Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Kama unajijua hutakiwi kula kwa jasho mbona usikae nyumbani ukalea watoto alafu mmeo akatafuta pesa za kujenga familia?
Si mnasema hamtaki mama wa nyumbani? Na mke akiomba kila kitu unaanza kulalamika, acha auze hata mandazi.
 
Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mchango wa mwanamke kifedha ndani ya ndoa. Wengine wanasema ni lazima awe na mchango ili ndoa iwe na usawa, wengine wanaamini kuwa majukumu ya kifedha ni jukumu la mwanaume, huku mwanamke akihusika zaidi na malezi na uangalizi wa familia.

Mimi binafsi naamini kuwa kila mtu ana majukumu yake ndani ya ndoa, na kusaidiana kifedha ni suala la hiari, si wajibu wa lazima kwa mwanamke. Ikiwa mke anafanya kazi na anataka kuchangia, ni sawa, lakini haipaswi kuwa sharti ili kuthibitisha thamani yake kwenye ndoa.

Nimekutana na watu wanaoamini kuwa mwanamke asiyesaidia kifedha ndani ya ndoa ni mzigo kwa mwanaume. Pia, wengine wanasema mwanaume asiyemudu majukumu ya kifamilia pekee hatakiwi kuoa.

Je, mna maoni gani kuhusu hili? Ni wajibu wa mwanamke kuchangia kifedha kwenye ndoa, au ni suala la hiari kulingana na uwezo wake?

Karibuni kwenye mjadala!
Kama mke ana uwezo wa fedha, kama vile kufanya biashara au kufanya kazi ya kuajiriwa, ni vizuri akishirikiana na mme wake katika maendeleo na matumizi ya nyumbani.
Swali:

Mwanamke anayefanya kazi na kupunguza mda wa kulea watoto na mume wako:

1. Anapeleka wapi fedha anazopata?
2. Kazi inawafaidisha nini watu wake?

Ukijibu hayo maswali utakuwa umejibu swali lako
Swali:

Mwanamke anayefanya kazi na kupunguza mda wa kulea watoto na mume wako:

1. Anapeleka wapi fedha anazopata?
2. Kazi inawafaidisha nini watu wake?

Ukijibu hayo maswali utakuwa umejibu swali lako
Inategemea na kipato Cha mume wake.
Waishi ndani ya uwezo wao
Hakika,
Changamoto inakuja mwanamke anapokuwa na kipato kikubwa kuliko mume wake.. huo uwezo wao utabalance vipi wakati mwanaume ndio inatakiwa uwe na mchango mkubwa kuzidi mwanamke
Kama mwanamke lazima achangie kifedha ili ndoa ifanye kazi, basi mume naye lazima ashiriki sawa kwenye majukumu ya nyumbani na malezi. Ndoa siyo biashara ya kugawana gharama, ni kushirikiana katika maisha kwa kila hali.
Sahihi kabisa, mimi binafsi siwezi kukaa na amani ninapo chukua au kupewa hela na mwanamke.
Ninakubaliana kabisa na wewe. Hasa katika ndoa, ni muhimu kwa mke na mume kushirikiana na kusaidiana katika kupanga matumizi ya fedha na kutunza familia. Mke anaweza kutoa msaada mkubwa kwa mume kwa kumsaidia kupanga matumizi, kuhakikisha fedha zinatumika vizuri, na kuleta usawa ndani ya nyumba. Ushirikiano huu unasaidia kudumisha amani na mafanikio ya kifamilia.
Haya ndio mambo ya kuangalia kabla ya kuoa, mwanamme asije akaona anadharauliwa sababu mwanamke hana muda kupika yupo anatafuta shilingi
Kama mwanamke anafanya kazi au biashara inayo muingizia kipato ni nirazima kipato chake kichangie maendeleo ya familia tofauti na hapo hiyo kazi na biashara hatoifanya na atakaa nyumbani kulea watoto kama hataki aondoke akaolewe na mwingine.

Mwanamke nikisha muoa ni lazima aende kwenye ndoto zangu sio aje kuwa mshindani wa ndoto zangu.

Alafu ww mwanamke kipato chako ambacho akichangii maendeleo ya familia kwa ajili future ya watoto wenu unakuwa unatafuta kipato cha nini hasa?
Nimeona wanaume wengi sana wakifika mbali zaidi kwa kusikiliza wake zao kuliko marafiki. Tatizo waume wengi masikio yao yapo kama mapambo
Kila siku mada zile zile uwa vikaoni hamuendi😹😹
Wanawake wengi wanaofanya kazi mara nyingi ni kwaajili ya uhuru wa kipato na kuwekeza kwaajili ya kipindi cha kiangazi. (Mume kufariki, kuugua, kukimbilia michepuko) kwaajili yake, wanaomtegemea na watoto wake
Mimi mwanamke wangu ata simama Kama mlezi wa familia, ka ni biashara ata simamia za familia pia.
Vipi kazi za nyumbani naye mwanaume atafanya kama mkewe anavyofanya?
Sio mnarudi wote jioni mke anaanza majukumu y nyumbani mwanaume anashika remote yeye na TV, mke achangie kwa hiari sio lazima.
Ndiyo maana wanashauriwa oa umayemudu , sio oversize
Eti kipindi cha kiangazi 😅😅😅
Maswala ya nani Kati ya mwanamke na mwanaume anapaswa kuchangia pesa katika familia hayana mpangilio maalumu, hayana kanuni na hayapaswi kabisa kuwekewa kanuni au Sheria kama mnavyotaka.

Binafsi huwa ninakerwa Sana na kauli inayosema "mke akiwa na milioni moja halafu mume ana laki tano familia ina laki tano kwa sababu mwanamke pesa zake anajua atazituamia vipi". Hii kauli ni ya kipuuzi mno, kwangu mimi pesa za mume ni za familia na pesa za mke pia ni za familia.

Nasema hivi kwa sababu siko tayari kuhudumia kiumbe ambacho hakina mchongo wowote zaidi ya kupiga domo. Hata ninyi mnaojaribu kujadiliana kujua nani anapaswa kuchangia acheni mara moja tabia hii, Kila mtu adili na mkewe/mumewe. Kama mtu hataki mke wake asichangie asipotoshe watu wengine humu.

Mke wangu atachangia Sana katika familia labda afiche pesa zake nisizione. Siko tayari kufanya mambo kwa presha ya jamii.

Eti "hamna hela ya mboga" halafu ana hela, NYAMBAFU!!
Al-mukheef Monetary doctor
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili ke na me kwa ajili ya kuweka pamoja changamoto zao ili waweze kupambana pamoja na hatimaye kufanikiwa. Ndiyo maana sie wa kitambo ulikuwa ukipata kazi tu unaambiwa oa ili upate mtu wa kushirikiana nae kuleta familia na maendeleo yenu kiujumla.

Sasa, Mama zetu waliokuwa wake wa nyumbani (house wifes) walikuwa hawachangii fedha ila walikuwa wanasimamia majukumu yote yahusuyo familia ikiwamo ulezi, kusimamia kipato kinachopatikana na kushirikia kwa karibu katika maswala ya kijamii!! Hivyo, mume alikuwa anatafuta kwa bidii akijua familia na kipato changu vipo sehemu salama.

Turudi kwenu; unafanya kazi, nyumbani huonekani kuanzia kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu na wakati mwingine utasafiri kikazi wiki nzima. Familia inakuwa muda mwingi kama si wote mikononi mwa dada wa kazi (zamani tuliwaita yaya).

Nyumbani huna contribution yoyote na kipato chako hakionekani hakihusiki na familia hii kwa madai wewe ni mke huna cha kuchangia! Ok, Watoto pia wanalelewa na dada wa kazi!! Nini contributions zako katika hii familia ambayo unasema ni yako kama mama, kama mke??

Tuanzie hapa kwanza!! Nikishajua hili ndiyo twaweza kuendelea
Uhodari mwingi sana kwneye kuelezea hali ilivyokuwa hapo zamani. Ni kwa vile bibi na mama zetu walivumilia sana kunyanyaswa kiuchumi, kila kitu ngoja baba aje. Haufafahamu hili sababu walikuwa hawalalamiki wala kuonesha kwa watoto wao. Lakini walihakikisha binti zao hawapitii waliopitia wao, zaidi wanapofiwa au kutelekezwa na mwanamme, au kipindi mwanamme anafuja mali kwenye jambo lisilo na manufaa kwa familia/watoto. Wamama hawa walibebea 'resentment' juu ya baba zenu, matokeo yake ikawa watoto wanapokuwa wakubwa, masaada mkubwa zaidi anapewa mama au tuseme anakumbukwa zaidi (si tunajionea wenyewe kwenye jamii zetu?) japo baba yupo hai na ndio aliyevuja jasho na damu kuwalea.

Pesa anayopata unaitolea macho ya nini? Kuhudumia familia kifedha narudia ni jukumu la mwanamme. Ukosefu wa wababa wengi wanaoelewa majukumu yao limekuwa jambo la kawaida kwenye jamii ya sasa. matokeo yake tunapata vijana ambao hawaoni umuhimu wa kuhudumia familia zao sababu hawana mfano unaoeleweka wa kiume. Wanaona mama zao walipambana na hivyo wake zao wapambane, hapana kubwa sana
 
Mimi mwanamke wangu ata simama Kama mlezi wa familia, ka ni biashara ata simamia za familia pia.
Kusimamia familia na biashara ni mchango mkubwa, lakini bado naamini kuwa kuchangia kifedha ni jambo la hiari kwa mwanamke, si jukumu lake la lazima. Ikiwa ataamua kusaidia, ni vizuri, lakini haipaswi kuwa sharti la ndoa.
 
Ndio maana nasema kuoa hawa wanawake wanaoitwa working class ladies ni hasara kubwa sana... mama wa nyumbani ana afadhari kubwa kuliko hawa.

Imagine unaoa mwanamke ambaye hana muda na familia yeye kila kukicha anaenda kazin anakimbizana na malengo yake binafsi, pesa anayoipata huko kazini haionekani ndani bali inaenda kwenye matumizi yake binafsi... majukumu yote ya nyumbani kamwachia beki tatu ambaye wewe ndio unamlipa mshaara.

Haya siku imetokea amaichoka ndoa anaenda mahakamani kufungua talaka halafu mahakamani inaamuru mgawane mali 50/50.. mali ambazo kwa asilimia kubwa pesa zako wewe mwanaume ndio zilitumika kununua, wakati huo mwanamke yeye pesa yake ilikuwa inatumika kusomeshea ndugu zake... Sasa kwanza si dhuluma kabisa hii jamani?

Sasa ni bora mtu umeoa mama wa nyumbani ambaye anawajibika kwenye majukumu yote ya ulezi wa familia huku akikupa na wewe faraja kwa heka heka unazopitia huko makazini?

Mwanamke goli kipa hata siku ikitokea mmeachana mnagawana mali 50/50 kiroho safi kabisa, kwa sababu wakati wewe huko bize kutafuta pesa yeye alikuwa bize kulea watoto wako au kwa namna nyingine aliutumia muda wake ambao na yeye angeutumia kutafuta mali zake kukulelea familia yako na hivyo basi ni sahihi kabisa yeye kupata hiyo 50% kama compesation.....

...hali hii ni tofauti kabisa na wale working class ladies, hao huwa ni wezi, yaani mtu mnatoka wote hasubui kwenda kazini, hela zake anatumia kuboresha maisha ya nyumbani kwao huko, huku ndani ya familia yake haitumiku hata buku ila eti siku mkiachana anataka mgawane pasu kwa pasu...!! Eboo huo utapeli nilishajiandaa kuukwepa mimi kitambo
Inaonekana una support wanawake golkipa, ila kwa maisha ya sasa ni wanaume wangapi Tanzania wana kipato cha kuweza ku-afford mwanamke golkipa, Yani baba, mama, watoto 3, wa-survive na kufanya maendeleo kwa kutumia single income ya baba Muhimbu
 
Maswala ya nani Kati ya mwanamke na mwanaume anapaswa kuchangia pesa katika familia hayana mpangilio maalumu, hayana kanuni na hayapaswi kabisa kuwekewa kanuni au Sheria kama mnavyotaka.

Binafsi huwa ninakerwa Sana na kauli inayosema "mke akiwa na milioni moja halafu mume ana laki tano familia ina laki tano kwa sababu mwanamke pesa zake anajua atazituamia vipi". Hii kauli ni ya kipuuzi mno, kwangu mimi pesa za mume ni za familia na pesa za mke pia ni za familia.

Nasema hivi kwa sababu siko tayari kuhudumia kiumbe ambacho hakina mchongo wowote zaidi ya kupiga domo. Hata ninyi mnaojaribu kujadiliana kujua nani anapaswa kuchangia acheni mara moja tabia hii, Kila mtu adili na mkewe/mumewe. Kama mtu hataki mke wake asichangie asipotoshe watu wengine humu.

Mke wangu atachangia Sana katika familia labda afiche pesa zake nisizione. Siko tayari kufanya mambo kwa presha ya jamii.

Eti "hamna hela ya mboga" halafu ana hela, NYAMBAFU!!
Al-mukheef Monetary doctor
Inaeleweka kuwa kila mtu ana mtazamo wake kuhusu suala hili. Muhimu ni makubaliano kati ya wanandoa. Kama unadhani mke wako atachangia sana, hilo ni sawa kwa ndoa yako. Lakini kuna wengine wanaoamini mwanamke asichangie au achangie kwa hiari, na hilo pia linaheshimika.
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili ke na me kwa ajili ya kuweka pamoja changamoto zao ili waweze kupambana pamoja na hatimaye kufanikiwa. Ndiyo maana sie wa kitambo ulikuwa ukipata kazi tu unaambiwa oa ili upate mtu wa kushirikiana nae kuleta familia na maendeleo yenu kiujumla.

Sasa, Mama zetu waliokuwa wake wa nyumbani (house wifes) walikuwa hawachangii fedha ila walikuwa wanasimamia majukumu yote yahusuyo familia ikiwamo ulezi, kusimamia kipato kinachopatikana na kushirikia kwa karibu katika maswala ya kijamii!! Hivyo, mume alikuwa anatafuta kwa bidii akijua familia na kipato changu vipo sehemu salama.

Turudi kwenu; unafanya kazi, nyumbani huonekani kuanzia kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu na wakati mwingine utasafiri kikazi wiki nzima. Familia inakuwa muda mwingi kama si wote mikononi mwa dada wa kazi (zamani tuliwaita yaya).

Nyumbani huna contribution yoyote na kipato chako hakionekani hakihusiki na familia hii kwa madai wewe ni mke huna cha kuchangia! Ok, Watoto pia wanalelewa na dada wa kazi!! Nini contributions zako katika hii familia ambayo unasema ni yako kama mama, kama mke??

Tuanzie hapa kwanza!! Nikishajua hili ndiyo twaweza kuendelea
Na pia, yaya yupo kumsaidia huyo mama na kazi za nyumbani. Hata zamani mama/bibi zetu walisaidiwa na ndugu zao wa kike au wifi zao hapo nyumbani kwa vitu vidogo vidogo siku hizi umbali unafanya watu wawe na wadada wa kazi. Hamna ubaya wa kupata msaada unapohitajika. Kipaumbele ni kuhudumia mumeo bila uchovu wa siku nzima kukuelemea.

Isitoshe dada wa kazi sio replacement ya kazi ya kuwa mzazi. Hajaingia leba, nyonyesha watoto wako wala kuwaapa uangalizi makini kama wa mama. Kufua na kudeki isilinganishwe na kulea kwa maana ya kulea
 
mwanamke kama anaamka asubuhi na Kwenda Kibaruani either kajiajiali au Kaajiliwa ni Muhimu sana Kuchangia maendeleo ya Familia kama Anataka Kutunzwa kwa kila Kitu basi akae tu ndani alee watoto na Mumewe apambane
 
Hii mada huwa ni ya kutafuta justification ya mwanamke kutochangia kipato kwa mumewe.

Kwa jamii yetu sisi huwa mwanamke anapoolewa anaenda kuwa sehemu ya familia hivyo anawajibika katika shughuli za uzalishaji na uchumi kwenye familia aliyoolewa. Ilikuwa hivyo toka zama za bibi, babu alikuwa karani wa serikalini na alikuwa anajishughulisha na kilimo hivyo alimiliki bunduki pia. Kuna wakati alikuwa anaenda winda na kuleta kitoweo. Walikuwa wakulima pia wanalima kahawa na ndizi hivyo bibi alikuwa anaenda sokoni kuuza kipindi cha mavuno na kurudi na fedha na kipato kilitumika ku support familia.

Hivyo ukiniuliza ni sahihi ntasema kweli ni sahihi.
Kila familia ina mfumo wake. Kama ilivyo kwa babu na bibi zako, walishirikiana kulingana na mazingira yao. Lakini si lazima kila ndoa ifuate mfumo huo. Kila wanandoa wanaamua kinachofanya kazi kwao.
 
Uhodari mwingi sana kwneye kuelezea hali ilivyokuwa hapo zamani. Ni kwa vile bibi na mama zetu walivumilia sana kunyanyaswa kiuchumi, kila kitu ngoja baba aje. Haufafahamu hili sababu walikuwa hawalalamiki wala kuonesha kwa watoto wao. Lakini walihakikisha binti zao hawapitii waliopitia wao, zaidi wanapofiwa au kutelekezwa na mwanamme, au kipindi mwanamme anafuja mali kwenye jambo lisilo na manufaa kwa familia/watoto. Wamama hawa walibebea 'resentment' juu ya baba zenu, matokeo yake ikawa watoto wanapokuwa wakubwa, masaada mkubwa zaidi anapewa mama au tuseme anakumbukwa zaidi (si tunajionea wenyewe kwenye jamii zetu?) japo baba yupo hai na ndio aliyevuja jasho na damu kuwalea.

Pesa anayopata unaitolea macho ya nini? Kuhudumia familia kifedha narudia ni jukumu la mwanamme. Ukosefu wa wababa wengi wanaoelewa majukumu yao limekuwa jambo la kawaida kwenye jamii ya sasa. matokeo yake tunapata vijana ambao hawaoni umuhimu wa kuhudumia familia zao sababu hawana mfano unaoeleweka wa kiume. Wanaona mama zao walipambana na hivyo wake zao wapambane, hapana kubwa sana
Kama unajiona sio jukumu lako kuhudumia familia kaa nyumbani ulee watoto uhudumiwe kila kitu.
Ukijitia kwenda kutafuta hela hizo hela zitakuwa chini ya familia.
 
Kutoa ni moyo usambe si utajiri.

1742117379592.png
 
Si mnasema hamtaki mama wa nyumbani? Na mke akiomba kila kitu unaanza kulalamika, acha auze hata mandazi.
Hatutaki goli kipa ili na mwana mke achangie kwenye maendeleo ya familia na sio kwenda kutafuta hela ili aende kufanya mambo yake ya kibinafisi.
 
Kusimamia familia na biashara ni mchango mkubwa, lakini bado naamini kuwa kuchangia kifedha ni jambo la hiari kwa mwanamke, si jukumu lake la lazima. Ikiwa ataamua kusaidia, ni vizuri, lakini haipaswi kuwa sharti la ndoa.
Hizo pesa zisizo hudumia familia zinaenda wapi na zinafanya kazi gani?
 
Ndio maana ndoa za siku hizi zimejaa migogoro kwa sababu watu wanaoana huku kila mmoja ana ndoto zake badala ya kujenga ndoto moja.
Mwanamke kama anaingiza kipato ni lazima kitumike kwenye maendeleo ya familia na sio mambo yake binafsi.

Ya kwamba ni sahihi mke wangu awe anatumia mshahara wake kuwalipia ada watoto wa dada yake ila mm nikimuambia tuchangie ada kwa ajili ya watoto wetu akatae na kusema eti ni jukumu langu tu?
Yaani watoto aliyo wazaa hana jukumu la kuwalipia ada ila anajukumu la kuwalipia ada watoto wa dada yake na si jukumu la dada yake na aliye mzalisha hao watoto?

Mmeoana kwa ajili ya kwenda kujenga familia moja sasa iweje kila mtu afanye mambo yake kibinafsi nini maana ya familia moja?
Ikiwa mwanamke ana jukumu la kuchangia kifedha kwa lazima, basi tunapaswa pia kuzungumzia usawa katika majukumu mengine ya familia. Je, mume naye anapaswa kushiriki kwa usawa kwenye kazi za nyumbani na malezi ya watoto?
 
Kama unajiona sio jukumu lako kuhudumia familia kaa nyumbani ulee watoto uhudumiwe kila kitu.
Ukijitia kwenda kutafuta hela hizo hela zitakuwa chini ya familia.
Tuliza jazba ndugu mdau, pingana kwa hoja. Hayo maneno ya kumuambia mkeo muelewane hivyo. Sio kila kiatu ni saizi yako
 
Inaeleweka kuwa kila mtu ana mtazamo wake kuhusu suala hili. Muhimu ni makubaliano kati ya wanandoa. Kama unadhani mke wako atachangia sana, hilo ni sawa kwa ndoa yako. Lakini kuna wengine wanaoamini mwanamke asichangie au achangie kwa hiari, na hilo pia linaheshimika.
Yeah, ndoto maana sitaki watu wapotoshane, wanandoa wataamua wenyewe bila kusukumwa na kitu chochote. Kumbuka nyinyi kama wanandoa mkikwama hakuna atakaye kuja kuwasaidia.

Mke wangu atachangia Sana!!!
 
Swali linabaki—je, mwanamke akichangia, inamaanisha mume naye anaweza kutarajia kusaidiwa kwenye majukumu mengine ya nyumbani kama kulea watoto na kazi za ndani?
Mtu unaamka saa 12:00 unarudi saa 3 za usiku hayo malezi ya watoto na hizo kazi za ndani unazifanya saa ngapi?
 
Back
Top Bottom