Halafu tukisema humu mwanamke mwenye kazi/kipato hana faida yoyote kwenye ndoa ni mara mia ya mama wa nyumbani, tunaonekana ni watu wa ajabu...!!Tupo kwenye ulimwengu ambao tuna fursa sawa za elimu, biashara, uongozi n.k. Kwa nyakati hizi mwanamke mwenye kipato sio hiari tena kushiriki kujenga uchumi wa familia yake.
Nimeshuhudia huu ujinga mtaani kwangu, mume uchumi umeyumba ikabidi watoto warudi shule za kayumba kutoka shule binafsi walikokuwa wanasoma tokea wakiwa wadogo, ili kukabiliana na ukata.
Mke anafanya biashara ya nafaka na kukopesha ela za riba, anakipato ambacho kama wangeunganisha nguvu wale watoto wasingerudi kayumba. Inasemekana mama alinukuliwa kwenye vyama vya kinamama akisema hawezi kusomesha watoto hilo sio jukumu lake.
Huyo jirani yako naamini ni miongoni mwa wale wanaume ambao wakati anataka kuoa kigezo kimoja wapo alichokuwa anakizingatia ni kwamba mwanamke lazima awe mpambanaji...!! Haya sasa apambane sasa awarudishe watoto wake huko private, huyo mkewe mpambanaji ana malengo yake binafsi hataki kuingiliwa kwenye hela zake.