Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mchango wa mwanamke kifedha ndani ya ndoa. Wengine wanasema ni lazima awe na mchango ili ndoa iwe na usawa, wengine wanaamini kuwa majukumu ya kifedha ni jukumu la mwanaume, huku mwanamke akihusika zaidi na malezi na uangalizi wa familia.

Mimi binafsi naamini kuwa kila mtu ana majukumu yake ndani ya ndoa, na kusaidiana kifedha ni suala la hiari, si wajibu wa lazima kwa mwanamke. Ikiwa mke anafanya kazi na anataka kuchangia, ni sawa, lakini haipaswi kuwa sharti ili kuthibitisha thamani yake kwenye ndoa.

Nimekutana na watu wanaoamini kuwa mwanamke asiyesaidia kifedha ndani ya ndoa ni mzigo kwa mwanaume. Pia, wengine wanasema mwanaume asiyemudu majukumu ya kifamilia pekee hatakiwi kuoa.

Je, mna maoni gani kuhusu hili? Ni wajibu wa mwanamke kuchangia kifedha kwenye ndoa, au ni suala la hiari kulingana na uwezo wake?

Karibuni kwenye mjadala!
Waasisi tu wenyewe wa sheria ya 50/50 wanashare cost bila kujali jinsia zao. Shida inaanzia huku umatumbini😂
 
Nimeona wanaume wengi sana wakifika mbali zaidi kwa kusikiliza wake zao kuliko marafiki. Tatizo waume wengi masikio yao yapo kama mapambo
Sasa utamsikiliza rafiki ambaye yeye mwenyewe kwake yamemshinda atakushauri nini zaidi atakwambia aaa mie huwa namsaidia mama chanja kukuna Nazi huku anakitumbo na ndevu uso mzima😂😂😂, hapo bora umsikilize mkeo
 
Yaani unaweza kujikuta unaachwa kwenye jangwa, jua kali
Kuna mkaka alifariki jamani walikuwa na mtoto mmoja , hivi unajua mkewe hakupewa kitu mpaka pesa ya mizigo alikula baba wa kijana pole zote za msiba Mzee anakusanya, miradhi wakajazana mtoto kaishia kupata milioni 2 mtoto ndiyo kaanza darasa la kwanza, yaani kuna watu wanaroho zakichawi kumzidi hata shetani.
 
Swali:

Mwanamke anayefanya kazi na kupunguza mda wa kulea watoto na mume wako:

1. Anapeleka wapi fedha anazopata?
2. Kazi inawafaidisha nini watu wake?

Ukijibu hayo maswali utakuwa umejibu swali lako
Hii mada huwa ni ya kutafuta justification ya mwanamke kutochangia kipato kwa mumewe.

Kwa jamii yetu sisi huwa mwanamke anapoolewa anaenda kuwa sehemu ya familia hivyo anawajibika katika shughuli za uzalishaji na uchumi kwenye familia aliyoolewa. Ilikuwa hivyo toka zama za bibi, babu alikuwa karani wa serikalini na alikuwa anajishughulisha na kilimo hivyo alimiliki bunduki pia. Kuna wakati alikuwa anaenda winda na kuleta kitoweo. Walikuwa wakulima pia wanalima kahawa na ndizi hivyo bibi alikuwa anaenda sokoni kuuza kipindi cha mavuno na kurudi na fedha na kipato kilitumika ku support familia.

Hivyo ukiniuliza ni sahihi ntasema kweli ni sahihi.
 
Wanawake wengi wanaofanya kazi mara nyingi ni kwaajili ya uhuru wa kipato na kuwekeza kwaajili ya kipindi cha kiangazi. (Mume kufariki, kuugua, kukimbilia michepuko) kwaajili yake, wanaomtegemea na watoto wake
Ndio maana ndoa za siku hizi zimejaa migogoro kwa sababu watu wanaoana huku kila mmoja ana ndoto zake badala ya kujenga ndoto moja.
Mwanamke kama anaingiza kipato ni lazima kitumike kwenye maendeleo ya familia na sio mambo yake binafsi.

Ya kwamba ni sahihi mke wangu awe anatumia mshahara wake kuwalipia ada watoto wa dada yake ila mm nikimuambia tuchangie ada kwa ajili ya watoto wetu akatae na kusema eti ni jukumu langu tu?
Yaani watoto aliyo wazaa hana jukumu la kuwalipia ada ila anajukumu la kuwalipia ada watoto wa dada yake na si jukumu la dada yake na aliye mzalisha hao watoto?

Mmeoana kwa ajili ya kwenda kujenga familia moja sasa iweje kila mtu afanye mambo yake kibinafsi nini maana ya familia moja?
 
Vipi kazi za nyumbani naye mwanaume atafanya kama mkewe anavyofanya?
Sio mnarudi wote jioni mke anaanza majukumu y nyumbani mwanaume anashika remote yeye na TV, mke achangie kwa hiari sio lazima.
Unashinda mihangaikoni hizo kazi utazifanya saa ngapi,kwenye situation kama hiyo ni lazima muwe na dada wa kazi ambaye naye jukumu la kumlipa umemtwisha mwanaume.

Mwanamke kama umeamua kutafuta pesa ni lazima uchangie maendeleo ya familia tofauti na hapo kaa nyumbani lea watoto.
 
Ndio maana ndoa za siku hizi zimejaa migogoro kwa sababu watu wanaoana huku kila mmoja ana ndoto zake badala ya kujenga ndoto moja.
Mwanamke kama anaingiza kipato ni lazima kitumike kwenye maendeleo ya familia na sio mambo yake binafsi.

Ya kwamba ni sahihi mke wangu awe anatumia mshahara wake kuwalipia ada watoto wa dada yake ila mm nikimuambia tuchangie ada kwa ajili ya watoto wetu akatae na kusema eti ni jukumu langu tu?
Yaani watoto aliyo wazaa hana jukumu la kuwalipia ada ila anajukumu la kuwalipia ada watoto wa dada yake na si jukumu la dada yake na aliye mzalisha hao watoto?

Mmeoana kwa ajili ya kwenda kujenga familia moja sasa iweje kila mtu afanye mambo yake kibinafsi nini maana ya familia moja?
Kwani wewe watoto wa dada zako huwa lipii ada? Mara nyingi migogoro huanza pale mme yupo busy na ndugu zake tu kwao laki 2 Kwa mke eldu 20 tena Kwa mbinde, sasa unategemea yeye atoe %? Itakuwa vigumu sana, maisha ya ndoa mkae mpange hili liwe hivi hili likae vile, sasa mmoja alimwambia mkewe unaona wivu ninavyowapa pesa kwetu si ndugu zangu, wewe kaka yako ahudumie huko mama yako sijaoa ukoo Mimi, embu ona kauli kama hiyo mke afanye nini!
 
Back
Top Bottom