Ndege Tai
JF-Expert Member
- May 6, 2020
- 5,215
- 9,719
Upo sahihi jina lako linasadifu uliyoandika.Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Upo sahihi jina lako linasadifu uliyoandika.Sio wajibu wa mwanamke kuhudumia familia kifedha. Mke anamsaidia mume wake namna ya kupangilia na kutumia fedha zake kuhudumia hapo nyumbani
Kwa mfano kama mke wangu hana kipato au pesa mimi sina shida naye at all ila kitu ambacho sitakikubali ni mwanamke kuwa na kipato halafu hataki kuitumia katika familia.Sidhani kama pesa za mke zinapaswa kuwa tu kwa ajili ya matumizi ya kifamilia. Kuna nafasi ya ushirikiano, na maelewano mapema ni muhimu. Ni muhimu kujua kwamba kila mtu katika ndoa ana majukumu yake, na si lazima michango yote iwe ya kifedha. Ikiwa mmoja ni mama wa nyumbani, bado ana mchango mkubwa katika familia.
Na ww ni muumini wa fifty fifty?50/50 ni kuhusu ushirikiano na msaada. Huwezi kupima mchango wa ndoa kwa kiwango cha kifedha tu. Usawa wa ndoa unahusisha kujitolea, kuelewana na kusaidiana kwa njia nyingi, na siyo tu kwa michango ya pesa.
Muda wa mke ni muhimu, lakini siyo lazima awekwe kwenye majukumu ya nyumbani pekee. Mama ni sehemu ya familia, na mchango wake unaweza kuwa kwenye kazi au biashara pia. Ikiwa mke anafanya kazi kwa faida ya familia, si vibaya, bali ni njia ya kusaidia familia kwa namna nyingine. Kuweka dada wa kazi siyo kwa ajili ya kupunguza mzigo wa mama, bali ni kuhakikisha kila mmoja anachangia kwa manufaa ya familia. Kazi ya mke ni muhimu, kama vile ya mume, na sio lazima kila kipato chake kionekane mara moja. Kila mmoja katika familia ana mchango wake.Muda wa mke ni muda wa familia huwezi kuutumia kwa mambo yako binafsi, kwamba tumeweka dada wa kazi na kumlipa mshahara akusaidie majukumu yako ya nyumbani ukiwa kwenye majukumu ya biashara au kazi kuingiza kipato.
Kuweka dada wa kazi kulea watoto ni risk kubwa sana familia imefanya maana sio mama yao anafanya majukumu ya mama na hatujui kwa hakika kama analea watoto vyema.
Halafu huyo mama apate fedha isionekane kwenye familia huo ni wizi na utapeli wa kutumia muda wa familia vibaya.
Kama mume anaruhusu hilo lazima ni mume mwenye mapungufu na hammudu mkewe mke anammudu mume.
Yaani uache watoto na majukumu yako ya nyumbani ukafanye biashara au kazi huko maofisini na hela isionekane maana yake hiyo kazi haina umuhimu wowote kwa familia inabidi iwekwe kando maana familia itaamini unafanya kazi na haulipwi unadhulumiwa na kama unalipwa unaidhulumu familia.
Yaani mwanamke uwe na pesa halafu utumie peke yako lakini pesa zangu tutumie wote?Sio wajibu wake ila ni kwa hiari. Lakini inapendeza akifanya hivyo kama anao huo uwezo.
**Rahisi sana hii:-Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mchango wa mwanamke kifedha ndani ya ndoa. Wengine wanasema ni lazima awe na mchango ili ndoa iwe na usawa, wengine wanaamini kuwa majukumu ya kifedha ni jukumu la mwanaume, huku mwanamke akihusika zaidi na malezi na uangalizi wa familia.
Mimi binafsi naamini kuwa kila mtu ana majukumu yake ndani ya ndoa, na kusaidiana kifedha ni suala la hiari, si wajibu wa lazima kwa mwanamke. Ikiwa mke anafanya kazi na anataka kuchangia, ni sawa, lakini haipaswi kuwa sharti ili kuthibitisha thamani yake kwenye ndoa.
Nimekutana na watu wanaoamini kuwa mwanamke asiyesaidia kifedha ndani ya ndoa ni mzigo kwa mwanaume. Pia, wengine wanasema mwanaume asiyemudu majukumu ya kifamilia pekee hatakiwi kuoa.
Je, mna maoni gani kuhusu hili? Ni wajibu wa mwanamke kuchangia kifedha kwenye ndoa, au ni suala la hiari kulingana na uwezo wake?
Karibuni kwenye mjadala!
Mkishafunga ndoa wote mnatumia muda wa familia kwaiyo ni lazima kila mmoja autumie huo muda kwa mambo ambayo yanaleta input kwenye familia. Mwanamke kwenda kutafuta halafu anachopata kisiwe na mchango wowote kwenye familia hayo ni matumizi mabaya ya muda wa familia.Sidhani kama pesa za mke zinapaswa kuwa tu kwa ajili ya matumizi ya kifamilia. Kuna nafasi ya ushirikiano, na maelewano mapema ni muhimu. Ni muhimu kujua kwamba kila mtu katika ndoa ana majukumu yake, na si lazima michango yote iwe ya kifedha. Ikiwa mmoja ni mama wa nyumbani, bado ana mchango mkubwa katika familia.
Hicho ndo tunacho maanisha ni lazima kila kitakacho kuwa kinafanywa na mwana ndoa basi kiwe ni kwa ajili ya manufaa ya familia kwa ujumla na si kwa faida za kibinafisi.Muda wa mke ni muhimu, lakini siyo lazima awekwe kwenye majukumu ya nyumbani pekee. Mama ni sehemu ya familia, na mchango wake unaweza kuwa kwenye kazi au biashara pia. Ikiwa mke anafanya kazi kwa faida ya familia, si vibaya, bali ni njia ya kusaidia familia kwa namna nyingine. Kuweka dada wa kazi siyo kwa ajili ya kupunguza mzigo wa mama, bali ni kuhakikisha kila mmoja anachangia kwa manufaa ya familia. Kazi ya mke ni muhimu, kama vile ya mume, na sio lazima kila kipato chake kionekane mara moja. Kila mmoja katika familia ana mchango wake.
Hiyo ni wewe na mke wako hatuwezi kukuingilia. Wengine tupo na wanaume ambao wanawajibika kwa kila kitu bila manung"uniko na tunasaidia pale inabobidi na hata tusipo saidia maisha yanasonga maana atatekeleza ni wajibu wake. Kama hataki aende huko na yeye akaolewe..Yaani mwanamke uwe na pesa halafu utumie peke yako lakini pesa zangu tutumie wote?
Hiyo wafanyie wanaume malofa na mabushoke lakini siyo mimi, kwenye ndoa pesa zangu ni zako na zangu ni zako.
Asubuhi njema.
Nahudumia pale ninapotaka na sio lazima kama mume yupo na anao uwezo wa kucover kila kitu.Ya kwamba kuhudumia watoto wako ulio wazaa sio wajubu wako ?
Maswala ya nani Kati ya mwanamke na mwanaume anapaswa kuchangia pesa katika familia hayana mpangilio maalumu, hayana kanuni na hayapaswi kabisa kuwekewa kanuni au Sheria kama mnavyotaka.
Binafsi huwa ninakerwa Sana na kauli inayosema "mke akiwa na milioni moja halafu mume ana laki tano familia ina laki tano kwa sababu mwanamke pesa zake anajua atazituamia vipi". Hii kauli ni ya kipuuzi mno, kwangu mimi pesa za mume ni za familia na pesa za mke pia ni za familia.
Nasema hivi kwa sababu siko tayari kuhudumia kiumbe ambacho hakina mchongo wowote zaidi ya kupiga domo. Hata ninyi mnaojaribu kujadiliana kujua nani anapaswa kuchangia acheni mara moja tabia hii, Kila mtu adili na mkewe/mumewe. Kama mtu hataki mke wake asichangie asipotoshe watu wengine humu.
Mke wangu atachangia Sana katika familia labda afiche pesa zake nisizione. Siko tayari kufanya mambo kwa presha ya jamii.
Eti "hamna hela ya mboga" halafu ana hela, NYAMBAFU!!
Al-mukheef Monetary doctor
Ni wajibu w mume. Kwani lini ilibadilika?Siyo wajibu wake kivipi.
Hahahaha 🤣 kama mmekubaliana ni sawa, pesa zenu mkazitumie kuhonga vijana wenye miguvu ya kiume.Hiyo ni wewe na mke wako hatuwezi kukuingilia. Wengine tupo na wanaume ambao wanawajibika kwa kila kitu bila manung"uniko na tunasaidia pale inabobidi na hata tusipo saidia maisha yanasonga maana atatekeleza ni wajibu wake. Kama hataki aende huko na yeye akaolewe..
Ndoa nimeshaishinda, huwa sifanyi mambo kwa kujilinganisha na wengine.Ndoa itakushinda
Unatoka saa 12 asubuhi unarudi saa 2 usiku utalea watoto saa ngapi, utatunza mume saa ngapi? embu acha blah blah zakoMchango wa mwanamke haukamiliki kwa pesa pekee. Kuna majukumu mengine muhimu, kama kulea watoto, kumtunza mume, na kuleta usawa na amani katika familia. Ingawa mke anafanya kazi, mchango wake katika familia haupimwi tu kwa pesa. Hata na dada wa kazi, bado kuna kazi za kipekee ambazo mwanamke anazifanya
Siyo Sheria ni makubaliano.Ni wajibu w mume. Kwani lini ilibadilika?
Sio hiari ni wajibu. Kitendo cha kuwa na kipato maana yake unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi, na utawajibika kulipia au kuchangia gharama zote za wewe kuishi.Sio wajibu wake ila ni kwa hiari. Lakini inapendeza akifanya hivyo kama anao huo uwezo.
Kama anajielewa ni afadhali siyo dude Lina hela alafu siku wewe kukosea hela mnalala na njaa.Mwaka wa tatu huu sijawahi kuuliza mshahara wake anafanyia nini Ila yuko smart sometimes unakuta kanunua kitu flani for the sake of the family...!! Pia anasave sana hata ikitokea nimetingwa huwa anasupport but NEVER ASK WOMAN TO CARE FOR THE FAMILY.. mambo ya kodi sijui ada hela ya chakula nyumbani bills zote Mwanaume pambana unaepusha ugomvi usiokuwa na lazima.