Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Yaani mtu na mkewe halafu changu chetu na chako chako.. huo ji upuuzi bora ukae nyumbani tu usubiri cha kupewa huku ukihudumia familia kwa ukaribu.

Na nyumbani sio kazi zote atafanya yeye iwapo nyote ni watafutaji, siku hizi kazi nyingi zinamalizwa na mashine labda muwe mnaishi kijima.
Kazi zipi zakumalizwa na machine? Kwa bongo hii au nchi nyingine? Hapa hapa mkuranga watu wapo wangapi wanamaliza kazi Kwa machine! Simu zinapotosha sana
 
Kama mnataka wanaume wawajibike zaidi kujenga uchumi wa familia basi wapewe kipaumbele kwenye ajira, vyeo na mishahara.

Kwanini tuwape kipaumbele watu ambao hawawajibiki kujenga uchumi wa familia?? Tunawapa kipaumbele ili iweje?
 
Unaoa mke ili azae na kulea watoto bahati mbaya unatakiwa kuajiri mfanyakazi wa ndani achukue majukumu ya kulea mke akiwa kazini
Bahati mbaya ya pili kazi ya mama haileti feedback financially,ugumu uko hapo
 
Alafu tukiachana unataka mgao wa 50 kwa 50 kwenye mali ambazo sio jukumu lako kuzichangia?
Sheria itaamua. Binafsi naweza ondoka hapa bila hata kijiko.
 
Uhodari mwingi sana kwneye kuelezea hali ilivyokuwa hapo zamani. Ni kwa vile bibi na mama zetu walivumilia sana kunyanyaswa kiuchumi, kila kitu ngoja baba aje. Haufafahamu hili sababu walikuwa hawalalamiki wala kuonesha kwa watoto wao. Lakini walihakikisha binti zao hawapitii waliopitia wao, zaidi wanapofiwa au kutelekezwa na mwanamme, au kipindi mwanamme anafuja mali kwenye jambo lisilo na manufaa kwa familia/watoto. Wamama hawa walibebea 'resentment' juu ya baba zenu, matokeo yake ikawa watoto wanapokuwa wakubwa, masaada mkubwa zaidi anapewa mama au tuseme anakumbukwa zaidi (si tunajionea wenyewe kwenye jamii zetu?) japo baba yupo hai na ndio aliyevuja jasho na damu kuwalea.

Pesa anayopata unaitolea macho ya nini? Kuhudumia familia kifedha narudia ni jukumu la mwanamme. Ukosefu wa wababa wengi wanaoelewa majukumu yao limekuwa jambo la kawaida kwenye jamii ya sasa. matokeo yake tunapata vijana ambao hawaoni umuhimu wa kuhudumia familia zao sababu hawana mfano unaoeleweka wa kiume. Wanaona mama zao walipambana na hivyo wake zao wapambane, hapana kubwa sana

Swali ni dogo tu, nini mchango wako kama mama kwa familia yako, ikiwa kipato chako hakionekani na muda wa familia umeuweka kwenye ajira??

Hayo maelezo yako ya manyanyaso na upendo ni ishu nyingine ya maswala ya kijinsia!! Hatujadili hayo hapa pls!!
 
Kazi ya mwanamke ni kusaidia kujenga familia kiuchumi, kijamii, na kihisia. Hata hivyo, kuchangia fedha sio lazima; kila mmoja anachangia kwa njia yake, na usawa na umoja kwenye familia ni muhimu zaidi kuliko kutegemea michango ya kifedha pekee.
Vema
 
Samahani, lakini siungi mkono mtazamo huu. Nadhani ndoa inapaswa kuwa ni ushirikiano wa pande zote mbili, na kila mmoja akichangia kwa njia yake, iwe ni kifedha, kihemko, au katika malezi ya familia. Kutoa ni hiari, lakini inapaswa kutokana na mapenzi, heshima, na kuelewana, siyo kwa kulazimishwa. Sidhani kama kumwambia mwanamke afanye kazi ili kuchangia kwa lazima ndiyo suluhisho la changamoto yoyote inayojitokeza. Ndoa inahitaji ushirikiano na siyo kutoza au kutoa, bali kuelewana na kusaidiana.

Oh For God Sake!! Hivi wewe unaelewa maana ya kutoka kwenda kutafuta? Simply kwa Wanandoa ni kuchuma kwa ajili ya Familia, whether you want it or not. Wewe umeiweka "HIARI" kwa sababu ya Ubinafsi. Yes, mbinafsi ndio mana unahisi kwa Mwanamke ni hiari. Sio hiari, Sio. Ni lazima Mwanamke atoe, huwezi kuacha nyumba na familia uende kutafuta halafu eti kwenye kutoa iwe hiari. This egocentrism inatokana na ubinafsi, yaani ni sawa Mwanamume aone suala la malezi na makuzi ya mtoto sio lazima eti kwa sababu anawajibikia mama, huu ni ulemavu wa fikra. Badilikeni, dunia ilishabadirika. Hiki sio kizazi cha, Mama akae home, baba akatafute. Ni kizazi cha fursa sawa za uchumi na ujenzi wa familia. Do not be short minded
 
Ni kweli. Mhasibu anashika pesa zilizotoka kwa waziri wa fedha na kuzipangia matumizi
Vipi Kama waziri katika serikali hiyo kipato chake haitoshi kuendesha serikali lakini mhasibu yeye yupo njema?
 
Wanasheria watakuja tusubiri. Ila tu nikutaarifu kwamba mke ana haki ya kukopa au kuuza mali ya mume ili kuhudumia familia..kama tu mume hatimizi majukumu yake.
Kuna miongozo lazima iangaliwe kama hayo majukumu yapo ndani ya uwezo wa mwanaume na mwanamke hawezi kuyamudu. Sio kwamba unaamka tu asubuhi unavhukua hati ya nyumba unaenda kutafuta mteja wa kuinunua. Haiwezekani una kipato cha milioni moja halafu uende kukopa kwa sababu mume hajaacha elfu 10 ya chakula. Hata hao wakopeshaji watakua wajinga labda upige nao dili.
 
Back
Top Bottom