Kulingana na sh
Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mchango wa mwanamke kifedha ndani ya ndoa. Wengine wanasema ni lazima awe na mchango ili ndoa iwe na usawa, wengine wanaamini kuwa majukumu ya kifedha ni jukumu la mwanaume, huku mwanamke akihusika zaidi na malezi na uangalizi wa familia.
Mimi binafsi naamini kuwa kila mtu ana majukumu yake ndani ya ndoa, na kusaidiana kifedha ni suala la hiari, si wajibu wa lazima kwa mwanamke. Ikiwa mke anafanya kazi na anataka kuchangia, ni sawa, lakini haipaswi kuwa sharti ili kuthibitisha thamani yake kwenye ndoa.
Nimekutana na watu wanaoamini kuwa mwanamke asiyesaidia kifedha ndani ya ndoa ni mzigo kwa mwanaume. Pia, wengine wanasema mwanaume asiyemudu majukumu ya kifamilia pekee hatakiwi kuoa.
Je, mna maoni gani kuhusu hili? Ni wajibu wa mwanamke kuchangia kifedha kwenye ndoa, au ni suala la hiari kulingana na uwezo wake?
Karibuni kwenye mjadala!
Eria iliyopo nchini na taasisi binafsi nyingi zinazotetea haki za binadamu zinampambania sana mwanamke kuwa awe na haki sawa na mwanaume,
Naaminisha hivi
👉Mwanamke anapaswa achangia asilimi sawa ndani ya ndoa kama mwanaume anatoa asilimia 60k ya matumizi mwanamke atoe 50k au 60k ilikuwepo na usawa na kuepuka unyonyaji.
👉Mwanamke anapaswa atafte kazi ya kufanya hata kama n kibarua ili awe na uwezo wa kumudu kununua nguo zake za ndani kama chupi, sindilia, lotion zake cyo kila kitu unamtegemea mume utamfanya mume uchoke haraka hata kupelekea kufa mapema,
👉Swala la kuchukulia eti mke anaangalia familia ni Big no kna wakat mwanaume unakuta mtoto anaumwa lakin mama hajui unaanza kuhangaika kumpeleka hospital, swala la kuangalia familia na la wanandoa wote.
👉 kulingana na maelezo ya point za juu ikitokea wamekosana ndo wagawane mali au kuuza nyumba kwa usawa.
Tofauti na hapo kama mwanamke
hachangii chochote ndani ya ndoa Atakufanye ufe kabla ya wakati, Atatumia nguvu nyingi kutafta pesa, kumnunulia nguo za ndani, lotion, mara akucheat, mara akwambie mtoto cyo wako na atataka muachane mgawane mali ulizotmia nguvu nyingi kuzitafta na ndo utaziona taasisi na madawat ya jinsia ya kikupgia kelele hakika utachanganyikiwa.
Kwa dunia ya sasa kwenye ndoa wote tuchangie, kutafta pesa , Mwanamke asiwe mtu wa kulala na kula na kunya
Hii ni according to me Na wewe njoo na mawazo yako ya ushawishi nawasilisha 🙏