Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Maswala ya nani Kati ya mwanamke na mwanaume anapaswa kuchangia pesa katika familia hayana mpangilio maalumu, hayana kanuni na hayapaswi kabisa kuwekewa kanuni au Sheria kama mnavyotaka.

Binafsi huwa ninakerwa Sana na kauli inayosema "mke akiwa na milioni moja halafu mume ana laki tano familia ina laki tano kwa sababu mwanamke pesa zake anajua atazituamia vipi". Hii kauli ni ya kipuuzi mno, kwangu mimi pesa za mume ni za familia na pesa za mke pia ni za familia.

Nasema hivi kwa sababu siko tayari kuhudumia kiumbe ambacho hakina mchongo wowote zaidi ya kupiga domo. Hata ninyi mnaojaribu kujadiliana kujua nani anapaswa kuchangia acheni mara moja tabia hii, Kila mtu adili na mkewe/mumewe. Kama mtu hataki mke wake asichangie asipotoshe watu wengine humu.

Mke wangu atachangia Sana katika familia labda afiche pesa zake nisizione. Siko tayari kufanya mambo kwa presha ya jamii.

Eti "hamna hela ya mboga" halafu ana hela, NYAMBAFU!!
Al-mukheef Monetary doctor
Umemaliza mkuu.....
 
Mke wa kwanza walishaachana na Mengi na alishapata mgao wake. Mgogoro wa klyn na familia ya mengi ni klyn alitaka yeye na wale watoto wake mapacha wachukue mali zote kwamba wale watoto wakubwa wasipate chochote. Wosia ni kweli ulionyesha klyn kaandikwa kama mmiliki lakini loopholes za kisheria na busara ya majaji ikatumika kutengua ule wosia.


kwa mantiki nafikiri pia unakubaliana na ukweli kwamba wewe ni mmoja ya sampuli za wanawake ambao mmefanya vijana waingie kwenye iyo kampeni ya kukataa ndoa
Vijana watajua wenyewe waingie kwenye ndoa ama wasiingie maamuzi ni ya kwao. Na wakikaa kizembe huko kwenye ndoa watapigwa tu.
 
Nyie ndio mlikuwa na haki sawa
Mna wajibu wa kuitumikia kwa vitendo katika nyanja zote na sio kwenye siasa peke yake
50/50 haitekelezeki hata kwa mwanaume. Wanaume wengi watakataa. Kama ni utafutaji wanawake wameanza kuweza kiasi flani..
Sasa wewe mume wangu nikuage natoka naenda bar na rafiki zangu nirudi nikute umenipikia unaweza?
50/50 inawezekana kwenye mambo kama ajira, elimu na umiliki wa mali. Linapokuja kwenye suala la ndoa mwanaume wa kiafrika hawezi hayo mambo.
 
Vijana watajua wenyewe waingie kwenye ndoa ama wasiingie maamuzi ni ya kwao. Na wakikaa kizembe huko kwenye ndoa watapigwa tu.
Unavyoongea hayo kumbuka circle ya vijana haiishi kwa watu baki tu. Hata wewe mwenyewe ni dada au mzazi/mzazi mtarajiwa wa kijana.
 
Unavyoongea hayo kumbuka circle ya vijana haiishi kwa watu baki tu. Hata wewe mwenyewe ni dada au mzazi/mzazi mtarajiwa wa kijana.
Bahati nzuri nina kaka mdogo wangu mmoja ameshaoa yupo na familia yake kitambo. Sina mtoto wa kiume. Na hata ningekua nae asingekuwa kataa ndoa maana angelelewa vizuri.
 
Hehehe!!!
Mwanamke ana haki ya kutumia hela yake bila kulazimishwa kuitumia kwa ajili ya familia.
Kama ataamua kusaidia kwa hiari basi hiyo ni sadaka na wema wake tu!
Wewe akili huna kabisa. Na sijui kwanini mtu ukiwa mtetezi wa serikali ya ccm mara nyingi akili nazo zinakimbia
 
Sio anavyoona ni sawa, sema anavyoona ni sahihi. Ukisema "sawa" hapa kwa asilimia kubwa umeongozwa na hisia, ukisema "sahihi" hapa umeongozwa na tafakuri ya kimantiki(na huo ndio uanaume)

Ni sawa kwa mwanafamilia kuwa na kipato na asichangie bill za nyumbani, lakini sio sahihi.
Kaka aina hii ya reasoning ni level za akina Socrate!! Naamini atakuwa amekuelewa
 
Hehehe!!!
Mwanamke ana haki ya kutumia hela yake bila kulazimishwa kuitumia kwa ajili ya familia.
Kama ataamua kusaidia kwa hiari basi hiyo ni sadaka na wema wake tu!
Uko sahihi. Hata akihonga vijana wa mjini no complaints.
 
Mwisho wa siku ukitaka ndoa iingie matatizoni gusa pesa ya mwanamke
 
Akifanya 10% ataipresent kama 70% ya mambo hayaendi bila yeye ila kwa mfumo wa malalamiko si mamlaka. Bado utakuwa na sauti ya mwisho kama mwanaume na atakuheshimu.

Akifanya 40% ataingilia mamlaka yako kiasi ila bado atakuheshimu maana 60 si haba. Mtakuwa mnabishana bishana na atakuwa mjuaji.

Akifanya 50% kwake hapo ni kama anafanya yote na wewe upo hapo kulishwa, kaheshima katakuwepo ila usipokuwa ngangari Kiburi kitakuwa 100% na anaweza kukupa maagizo ni nini cha kufanya na maisha yako. Sentensi za ushauri za nyodo mfano" Maisha si mepesi kama unavyoyachukulia, Sipendi mwanaume awe mzembe mzembe n.k " utazoea kuyasikia.

Akifanya above 50% kwake wewe ni sawa na BEKI TATU saa yoyote anakuondoa.
 
Yeah Tena uchumi WA familia unatakiwa uwezeshwe na %75 ya kipato Cha mwanamke sa Jichanganye uoe Jobless
 
Kaka aina hii ya reasoning ni level za akina Socrate!! Naamini atakuwa amekuelewa
Wanawake na logic ni vitu viwili tofauti kabisa. Mtu anataka usawa lakini hataki wajibu unaikuja na huo usawa. Mimi ndio maana hata wadogo zangu naenda nao kwa logic, sio huu ujinga wa usawa wa kijinsia.

Kuna madogo wawili wanasoma chuo, mwaka mmoja na umri wao sawa, mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Ninapowatumia hela za matumizi yule wa kiume namtumia kiasi kikubwa zaidi, kwa sababu najua yule wa kike pesa ypte anaweza kuibana na kumbebesha mzigo boyfriend wake privilege ambayo yule wa kiume hana. Na yule wa kiume nae atabebeshwa bill na girlfriend wake cost ambayo yule kike hawezi kuingia. Kwa logic kama iyo hata siku moja siwezi kutumia kanuni ya usawa ninapowapa hela. Ni lazima dogo wa kiume nimpe kiasi kikubwa zaidi
 
Ndoa na mwanamke msomi au mwenye hela ni Mungu mwenyewe aingilie kati la sivyo inavunjika wakati wowote.
 
Comments ni nyingi sijasoma,. Ila nadhani wachangiaji wengi walikuwa wanaume wakisupport mada
 
Back
Top Bottom