Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

mangatara,

Nakubaliana na mengi uliyowasilisha. Kuzungumzia suala hili halina uhusiano wa mimi kuwa katika ndoa or not. Hata hivyo naongea from experience, na naongea from experience ya wale ambao wapo katika ndoa pia.Ubakaji ndani ya ndoa maana ni hali ya mume au mke kumlazimisha mwenza wake kufanya tendo la ndoa bila ridhaa yake. Hivyo unaweza usikubaliane nalo ila ubakaji ndani ya ndoa upo.

Ni ndoa nyingi ambazo zina matatizo ya tendo la ndoa katika familia. Hasa ndoa ambazo ni za mda mrefu na si ndoa changa. Hamu ya tendo la ndoa la mwanamke na mwanaume ni tofauti. Wakati kwa mwanaume ni rahisi kwa mwanamke ni lazima ajiandae psychologically na kimwili. Na ndiyo hapo ambapo wewe unaeleza kwamba kukiwa na na mapenzi ndani ya nyumba akisha guswa tayari anakuwa na hamu. Watu kuwa ndani ya ndoa haina maana kwamba ndiyo wanapendana, kuna watu hakuna mapenzi (sina maana wana chukiana) lakini ni wenza na hali kuna wale ambao ni wenza na wanapendana.

Nimejibu mada tokana na mleta mada alivyowasiisha, ila si kwamba naunga mkono mwanamke kumnyima unyumba mume wake, sababu aidha atatafuta pa kwenda kufanya au ataishia kumlazimisha na kumbaka. Ila halibadilishi uhalisia kwamba kuna tabia ya waume kumlazimisha mke wake kufanya tendo hilo bila ridhaa ya mke wake (bila kujalisha ni kosa la nani). Haikwepeki tendo al ndoa ni moja ya kitu muhimu kati ya wanandoa (zaidi soma - Tendo la ndoa na umuhimu wake katika ndoa | Fikra Pevu).

Kuna sababu kadhaa zinafanya mwanamke akose hamu ya tendo la ndoa.

1. Kisha wahi hisi, sikia, ona kuwa mume wake ana mwanamke mwingine.
2. Kuzaa mfurulizo na hivyo kulea watoto wake wadogo hivyo kumfanya kuwa na majukumu mengi kama kuwaandaa shule, kuwalisha, usafi nyumbani n.k
3. Mwanamke kuwa na kazi ambayo humchukua masaa mengi (mfano hurudi nyumbani saa 2 usiku na zaidi) huku akiwa tayari ni mama.
4. Kuwa mvivu wa kupindukia. Kuna baadhi tokana na kuongezeka kwa majukumu anashindwa kujipanga. Akiwa mama, mwenye makukumu zaidi akijilaza kitandani hadi saa 3/4 asbuhi kila siku ni vigumu kufanya vitu kwa wakati labda awe na msaidizi.
5. Kuwa mnywaji wa pombe kupita kiasi, inakata hamu ya tendo la ndoa.
6. Kuna wengine uhamisha mapenzi ya baba kwa mtoto na anashindwa kuyagawa. Akili yote kwa mtoto wake na hana habari tena na mume.

Hayo ni baadhi ninayofahamu na vile ninavyofahamu, ingawa bado ningependa mawazo zaidi toka kwako. Ndiyo maana unakuta kwamba wanandoa ambao wanajiweza (uwezo wwa kutimiza majukumu ya msingi ya kifamilia) na kutokuwa na pressure au ugomvi kuhusu pesa wana nafuu kidogo kufananisha na wale ambao wana pressure za kifedha.
 
Last edited by a moderator:
mangatara, Nakubaliana na mengi uliyowasilisha. Kuzungumzia suala hili halina uhusiano wa mimi kuwa katika ndoa or not. Hata hivyo naongea from experience, na naongea from experience ya wale ambao wapo katika ndoa pia.Ubakaji ndani ya ndoa maana ni hali ya mume au mke kumlazimisha mwenza wake kufanya tendo la ndoa bila ridhaa yake. Hivyo unaweza usikubaliane nalo ila ubakaji ndani ya ndoa upo. Ni ndoa nyingi ambazo zina matatizo ya tendo la ndoa katika familia. Hasa ndoa ambazo ni za mda mrefu na si ndoa changa. Hamu ya tendo la ndoa la mwanamke na mwanaume ni tofauti. Wakati kwa mwanaume ni rahisi kwa mwanamke ni lazima ajiandae psychologically na kimwili. Na ndiyo hapo ambapo wewe unaeleza kwamba kukiwa na na mapenzi ndani ya nyumba akisha guswa tayari anakuwa na hamu. Watu kuwa ndani ya ndoa haina maana kwamba ndiyo wanapendana, kuna watu hakuna mapenzi (sina maana wana chukiana) lakini ni wenza na hali kuna wale ambao ni wenza na wanapendana. Nimejibu mada tokana na mleta mada alivyowasiisha, ila si kwamba naunga mkono mwanamke kumnyima unyumba mume wake, sababu aidha atatafuta pa kwenda kufanya au ataishia kumlazimisha na kumbaka. Ila halibadilishi uhalisia kwamba kuna tabia ya waume kumlazimisha mke wake kufanya tendo hilo bila ridhaa ya mke wake (bila kujalisha ni kosa la nani). Haikwepeki tendo al ndoa ni moja ya kitu muhimu kati ya wanandoa (zaidi soma - Tendo la ndoa na umuhimu wake katika ndoa | Fikra Pevu). Kuna sababu kadhaa zinafanya mwanamke akose hamu ya tendo la ndoa. 1. Kisha wahi hisi, sikia, ona kuwa mume wake ana mwanamke mwingine. 2. Kuzaa mfurulizo na hivyo kulea watoto wake wadogo hivyo kumfanya kuwa na majukumu mengi kama kuwaandaa shule, kuwalisha, usafi nyumbani n.k 3. Mwanamke kuwa na kazi ambayo humchukua masaa mengi (mfano hurudi nyumbani saa 2 usiku na zaidi) huku akiwa tayari ni mama. 4. Kuwa mvivu wa kupindukia. Kuna baadhi tokana na kuongezeka kwa majukumu anashindwa kujipanga. Akiwa mama, mwenye makukumu zaidi akijilaza kitandani hadi saa 3/4 asbuhi kila siku ni vigumu kufanya vitu kwa wakati labda awe na msaidizi. 5. Kuwa mnywaji wa pombe kupita kiasi, inakata hamu ya tendo la ndoa. 6. Kuna wengine uhamisha mapenzi ya baba kwa mtoto na anashindwa kuyagawa. Akili yote kwa mtoto wake na hana habari tena na mume. Hayo ni baadhi ninayofahamu na vile ninavyofahamu, ingawa bado ningependa mawazo zaidi toka kwako. Ndiyo maana unakuta kwamba wanandoa ambao wanajiweza (uwezo wwa kutimiza majukumu ya msingi ya kifamilia) na kutokuwa na pressure au ugomvi kuhusu pesa wana nafuu kidogo kufananisha na wale ambao wana pressure za kifedha.
Ashaadii;
Kwanza nianze kwa shukrani kuwa umenielewa vizuri. Pili niseme kuwa, mchango wako hapa ni wa kipekee. Unaonesha muelewa na pia ungeweza kuwasaidia wamama wengine wenye mawazo hata ya kutengana na waume zao. Kila point uliyoitoa inaonesha kuwa kama huyu mwanamke angetulizana kidogo na kusema kuwa yawezekana kuna mama ka yeye mwenye mateso zaidi yake, angeleta ushindi kwa nyumba yake.

Kuna kisa kilitokea, ati mwanamke alikuta mume wake kazaa na jirani yao. Hasira ikampeleka naye kwenda kuzaa na mwanamume mwingine. Kichekesho ni kwamba, alikuwa anamnyima mumewe unyumba, huku anagawa nje, ana miba sasa hivi. Ukimuuliza, una nyumba ya kukaa hana, ati anasema tutabanana hapa hapa. Huu nasema ni ujuha, na anataka kukatisha tu maisha. Hili halikubaliki. Mwanamke kuwa na kazi nyingi kiafrika hili halipo. Ninapompa mtu ushauri huwa namwambia kuwa mwenzio akikutaka hakuna neno baya kama kumwambia; Nimechoka. Hilo ni neno baya kuliko hata tusi.

Choka siku moja moja si kila siku. J3 mpaka j3. Umeona wapi?? Basi lipa kodi yanyumba na kitanda kwani yaonesha umekuja guest house. Sipendi kusema mengi ila wapo wamama husingizia hata ugonjwa. Kinacho wafanya waunguze unyumba wao ni kuwa, yule mume si mjinga, Ugonjwa gani utakuanza mara tuninapokutaka?? Hilo la kuhamishia mapenzi kwa watoto, ndilo linavunja nyumba nyingi zaidi, za muda mrefu au hata nyumba changa tu. Wamama wengine wakiisha kuzaa mtoto wa kiume hujiona bora tena anayestahili kuogopwa. Huku ni kukosa ufahamu tu. Nadhani ndo maana simba huua watoto akiwafuma. Ni kwa sababu simba jike hujali watoto kuliko kitu kingine. Angekuwa hata anakaa kaa karibu na simba dume sidhani kama dume lingewaua watoto. Usiivunje nyumba yako kwa sababu ati umepata mtoto. Kumbuka, umeolewa si kwa sababu mwenzio alihitaji watoto. Alikuhitaji weye. Kuhusu uchafu, wengi huvumiliwa kama anamtimizia mume hayo ya sita kwa sita. Nashukuru kwa mchango wako, endapo wataufuata wengi wataponya nyumba zao
 
Last edited by a moderator:
Unazungumziaje ubakaji ndani ya ndoa? Je mwanandoa anaweza kumbaka mwandani wake??

Kulingana na ibara 130(2)(a) ya kanuni ya adhabu(penal code as amended by SOSPA) Ubakaji ndani ya ndoa hautambiliki isipokuwa tu pale wanandoa wanapotengana (during period of legal separation) kwa misingi mme aweza kumbaka mke wake na haitakuwa kosa mbele ya sheria.

Unalichukuliaje swala hili? Mabadiliko yapi yafanyike ili kulinda wanawake walioolewa?
 
Yafanyike mabadiliko ya sheria ktk kanuni za adhabu na kosa la ubakaji litolewe maana mpya itakayo huisha ubakaji ndani ya ndoa, ama sheria ya ndoa ifanyiwe mabadiliko...
 
Kukubali kuolewa ni sawasawa na kulala bila ch*p*, kama huwezi hilo, inabidi muachane. hiyo ni ndoa gani inayowahitaji kuishi kama dada na kaka?
 
Unazungumziaje ubakaji ndani ya ndoa? Je mwanandoa anaweza kumbaka mwandani wake??

Kulingana na ibara 130(2)(a) ya kanuni ya adhabu(penal code as amended by SOSPA) Ubakaji ndani ya ndoa hautambiliki isipokuwa tu pale wanandoa wanapotengana (during period of legal separation) kwa misingi mme aweza kumbaka mke wake na haitakuwa kosa mbele ya sheria.

Unalichukuliaje swala hili? Mabadiliko yapi yafanyike ili kulinda wanawake walioolewa?
Ulichoandika ni kweli kabisa.

Wabunge wetu[vyama vyote], hivi sasa tunapigana na gender violence na moja ya udhalilishaji mkubwa kwa wake zetu ni hili la kulazimisha tendo la ndoa hata kama mke hataki. Ukweli uliodhahiri ni kwamba hili kosa moja kubwa ambalo linaonekana kama la kawaida.

Hadi sasa ,Ghana, India, Indonesia, Jordan, Lesotho, Nigeria, Oman, Singapore, Sri lanka na Tanzania ndiyo nchi pekee zilizohalalisha kitendo hiki.

Wabunge kina mama, huu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia hili [bila kujali itikadi] hadi hii sheria ya kishenzi iondolewe.
 
Wakati marekebisho yanaendelea hao wanawake wakalale na wazazi wao.

Maana visingizio vitazalisha manundu kwa Ke/Me vichwa emte juu ya mnachojadili.

Ulichoandika ni kweli kabisa.
Wabunge wetu[vyama vyote], hivi sasa tunapigana na gender violence na moja ya udhalilishaji mkubwa kwa wake zetu ni hili la kulazimisha tendo la ndoa hata kama mke hataki. Ukweli uliodhahiri ni kwamba hili kosa moja kubwa ambalo linaonekana kama la kawaida.
Hadi sasa ,Ghana,India,Indonesia,Jordan,Lesotho,Nigeria,Oman,Singapore, Sri lanka na Tanzania ndiyo nchi pekee zilizohalalisha kitendo hiki.
Wabunge kina mama, huu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia hili [bila kujali itikadi] hadi hii sheria ya kishenzi iondolewe.
 
aisee, na je mke akimbaka mme, baada ya legal separation , inakuaje hapo? haitambuliki pia?
Kimsingi na kisheria mwanamke hawezikumbaka mwanaume kwasababu the key element of rape is penile penetration kwa maana kwamba ushahidi wa ubakaji ni pale sehemu za siri za mwanaume zimuigilapo mwanamke. Kwa kukosa sehemu hizo za siri( za kiume) wanawake hawawezi kubaka

Hiii haimaanishi hamna makosa mengine ambayo yanawagusa wanawake ... (mfano sexual violence, sexual intimidation, sexual coercion, sexual harassment etc)

Ki ufupi mwanamke hawezi kubaka kisheria kama nilivyoeleza hapo juu...ila kuna makosa mengine unaweza kumshtaki kama tajwa hapo juu !!
 
Wakati marekebisho yanaendelea hao wanawake wakalale na wazazi wao.

Maana visingizio vitazalisha manundu kwa Ke/Me vichwa emte juu ya mnachojadili.
Nashukuru kwa mchango wako, ila inatupasa kutatua matatizo kwa ustaarabu na hekima hasa hasa inapogusa haki za mwanadamu. Nakusihi kuto toa vipigo wala kuchukua sheria mkononi bali kuanzisha maongezi na kuchukua hatua yakinifu kutatua matatizo ni hapo tuu tutapata maendeleo. Asante.
 
Yafanyike mabadiliko ya sheria ktk kanuni za adhabu na kosa la ubakaji litolewe maana mpya itakayo huisha ubakaji ndani ya ndoa, ama sheria ya ndoa ifanyiwe mabadiliko...
Kwa Mimi mpaka leo naona ni ngumu ku-prove marital rape hata kama sheria inaitambua.utajuaje kama kweli mke amebakwa na mumewe au mke amembaka mumewe kama wakati wanafanya hivo walikuwa wawili tu? Je mhusika akikataa akasema sikubaka utakuwa na ushahidi?
 
Ulichoandika ni kweli kabisa.
Wabunge wetu[vyama vyote], hivi sasa tunapigana na gender violence na moja ya udhalilishaji mkubwa kwa wake zetu ni hili la kulazimisha tendo la ndoa hata kama mke hataki. Ukweli uliodhahiri ni kwamba hili kosa moja kubwa ambalo linaonekana kama la kawaida.
Hadi sasa ,Ghana,India,Indonesia,Jordan,Lesotho,Nigeria,Oman,Singapore, Sri lanka na Tanzania ndiyo nchi pekee zilizohalalisha kitendo hiki.
Wabunge kina mama, huu ndiyo wakati wenu wa kulisimamia hili [bila kujali itikadi] hadi hii sheria ya kishenzi iondolewe.
Nashukuru sana kwa mchango wako, ni kweli usemavyo kuwa sheria hii inabidi iangaliwe upya kama wenzetu walivyofanya ili kulinda haki za wanawake ambazo kimsingi ni haki za kibinadamu. Asante!
 
Kwa Mimi mpaka leo naona ni ngumu ku-prove marital rape hata kama sheria inaitambua.utajuaje kama kweli mke amebakwa na mumewe au mke amembaka mumewe kama wakati wanafanya hivo walikuwa wawili tu? Je mhusika akikataa akasema sikubaka utakuwa na ushahidi?

Nashukuru kwa mchango wako, ila unaposema wapo wawili tuu naomba nikuulize ubakaji wa kawaida watu wanakuwepo?? Kwani ubakaji kawaida hutokea wazi wazi?

Na ushahidi unatokaga wapi katika kesi za ubakaji ambao sio wa ndani ya ndoa? Au watu hubakwa mbele ya jamii?

Ubakaji wowote ule hutokea kwa siri ila ni jukumu la sheria kuwalinda wote wanaokumbwa na jambo hili.
 
Nashukuru kwa mchango wako, ila unaposema wapo wawili tuu naomba nikuulize ubakaji wa kawaida watu wanakuwepo?? Kwani ubakaji kawaida hutokea wazi wazi?? Na ushahidi unatokaga wapi katika kesi za ubakaji ambao sio wa ndani ya ndoa? Au watu hubakwa mbele ya jamii??
Ubakaji wowote ule hutokea kwa siri ila ni jukumu la sheria kuwalinda wote wanaokumbwa na jambo hili.
Me kesi zote za ubakaji huwa naona zina utata ..mfano sheria inasema ni lazima itokee penetration. How can you prove penetration wakati pengine mtu huwa ana-have sex daily? Maybe kwa mtoto mdogo...kitu kingine wanasemaga kuwe na semen labda hii inaweza kuwa proved. Lakini what if mtu amebakwa na hajamwagiwa semen??? Ndiyo maana katika kesi za ubakaji wanashauri mtu akikubaka jaribu kumjeruh ili iwe ushahid au unaweza chukua hata kitu chake kama mkanda wa surual n.k sasa labda hao wanandoa pia wafanye hivo kwa ajili ya ushahidi pia
Sijui nimeeleweka mkuu?
 
Asante ila naomba nikujulishe kuwa kuna vipimo vya kubaini kama kuna penetration. Vilevile penetration is not the only element or evidence of rape kuna circumstantial evidence kuna collaborative evidence na kuna the issue of consent...nnacho taka kusema nikuwa marital rape ipo, inatokea na kuna uwezo wakulibaini kisheria tatizo linakuja pale sheria yenyewe haitambui kabisa jambo hili. Tatizo lingine ni mawazo ya jamii kuwa mwanaume anayo haki juu ya mke wake bila kujali her consent.
Wanasheria na wabunge wakikaa pamoja na wananchi inawezekana kabisa kutengeneza parameters zitakazo ongelea marital rape kwa ufanisi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake!
 
Back
Top Bottom