Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Ndio maana mfumo wa asili wa familia umeweka majukumu wazi—mwanaume ndiye mtoa huduma mkuu, na mwanamke ana hiari ya kusaidia kulingana na uwezo wake. Tatizo linakuja pale watu wanapolazimisha usawa wa majukumu ya kifedha lakini siyo usawa wa majukumu mengine ya kifamilia.
Mkuu,
Nikuulize, umekulia mjini au kijijini? Hivi unajua wazee wa zamani hawakuwa wanalima? Unajua mama na watoto ndio walienda shamba kulima na wazee walionekana msimu wa mavuno na mauzo tu?

Ukifuatilia huo mfumo unaousema utashangaa toka zamani wazee hawakuwa watafutaji, mama na watoto ndio walilima na kutafuta chakula.

Sema tu mmekariri kwamba Me ndio alikuwa anaprovide kimfumo ila sio kweli.

Ukija zama za kwetu, hatulimi tena, mashamba yapo kazini na biashara. Wote wakitoka lazima wote wachangie, japo kila familia ina kanuni zake hakuna kanuni maalumu coz kuna Me wanafanya kila kitu, hawataki wake zao wachangie chochote zaidi ya kwenda leba, while kuna kina sisi, lazima mke achangie maendeleo ya familia.
 
Kutoa si jukumu la asili. Haya majukumu yana maana, maana ya kutoa inatokana na physical advantages ambazo Mwanamume aliumbwa nazo zikawa favoured na mazingira, ila haikumaanisha kuwa Wanawake hawawezi. Ujio wa mashine na Maendeleo ya Teknolojia yamefanya zoezi la utafutaji na uzalishaji liwe rahisi kwa jinsia zote. So mantiki ya kutoa haipo kwa Mwanamume pekee tena kama ilivyo awali. Na kutoa kunatokana na kupata, nowadays wote tunapata. So, kutoa kwako sio hiari; usisingizie asili, kutoa ni social construct. Majukumu ya asili ni pamoja na kutia na kubeba mimba. Sio kutafuta pesa.

Imagine mtoto wako analelewa na beki 3, wote mnatoka halafu eti unasema ni jukumu la Mwanamume kutoa eti wewe unalea, unalea kitu gani? Wewe umetoka nje kufanya nini? Fikiria hilo zaidi ya hapo utanielewa
Huwa napinga sana huo mtazamo wa sisi tunachukuliwa kama watoaji wao wapokeaji tu, sawa kipato unaweza kuwa nacho kikubwa Mali nyingi haimaanishi mke akiwa na kazi asichangie kwenye maendeleo ya familia hata kama akiwa hana kazi awe karibu kwa kujitoa kuongeza kipato zaidi.
 
Wanawake na logic ni vitu viwili tofauti kabisa. Mtu anataka usawa lakini hataki wajibu unaikuja na huo usawa. Mimi ndio maana hata wadogo zangu naenda nao kwa logic, sio huu ujinga wa usawa wa kijinsia.

Kuna madogo wawili wanasoma chuo, mwaka mmoja na umri wao sawa, mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Ninapowatumia hela za matumizi yule wa kiume namtumia kiasi kikubwa zaidi, kwa sababu najua yule wa kike pesa ypte anaweza kuibana na kumbebesha mzigo boyfriend wake privilege ambayo yule wa kiume hana. Na yule wa kiume nae atabebeshwa bill na girlfriend wake cost ambayo yule kike hawezi kuingia. Kwa logic kama iyo hata siku moja siwezi kutumia kanuni ya usawa ninapowapa hela. Ni lazima dogo wa kiume nimpe kiasi kikubwa zaidi
Bro you have such a big brain which is filled with deep sophistication of life, your redpill understanding is top notch. Hongera sana.

Huu ufahamu ulionao unastahili kusambazwa kwa kile mwanaume mpenda haki na anayeijali jinsia yake ya kiume.

Ni jambo ambao liko wazi kati ya kijana wa kiume na kijana wakiwa kwenye hali ngumu ya kimaisha, yule wa kike ana nafasi kubwa sana ya kuwa bailed out kuliko wa kiume.

Mimi hata kwenye suala la ajira tu siku hizi fursa yoyote iliyopo ndani ya uwezo wangu huwa nampa kijana wa kiume, maana najua asipopata ajira leo, anaweza akaa mwaka mzima mitaani bila kupewa hata kibarua, na wakati huo hakuna hata mtu wa kumpa buku ya maji.. hii ni tofauti na kijana wa kike ambapo yeye anaweza akaishi bila kazi na asiwe na stress maana kuna masimps kibao yanayomuomba namba daily na yako tayari kumtumia hela za matumizi hata bila kuombwa....!!

mkuu unachofanya kwa hao madogo inatakiwa iwe ni jambo la kuigwa na kila mwanaume kwa maslahi ya kuleta usawa wa mnufaiko kiuchumi kwa jinsia zote mbili.
 
Ukifa au ukipotelea kwa mchepuko faida ya hiyo hela itaonekana
Hili jibu lako linatia hasira sana, na ungekuwa karibu ningekutemea makohozi usoni au kukuwasha vibao..!!

Kwamba umuhimu wa pesa zako ndani ya familia utaonekana siku mumeo atakapokufa? Utakuwa mchawi wewe mwanamke sio bure.
 
Huwa napinga sana huo mtazamo wa sisi tunachukuliwa kama watoaji wao wapokeaji tu, sawa kipato unaweza kuwa nacho kikubwa Mali nyingi haimaanishi mke akiwa na kazi asichangie kwenye maendeleo ya familia hata kama akiwa hana kazi awe karibu kwa kujitoa kuongeza kipato zaidi.
Mimi siungi mkono hiari kwa Mwanamke mfanya kazi, hizo ni mentality za Kimasikini
 
Ndio maana mfumo wa asili wa familia umeweka majukumu wazi—mwanaume ndiye mtoa huduma mkuu, na mwanamke ana hiari ya kusaidia kulingana na uwezo wake. Tatizo linakuja pale watu wanapolazimisha usawa wa majukumu ya kifedha lakini siyo usawa wa majukumu mengine ya kifamilia.
Mfumo upi wa asili??? Huu utaratibu sio wa asili kwa hapa Tanzania.

Tanzania huko nyuma ilikuwa ni nchi ya wakulima na wafugaji kwa zaidi ya 90%, kwakuwa hizo ndizo zilikuwa shughuli za kiuchumi mke na mume walishiriki kwa pamoja kujenga uchumi wa familia.

Kwa wakulima mke ndiye alikuwa mzalishaji mkuu wa chakula cha familia. Muda mwingine mazao ambayo mke ndiye aliweka mchango mkubwa yaliuzwa kupata mahitaji ya familia..

Upande wa wafugaji pia hali ilikuwa vivohivyo, mke alishiriki kuchunga mifugo, kukamua maziwa, kupeleka ng'ombe minadani n.k

Huu utaratibu wenu wa mwanaume kujenga uchumi wa familia pekeake ndiyo unasababisha familia nyingi ziendelee kuwa masikini, kwasababu hakuna uwiano wa watafutaji na watumiaji.
 
Tupo kwenye ulimwengu ambao tuna fursa sawa za elimu, biashara, uongozi n.k. Kwa nyakati hizi mwanamke mwenye kipato sio hiari tena kushiriki kujenga uchumi wa familia yake.

Nimeshuhudia huu ujinga mtaani kwangu, mume uchumi umeyumba ikabidi watoto warudi shule za kayumba kutoka shule binafsi walikokuwa wanasoma tokea wakiwa wadogo, ili kukabiliana na ukata.

Mke anafanya biashara ya nafaka na kukopesha ela za riba, anakipato ambacho kama wangeunganisha nguvu wale watoto wasingerudi kayumba. Inasemekana mama alinukuliwa kwenye vyama vya kinamama akisema hawezi kusomesha watoto hilo sio jukumu lake.
 
Hivi, kama hataki kusaidia kutunza familia, kazi yake nini? Ni kama vile wanaume wapo kuwahangaikia wao, huku hawana hata chochote cha kutoa! Wasingekuwa na kashimo kale, wangelingia nini!?
 
Sasa mtoke wote asubuhi muende kazini na mrudi wote jioni huku kazi za nyumbani pamoja na kuangalia watoto zinafanywa na dada wa kazi. Wewe mwanamke unakua na mchango gani kwenye iyo ndoa? Kipato chako unapeleka wapi?
Ukisema bora dada wa kazi, wataleta maneno
 
KAMA ANAFANYA SHUGHULI YA KUINGIZA KIPATO KUCHANGIA NI LAZIMA. WANASHERIA AU MAWAKILI WAJE WATUAMBIE SHERIA YA NDOA INASEMAJE KWENYE HILI.
 
Ukifa au ukipotelea kwa mchepuko faida ya hiyo hela itaonekana

Kwa nini muweke guarantee kuwa kufa lazima aanze mwanaume!! Then umechagua mtu jiamini! Habari za michepuko hazikuhusu!!

Swali ni lile lile tu linahitaji jibu!! Una faida gani na kwenye familia....!?
 
Back
Top Bottom