Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Kutunza familia ni suala jumuishi, iweje unajiona unawajibika kwingine kote isipokua hapo kwenye hela tu?
Ww mwanume ni provider mwnaamke anatoa kwa hiari yake. Kwasababu kila moja Ana majukumu yake ila mwanamke anaweza kusaidia endapo mwenzake amekwama
 
Basi hapa hatuongelei familia moja moja tunaongelea kwa ujumla. Katika hali ya kawaida kabisa kitendo cha kuwa na kipato maana yake unaondoka kwenye kundi la watu tegemezi.
Huwezi kuongelea familia kwa ujumla wakati hizo familia zinatofautiana mtazamo na kiuchumi pia.
 
Umezungumza hisia zako sio uhalisia. Nenda kafatilie watangulizi wa ukoo wako waliishije. Tanzania hii zaidi ya 90% walikuwa wakulima na wafugaji na waliishi kwenye hiyo misingi niliyoizungumza.
Mie mwenyewe nimetoka familia kama hiyo ya wakulima Baba anafanya majukumu yake na mama yake kama kawaida, hakuna siku baba analalama sijui kitu gani, kama ni bidhaa alienda kuuza siku akirudi Wana Kaa na mkewe huko wanapanga kila kitu wenyewe, na ufugaji ulikuwepo kama kawaida Kijiji huwezi kosa mbuzi kuku wakutosha kabisa.
 
Huwezi kuongelea familia kwa ujumla wakati hizo familia zinatofautiana mtazamo na kiuchumi pia.
Mtoa mada tayari ameshatoa taswira ya familia anayoiongelea, anaongelea familia ambayo mke na mume wote wa kipato. Katika familia kama iyo mchango wa mwanamke ni wajibu sio hiari
 
Mie mwenyewe nimetoka familia kama hiyo ya wakulima Baba anafanya majukumu yake na mama yake kama kawaida, hakuna siku baba analalama sijui kitu gani, kama ni bidhaa alienda kuuza siku akirudi Wana Kaa na mkewe huko wanapanga kila kitu wenyewe, na ufugaji ulikuwepo kama kawaida Kijiji huwezi kosa mbuzi kuku wakutosha kabisa.
Baba yako na mama yako sio wazee wa zamani soma kuelewa sio kusoma na kujibu.

Nimekurudisha nyuma sana ili uelewe, alafu sasa unambie hivyo walivyoishi baba na mama yako huo utaratibu waliutolea wapi kama watangulizi wao walishiriki kwa pamoja kujenga uchumi wa familia?

Kama umesoma na kuelewa, mtoa mada anazungumzia familia ambayo mke na mume wanaingiza kipato. Sasa mimi na wewe tujiulize familia ya namna hii ikiamua kuungana pamoja kujenga uchumi wa familia itakuwa sawa na familia inayomtegemea mume pekeake??

Huu uchumi binafsi anaoutengeneza mwanamke mwenye kipato nje ya ndoa nikwajili ya nini?? Na ni kwajili ya nani??
 
Ndio sio lazima ni hiari. Hata wasipotaka hakuna kosa lolote. Mwanaume pambana..ndoa umeitaka mwenyewe
Alafu tukiachana unataka mgao wa 50 kwa 50 kwenye mali ambazo sio jukumu lako kuzichangia?
 
Baba yako na mama yako sio wazee wa zamani soma kuelewa sio kusoma na kujibu.

Nimekurudisha nyuma sana ili uelewe, alafu sasa unambie hivyo walivyoishi baba na mama yako huo utaratibu waliutolea wapi kama watangulizi wao walishiriki kwa pamoja kujenga uchumi wa familia?
Embu waache wapumzike mmoja alimzika mwenzie, Kisha mwingine tukamhifadhi sie watoto, na malezi yao tunatembelea humo
 
Yaani mtu na mkewe halafu changu chetu na chako chako.. huo ji upuuzi bora ukae nyumbani tu usubiri cha kupewa huku ukihudumia familia kwa ukaribu.

Na nyumbani sio kazi zote atafanya yeye iwapo nyote ni watafutaji, siku hizi kazi nyingi zinamalizwa na mashine labda muwe mnaishi kijima.
 
Hii ni mojawapo ya fikra za kimasikini, familia ya watu 10 kumtegemea mtu mmoja kwa kilakitu wakati mwenza anaingiza kipato ni upuuzi wa kiwango Cha juu cha mwisho.

Labda niwaulize swali jepesi, huu utaratibu mmeutoa wapi?

Niwakumbushe naona mnataka kujisahaulisha:-

Wazee wetu, mume na mke walishiriki kujenga uchumi wa familia. Kama ni wafugaji mke alishiriki kikamilifu kwenye ufugaji hakuwa mama wa nyumbani, na kwa wakulima mama alishiriki kikamilifu kuhakikisha mji wake una chakula cha kutosha.

Mazao yaliyolimwa na mke ndiyo yalinunua mahitaji mbalimbali ya familia, mifugo iliyosimamiwa na mke ndiyo pesa yake ilinunua mahitaji mbalimbali ya familia.

Kwa zamani kilimo na ufugaji ndizo zilikuwa shughuli za kiuchumi. Wanafamilia wote walishiriki kuhakikisha familia inapata mahitaji yote muhimu.

Sasa huu utaratibu wa uchumi wa familia kujengwa na mwanaume pekeake ninyi mmeutoa wapi??? Huu utaratibu wa pesa ya mwanamke inafanya mambo yake binafsi tena nje ya ndoa mmeutolea wapi?
Hiyo familia ya watu 10 inatokea wapi wakati ndiyo mmetoka kuoana? Mpaka mnafiki watoto 8 hapo mlishanana mpaka sura kutembea mkiongozana kama kaka na dada.

Au unakusanya ndugu au mnaishi kwenu!
 
Back
Top Bottom