Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Ikiwa tunaongelea 50/50, basi inapaswa kuwa sawa kwa pande zote. Kama mwanamke anachangia kifedha na kazi za nyumbani, basi ni haki pia mwanaume achangie katika malezi ya watoto na majukumu ya familia. Usawa unapaswa kuwa katika kila eneo la ndoa, sio tu kwenye pesa, bali pia katika kulea watoto na kusaidiana kwa kila mmoja. Kila mmoja anapaswa kuchukua jukumu lake bila kumwacha mwingine kubeba mzigo peke yake.
Sure,
 
Kama najimudu kiuchumi pesa ya mwanamke ya nini.
Mke kufanya KAZI ni sababu ya umasikini tu.
Mfano namiliki biashara kubwa kubwa miradi mikubwa majengo nk hio Kazi yake Ina msaada

Unapotaka mwanamke asifanye kazi za kiuchumI huko ndiko kumjengea umaskini na kusababisha nchi hii kuwa na tegemezi wengi zaidi. Mwanamke anatakiwa afanye kazi za kiuchumi bila kujali fedha yake inafaida kwako ama laa. Usikae na mwanamke mzigo , mwanamke afanye kazi za kiuchumi alipie Kodi Tra , na wewe hivyo hivyo Tabia za kufuga wanawake ndani wasifanye kazi zilishapitwa na wakati . Nchi hii inahitaji maendeleo , hata familia yake kwa wazazi wake sio vibaya akawasaidia
 
Kwanini tuwape kipaumbele watu ambao hawawajibiki kujenga uchumi wa familia?? Tunawapa kipaumbele ili iweje?
Kaka moja ya vitu ambavyo binafsi vinaniumiza sana na kunifanya niichukie sana hii dunia yetu ya leo.. ni hili suala la kuwapendelea wanawake kwenye fursa za kuichumi ilihali huo uchumi wao hauna manufaa yoyote kwenye familia zao unless awe ni single mother.

Yaani sasa hivi kila fursa ya kiuchumi kipaumbele ni wanawake.. wanawake, mwanaume amesahaulika kabisa, halafu hapo hapo eti mwanaume huyo anapaswa kuwa main provider wa familia..!! Sasa ndio nini?

Yaani wametengeneza Mfuno unao mmarginalize mwanaume kiuchumi na kumpandisha mwanamke kiuchumi, halafu mwanaume bado ndio aendelee kuidumia familia kiuchimi wakati huo mwanamke kutoa pesa zake kwenye familia ni ihari... huu ujinga umeleta mvurugano mkubwa sana kwenye jamii na impact yake imeshaanza kuonekana.
 
ishi mwenyewe mkuu🤣
 
Ndoa na mwanamke msomi au mwenye hela ni Mungu mwenyewe aingilie kati la sivyo inavunjika wakati wowote.
Mweleze kuwa mafanikio ya ndoa hayategemei elimu au kipato cha mwanamke bali hekima, maelewano, na nia njema ya wanandoa wote wawili. Kama ndoa inavunjika kwa sababu mwanamke ana elimu au kipato, basi tatizo si mwanamke bali mwanaume asiye na uhakika na nafasi yake kama mume. Ndoa imara inajengwa kwa ushirikiano, si kwa hofu ya mmoja kufanikiwa kuliko mwingine.
 
Swali ni dogo tu, nini mchango wako kama mama kwa familia yako, ikiwa kipato chako hakionekani na muda wa familia umeuweka kwenye ajira??

Hayo maelezo yako ya manyanyaso na upendo ni ishu nyingine ya maswala ya kijinsia!! Hatujadili hayo hapa pls!!
Ukifa au ukipotelea kwa mchepuko faida ya hiyo hela itaonekana
 
Kama mnataka wanaume wawajibike zaidi kujenga uchumi wa familia basi wapewe kipaumbele kwenye ajira, vyeo na mishahara.

Kwanini tuwape kipaumbele watu ambao hawawajibiki kujenga uchumi wa familia?? Tunawapa kipaumbele ili iweje?
Kipaumbele kwenye ajira na mishahara kinapaswa kutegemea uwezo na sifa za mtu, siyo jinsia. Kujenga uchumi wa familia ni jukumu la wote kulingana na uwezo wao. Kama mume anapaswa kuwajibika kifedha zaidi, haimaanishi mwanamke hana mchango au hastahili nafasi sawa kazini. Ajira na vyeo vitolewe kwa haki, si kwa misingi ya nani anapaswa kulipa bili nyumbani.
 
Yaani mtu na mkewe halafu changu chetu na chako chako.. huo ji upuuzi bora ukae nyumbani tu usubiri cha kupewa huku ukihudumia familia kwa ukaribu.

Na nyumbani sio kazi zote atafanya yeye iwapo nyote ni watafutaji, siku hizi kazi nyingi zinamalizwa na mashine labda muwe mnaishi kijima.
Ndoa si biashara ya kugawana mizigo kwa usawa wa asilimia. Kila mmoja anatoa kulingana na uwezo wake, na mchango wa mwanamke si lazima uwe wa kifedha. Kama mke anahakikisha nyumba iko sawa, watoto wanalelewa vyema, na familia inapata utulivu, huo tayari ni mchango mkubwa kuliko pesa. Familia ni ushirikiano, si hesabu za kugawana bili.
 
Kila mtu awajibike kwa familia yake, be proud kuhudumia familia yako. Ukishaweka material things mblele na ubinafsi kwenye ndoa yako unaharibu ustawi wa familia yako.
Ndio maana mfumo wa asili wa familia umeweka majukumu wazi—mwanaume ndiye mtoa huduma mkuu, na mwanamke ana hiari ya kusaidia kulingana na uwezo wake. Tatizo linakuja pale watu wanapolazimisha usawa wa majukumu ya kifedha lakini siyo usawa wa majukumu mengine ya kifamilia.
 
Lakini sheria ya ndoa haitambui hiyo mifumo ya kila ndoa. Nyie ni parasites na selfish sana
Sheria ya ndoa inaweka misingi ya haki na wajibu kwa wote, lakini haibadilishi ukweli kwamba mwanaume ndiye mtoa huduma mkuu katika familia. K
 
Hakuna cha hiari, wewe ni mbinafsi tu. Suala la ndoa halina changu, wala chake. Kama unatoka kutafuta lazima utoe, utaishiaje kusema unatoka kwenda kufanya kazi, unaacha watoto nyumbani halafu unachopata kiwe hiari kutoa? Mna kichaa kizazi hiki kwa sababu hamkuelewa kwanini dunia imewapa fursa za kufanya kazi, nenda katafute urudishe kwenye ndoa na familia yako. Huwezi kaa nyumbani usubiri kuletewa, msitupunguzie mzunguko wa fedha.
Kutoa ni jambo la hiari kwa mwanamke kwa sababu mwanaume ndiye mwenye jukumu la kifedha katika ndoa. Mwanamke anapochangia, anafanya hivyo kwa upendo na si kwa lazima. Kama fursa za kazi zimetolewa kwa wote, haimaanishi majukumu ya asili yamebadilika.
 
Kaka moja ya vitu ambavyo binafsi vinaniumiza sana na kunifanya niichukie sana hii dunia yetu ya leo.. ni hili suala la kuwapendelea wanawake kwenye fursa za kuichumi ilihali huo uchumi wao hauna manufaa yoyote kwenye familia zao unless awe ni single mother.

Yaani sasa hivi kila fursa ya kiuchumi kipaumbele ni wanawake.. wanawake, mwanaume amesahaulika kabisa, halafu hapo hapo eti mwanaume huyo anapaswa kuwa main provider wa familia..!! Sasa ndio nini?

Yaani wametengeneza Mfuno unao mmarginalize mwanaume kiuchumi na kumpandisha mwanamke kiuchumi, halafu mwanaume bado ndio aendelee kuidumia familia kiuchimi wakati huo mwanamke kutoa pesa zake kwenye familia ni ihari... huu ujinga umeleta mvurugano mkubwa sana kwenye jamii na impact yake imeshaanza kuonekana.
Kuna mpango wangu mmoja hivi wa kuanzisha association nauandaa, kwa sasa nipo kwenye hatua ya mwanzo ya kuandika miongozo, malengo na kuweka kila kitu kiwe katika document. Mpango huu nimeupa jina la Men for Greatness(M4G) lengo kuu ni kumrudisha mwanaume katika nafasi yake na kumwondoa kwenye matrix ya feminism world ambayo akili ya mwanaume imefungiwa kwa sasa. Mimi naamini kabisa ili jamii yetu iwe na ustawi mzuri lazima tuwe na man superiority kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa

Association hii itajumuisha
-kutoa mahitaji ya kielimu kwa watoto wa kiume
-kuanzisha miradi ya kibiashara ambayo wanufaika watakua ni wanaume tu
-kusaidia kisheria wanaume especialy kwenye kesi zinazohusu mahusiano na ndoa
-ku-push ajenda zinazolinda masilahi ya mwanaume mfano upimaji wa dna usiokua na makando kando,
-kutengeneza platform kwa ajiri ya kuwawezesha wanaume mikopo, kupata ajira, scholarship n.k
-kusambaza elimu ya wanaume kujua thamani yao
na mambo mengine mengi.

Mpaka kufikia january mwakani nafikiri nitakua nimekamilisha mambo muhimu. Kelele za ubaguzi wa kijinsia nitazipuuzia tu maana ubaguzi wa kijinsia ndicho kitu kinachofanywa kwa sasa kwa kupewa jina la women empowerment
 
Mweleze kuwa mafanikio ya ndoa hayategemei elimu au kipato cha mwanamke bali hekima, maelewano, na nia njema ya wanandoa wote wawili. Kama ndoa inavunjika kwa sababu mwanamke ana elimu au kipato, basi tatizo si mwanamke bali mwanaume asiye na uhakika na nafasi yake kama mume. Ndoa imara inajengwa kwa ushirikiano, si kwa hofu ya mmoja kufanikiwa kuliko mwingine.
Ndio ukweli mwenye ukubali ukatae,ndio ipo hivyo Ndoa na mwanamke msomi au mwenye hela ni Mungu mwenyewe aingilie kati la sivyo inavunjika wakati wowote.

Majority ya wanawake wasomi na wenye hela kichwani mwao wanaamini wao ni Strong Independent Woma.Ukiona mwanamke msomi ana hela halafu still ni submissive kwa mmewe, jua malezi ya wazazi wake plus ana makuzi mazuri ya kumjua Mungu,kinyume chake hata uongee nae vipi huwezi mbadilisha na ukijaribu kutumia nguvu utajitafutia matatizo ndio maana wengi wao wanagongwa na kuachwa.

Wewe unafikiri why US na nchi ya Ulaya,ndoa kwao zimekuwa changamoto na kila siku rate ya kuoana inazidi kushuka.Pili kafuatile hizi Podcast na Interview za hawa wanaoitwa Passport Bros,zipo YouTube na kuna Podcast nyingi sana.
 
Sikubaliani na mtazamo wako. Ndoa haiwezi kutegemea tu kipato au elimu ya mke au mume. Ndoa inahitaji maelewano, upendo, na heshima kutoka pande zote mbili. Mwanamke mwenye elimu na kipato anaweza kuwa mke mwema kama ana maadili mazuri na anaheshimu ndoa yake. Tatizo haliko kwenye pesa au elimu, bali katika jinsi mtu anavyojijua na anavyohusiana na mwenza wake. Kila ndoa ina mfumo wake na inategemea pande zote mbili kuishi kwa usawa na kushirikiana.
 
Kutoa ni jambo la hiari kwa mwanamke kwa sababu mwanaume ndiye mwenye jukumu la kifedha katika ndoa. Mwanamke anapochangia, anafanya hivyo kwa upendo na si kwa lazima. Kama fursa za kazi zimetolewa kwa wote, haimaanishi majukumu ya asili yamebadilika.

Kutoa si jukumu la asili. Haya majukumu yana maana, maana ya kutoa inatokana na physical advantages ambazo Mwanamume aliumbwa nazo zikawa favoured na mazingira, ila haikumaanisha kuwa Wanawake hawawezi. Ujio wa mashine na Maendeleo ya Teknolojia yamefanya zoezi la utafutaji na uzalishaji liwe rahisi kwa jinsia zote. So mantiki ya kutoa haipo kwa Mwanamume pekee tena kama ilivyo awali. Na kutoa kunatokana na kupata, nowadays wote tunapata. So, kutoa kwako sio hiari; usisingizie asili, kutoa ni social construct. Majukumu ya asili ni pamoja na kutia na kubeba mimba. Sio kutafuta pesa.

Imagine mtoto wako analelewa na beki 3, wote mnatoka halafu eti unasema ni jukumu la Mwanamume kutoa eti wewe unalea, unalea kitu gani? Wewe umetoka nje kufanya nini? Fikiria hilo zaidi ya hapo utanielewa
 
Wewe kama unataka kujua baadhi ya wanawake ni tegemezi hata mwanzonwa mahusiano hela yake huli hata "jero la masimango" we mtoe out jifanye umesahau wallet 😂.

All in all mimi naona kama atajali kilichopo mbele yenu kwa maendeleo na familia kukua vizuri atachangia lakini huwa ni wachache sana. Wengine bampa to bampa anaweka hela mezani mnafanya maendeleo safi kabisa ila na sisi wanaume tuwe tunaeleweka at same time, maana ukimuona mkeo mtoaji tunatafuta wakuchukua hela zetu tunasahu familia, balaa linaanza hapo kuwatafuta wale "machachari" 🤣🤣
 
Sikubaliani na mtazamo wako. Ndoa haiwezi kutegemea tu kipato au elimu ya mke au mume. Ndoa inahitaji maelewano, upendo, na heshima kutoka pande zote mbili. Mwanamke mwenye elimu na kipato anaweza kuwa mke mwema kama ana maadili mazuri na anaheshimu ndoa yake. Tatizo haliko kwenye pesa au elimu, bali katika jinsi mtu anavyojijua na anavyohusiana na mwenza wake. Kila ndoa ina mfumo wake na inategemea pande zote mbili kuishi kwa usawa na kushirikiana.
Huwezi mwelewesha mwanamke aliye msomi au mwenye elimu huwezi,kama hajakuzwa kwenye maadili na wazazi na kujumjua Mungu. KINYUME CHA HAPO NDOA ITAVUNJIKA MDA WOWOTE. .

Sio unabishabisha UNAWAJUA PASSPORT BROS,ukitizama podcast utaelewa ninacho kiongea.

SINA CHA KUONGEZA endelea kubisha.
 
Back
Top Bottom