatoifanya na atakaa nyumbani kulea watoto kama hataki aondoke akaolewe na mwingine.Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Mwanamke anayefanya kazi na kupunguza muda wa kulea watoto, anapata fedha ambazo anaweza kuzitumia kwa ajili ya familia yake, kujihudumia mwenyewe, au kuwekeza katika maendeleo ya familia. Hizo fedha zinaweza kutumika kugharamia mahitaji ya watoto, malipo ya nyumba, chakula, na hata masomo kwa watoto. Aidha, kazi inamfaidi mke mwenyewe kwa kumwezesha kuwa na uhuru wa kifedha, kujiendeleza kitaaluma, na kutoa mchango wa kiuchumi kwa familia yake. Kazi pia inamfaidi mume kwa kuwa na mchango wa ziada kwenye gharama za familia, huku pia ikimsaidia mke kumsaidia katika majukumu ya nyumbani. Kazi ya mke inafaidi familia kwa ujumla kwa kuongeza mapato na usawa katika majukumu ya kifamilia.Swali:
Mwanamke anayefanya kazi na kupunguza mda wa kulea watoto na mume wako:
1. Anapeleka wapi fedha anazopata?
2. Kazi inawafaidisha nini watu wake?
Ukijibu hayo maswali utakuwa umejibu swali lako
Nimeona wanaume wengi sana wakifika mbali zaidi kwa kusikiliza wake zao kuliko marafiki. Tatizo waume wengi masikio yao yapo kama mapamboNinakubaliana kabisa na wewe. Hasa katika ndoa, ni muhimu kwa mke na mume kushirikiana na kusaidiana katika kupanga matumizi ya fedha na kutunza familia. Mke anaweza kutoa msaada mkubwa kwa mume kwa kumsaidia kupanga matumizi, kuhakikisha fedha zinatumika vizuri, na kuleta usawa ndani ya nyumba. Ushirikiano huu unasaidia kudumisha amani na mafanikio ya kifamilia.
Wanawake wengi wanaofanya kazi mara nyingi ni kwaajili ya uhuru wa kipato na kuwekeza kwaajili ya kipindi cha kiangazi. (Mume kufariki, kuugua, kukimbilia michepuko) kwaajili yake, wanaomtegemea na watoto wakeKama mwanamke anafanya kazi au biashara inayo muingizia kipato ni nirazima kipato chake kichangie maendeleo ya familia tofauti na hapo hiyo kazi na biashara hatoifanya na atakaa nyumbani kulea watoto kama hataki aondoke akaolewe na mwingine.
Mwanamke nikisha muoa ni lazima aende kwenye ndoto zangu sio aje kuwa mshindani wa ndoto zangu.
Alafu ww mwanamke kipato chako ambacho akichangii maendeleo ya familia kwa ajili future ya watoto wenu unakuwa unatafuta kipato cha nini hasa?
Vipi kazi za nyumbani naye mwanaume atafanya kama mkewe anavyofanya?Kama mke ana uwezo wa fedha, kama vile kufanya biashara au kufanya kazi ya kuajiriwa, ni vizuri akishirikiana na mme wake katika maendeleo na matumizi ya nyumbani.
Eti kipindi cha kiangazi 😅😅😅Wanawake wengi wanaofanya kazi mara nyingi ni kwaajili ya uhuru wa kipato na kuwekeza kwaajili ya kipindi cha kiangazi. (Mume kufariki, kuugua, kukimbilia michepuko) kwaajili yake, wanaomtegemea na watoto wake
Ndiyo maana wanashauriwa oa unayemudu , sio oversizeHakika,
Changamoto inakuja mwanamke anapokuwa na kipato kikubwa kuliko mume wake.. huo uwezo wao utabalance vipi wakati mwanaume ndio inatakiwa uwe na mchango mkubwa kuzidi mwanamke