Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Kama mke ana uwezo wa fedha, kama vile kufanya biashara au kufanya kazi ya kuajiriwa, ni vizuri akishirikiana na mme wake katika maendeleo na matumizi ya nyumbani.
Nakubaliana na wewe. Ni muhimu ingawa huwa inaleta ugomvi endapo mwanaume akihitaji mke ashiriki.
 
Sio hiari ni wajibu. Kitendo cha kuwa na kipato maana yake unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi, na utawajibika kulipia au kuchangia gharama zote za wewe kuishi.
Safi Sana mkuu.
Hawa viumbe sijui pesa zao Wanataka wazifanyie nini.
 
Hahahaha 🤣 kama mmekubaliana ni sawa, pesa zenu mkazitumie kuhonga vijana wenye miguvu ya kiume.
Mimi ni housewife. Nafanya shughuli zote za nyumbani unazozijua wewe yeye jukumu lake ni kusupport financially. Akitaka na mimi nianze kutoa pesa zangu basi akubali na yeye kuosha vyombo. Ipo hivyo.
 
Siyo Sheria ni makubaliano.
Kwa tabia yako unaweza kuwalaza watoto wako njaa kisa bwana wako hana pesa huku wewe ukiwa na pesa.
Siwezinkuwalaza watoto njaa. Ninatoa pale inapobidi. Naelewa kwamba ipo siku anakwama lakini sio jukumu langu ni lake. as long as he is alive akatafute alete..nitatoa kwa siku chache
 
Kama mwanamke anafanya kazi au biashara inayo muingizia kipato ni nirazima kipato chake kichangie maendeleo ya familia tofauti na hapo hiyo kazi na biashara hatoifanya na atakaa nyumbani kulea watoto kama hataki aondoke akaolewe na mwingine.

Mwanamke nikisha muoa ni lazima aende kwenye ndoto zangu sio aje kuwa mshindani wa ndoto zangu.

Alafu ww mwanamke kipato chako ambacho akichangii maendeleo ya familia kwa ajili future ya watoto wenu unakuwa unatafuta kipato cha nini hasa?
Shikilia hapohapo young man. Mnaamka wote asubuhi mnatawanyika kwenye majukumu mnarudi mmechoka. Halafu mwanaume unahudumia kila kitu ikiwemo mwanamke mwenyewe huu unakuwa utumwa.

Hizo pesa atakozosave zitatumika kuvunja ndoa. Akipata pesa aziweke mahitaji ya familia.
 
Na aliyesema Adam utakula Kwa jasho na wewe Eva utazaa Kwa uchungu alimaanisha nini?
Kula Kwa jasho na kuzaa Kwa uchungu halikua jukumu Bali Laana baada ya dhambi!!

Sasa unataka kuniambia Mungu alisubiri baada ya dhambi ndio agawe majukumu!!?!?
Hiyo ni laana wala sio mgawanyo wa majukumu kwenye ndoa!!

Majukumu makuu waliyopewa Adam na Hawa :-

1.zaeni mkaongezeke mkatawale wanyama wote na samaki wa baharini!

2.Muitunze na kuipalilia Bustani iendelee kuzaa matunda!!

JITAHIDI KUYAELEWA MAANDIKO,MUNGU HAKUMUUMBA MWANADAMU ILI AZAE KWA UCHUNGU NA KULA KWA JASHO BALI NI BAADA YA KUTENDA. DHAMBI NDIPO AKAWALAANI NA HIYO LAANA HAIJAWAHI KUWA JUKUMU HATA SIKU MOJA!!

UTAJIRI WA WANA WA MUNGU UPO MIKONONI MWA MATAIFA,IKIWA WATANYENYEKEA NA KUTII UTAJIRI WA MATAIFA UTAKUA WAO KAMA MFALME SULEIMAN ALIVYOKUA TAJIRI BILA JASHO!!!
 
Sio hiari ni wajibu. Kitendo cha kuwa na kipato maana yake unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi, na utawajibika kulipia au kuchangia gharama zote za wewe kuishi.
Hiyo ni mipango yako na mke wako. Mimi wa kwangu anafanya kila kitu. Nasaidia pale inabidi, ni kwa hiari yangu na si lazima. Naweza nikauchuna hata kama pesa ninayo,atapambana atekeleze. Kama ambavyo mimi nafanya shughuli zote za nyumbani na yeye kaweka miguu juu.
 
Mimi ni housewife. Nafanya shughuli zote za nyumbani unazozijua wewe yeye jukumu lake ni kusupport financially. Akitaka na mimi nianze kutoa pesa zangu basi akubali na yeye kuosha vyombo. Ipo hivyo.
Una kipato?
 
Mimi ni housewife. Nafanya shughuli zote za nyumbani unazozijua wewe yeye jukumu lake ni kusupport financially. Akitaka na mimi nianze kutoa pesa zangu basi akubali na yeye kuosha vyombo. Ipo hivyo.
Halafu pesa unazitafuta ukiwa wapi? Na matumizi ya pato lako ni kwenye nini?
 
Siwezinkuwalaza watoto njaa. Ninatoa pale inapobidi. Naelewa kwamba ipo siku anakwama lakini sio jukumu langu ni lake. as long as he is alive akatafute alete..nitatoa kwa siku chache
Pesa unazopata unazifanyia nini.
 
Hiyo ni mipango yako na mke wako. Mimi wa kwangu anafanya kila kitu. Nasaidia pale inabidi, ni kwa hiari yangu na si lazima. Naweza nikauchuna hata kama pesa ninayo,atapambana atekeleze. Kama ambavyo mimi nafanya shughuli zote za nyumbani na yeye kaweka miguu juu.
Maisha yako na mume wako sio muongozo wa jamii. Ukiwa na ajira unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi na utawajibika na gharama zote zinazokuhusu.
 
Wanawake wenye vipato huwa hawana ndoa,bali wengi wao ni ma single mama,mwanamke wajibu wake ni kulea watoto na mwanaume ni kutafuta pesa kwa ajiri ya familia,ukimkuta mwanamke ana majukumu ya kiume katika familia basi hakuna ndoa hapo.
Na bibi yako aliekua analima pamba na migomba plus kukamua maziwa akiuza mazao hayo enzi hizo Hadi akamzaa baba Yako akaja akakuzaa wewe na yeye hakua na ndoa!!?yaani usomi huu na ajira hizi ndio ziwatofautishe na bibi zetu enzi zile!!?

Rudi kwenye misingi mkuu!!Bibi Yako alichunga Hadi ngombe wakati akiwa na baby yako zama zile!!

Mimi nakumbuka Bibi yangu akiuza maziwa na kukamua plus kulima pamba na kufunga robota Hadi mwanza mjini na kuuza na kununua Hadi viatu vya kuchungia vya Babu!!

Wanawake WA Leo wenye ajira wanashindwa nini!!?
 
Nafanyia mambo binafsi ambayo yeye alishindwa kuyatekeleza. Na zingine nanunua mahitaji ya nyumbani hasa ya jikoni.
Hongera kwa kuwa mke nzuri, wewe ndo type ya mwanamke ninayemtaka.

Mungu alinde ndoa yenu.
 
Back
Top Bottom