Hii ni mojawapo ya fikra za kimasikini, familia ya watu 10 kumtegemea mtu mmoja kwa kilakitu wakati mwenza anaingiza kipato ni upuuzi wa kiwango Cha juu cha mwisho.
Labda niwaulize swali jepesi, huu utaratibu mmeutoa wapi?
Niwakumbushe naona mnataka kujisahaulisha:-
Wazee wetu, mume na mke walishiriki kujenga uchumi wa familia. Kama ni wafugaji mke alishiriki kikamilifu kwenye ufugaji hakuwa mama wa nyumbani, na kwa wakulima mama alishiriki kikamilifu kuhakikisha mji wake una chakula cha kutosha.
Mazao yaliyolimwa na mke ndiyo yalinunua mahitaji mbalimbali ya familia, mifugo iliyosimamiwa na mke ndiyo pesa yake ukinunua mahitaji mbalimbali ya familia.
Kwa zamani kilimo na ufugaji ndizo zilikuwa shughuli za kiuchumi, na wake walishiriki kikamilifu. Tena kwa wakulima mji kukosa chakula haikuwa aibu ya mme ila mke ndiye angeonekana mvivu.
Sasa huu utaratibu wa uchumi wa familia kujengwa na mwanaume pekeake ninyi mmeutoa wapi??? Huu utaratibu wa pesa ya mwanamke inafanya mambo yake binafsi tena nje ya ndoa mmeutolea wapi.