Je, Mwenyezi Mungu anaweza kutenda hivi?

Jibu ni moja "Jifunze kuongea na Mungu" ukifanikiwa hilo we muulize maswali yako yote atakujibu.
 
Naweza kuongea na mmoja niliyemchagua, atanihakikishia ana uwezo kuliko mwenzake, lkn mwenzake naye akasema ana uwezo kuliko yeye. Sasa hapo unafanyaje? Waelewane kwanza halafu watoe muongozo mmoja kwa watu wao
 
Umenena hakika
 
Hata huyo yesu unayemtaja alivyoleta ujumbe wake wengi walimpinga na kusema kuwa ni mzushi na muongo, endeleeni kumdhihaki mungu ila kila jambo lina mwisho wake na kila kiumbe kitavuna kilichopanda
Hujajibu swali mkuu.. Yesu ni wa dhehebu lipi?
 
Hii miungu ni ya ajabu mno,Imagine mungu anaamrisha watu wenye midevu waliovalia makobazi wajifunge mabomu viunoni wakajilipue ili kuua wengine.Si mda kuna mmoja wetu povu litaanza kummiminika kinywani lakini ndio uhalisia
 
Tunaenda pamoja. Je Madhehebu yote wanaamini wao ni wamoja?
Siyo lazima kuamini hivyo maana kwenye mapokeo na mafundisho utafauti lazima utatokea, ila wote wanaamini uwepo wa mungu, tofauti na wewe na mleta mada mliojawa viburi kisa tu mpo hai na mnavuta pumzi ya bure hadi mnafikia kumdhihaki mungu ,siku yenu haipo mbali, hata farao alikuwa na akili mbovu kama zenu angalia kilichomkuta
Usidanganyike fanya utubu acha ujuaji
 
🔵Narudia tena. Mungu yupo, Dini ni Hadithi. Mungu kwenye Maandiko ni complicated mpaka watu wametengana.

Iko sheria ya Hekima inayokubalika na kila Dini, Falsafa, kabila, kila Tabaka na kila mtu.. Inaitwa;

👉GOLDEN RULE: Watendee wengine sawa na unavyopenda kutendewa wewe.

🟤Kama ni jambo lisilofaa kumtendea mwingine kuna Alarm inakufanya usite kwanza. Hii iko Automatic na hutakiwi kupingana nayo [Hutakiwi kushindana na kitu usichoweza kukibadili}. Wanaoshindana na alert hii huishia kujutia au kupata matokeo yenye maumivu.

🟢Wanaoisikia alert hii na Kujizuia Ni kundi la watu Wenye nguvu nyingi. ambao wanamafanikio makubwa sana Wana uwezo wa kushinda kishawishi chochote, Kutumia pesa vizuri nk. Hii alert inatusaidia kujiepusha na vingi [Tamaa, Upumbavu, Udhalimu nk}


NB: Mungu ametuumba na kutupa vieelelezo vya kutosha ambavyo tukitafakari kwa kina {Meditation} Tunauona uwezo wake like Mfumo wa miili yetu wenyewe, Mimea, Wanyama, Maji, Mvua, Jua, Nyota. Vinatosha kua kielekezo cha kutafakari na kuona nguvu zake na kuthibitisha kua yupo na Kwamba Anaweza kutufanyia chochote akiamua.

🟢 Dini ni matokeo ya fikra za wanadamu. Labda walioanzisha walikua na nia njema lakini wakakosa Hekima ya kumuelezea. Wakapunguza ubora wa Mungu kwenye maandiko: Wakamdhihaki Eti mfano Mungu atachoma moto wanadamu kwa uzembe wake mwenyewe wa kumuumba Shetani.

Binafsi hua nasoma Biblia. Kuna concept zingine ziko safi tu lakini nyingi ziko very complicated.. like Utatu Mtakatifu, Kunena kwa lugha, Siku rasmi ya kuabudu, Ulaji, Uvaaji, Unywaji, Sadaka, Michango, Ndoa, Taraka, Namna ya kusali, Kufunga, Ubatizo, Moto wa milele, Simulizi ya yesu kutoka miaka12 hadi anarudi na kubatizwa akiwa na miaka30 kufichwa na vingine vingi. Vinafanya utengano kimadhehebu.

MUNGU YUPO!! Muamini Tenda mema. Ukimkosea mtu mara moja mteendee wema mara 2,3,4..

Dini ni Fursa ya wahuni kupigia pesa.. Umewahi kujiuliza zile sadaka zinaenda wapi? 😂😂
 
Halafu wanasema ana uwezo wote, anajua yote, yaani anajua mwisho kabla ya mwanzo. Kwa hiyo alijua hata angemkataza vipi Adam kula tunda la mti wa Kati Adam angekula tu. Sasa alimlamu kwanini wakati alijua Huo mtihani hataushinda? Hizi Ni fikra za watu baada ya kukosa majibu ya maswali waliyokuwa wakiulizwa huko Zamani. Hizi hekaya haziingii kwenye akili za watu wanaohoji. Unatakiwa ukubali tu ht km kitu hakina mazntiki ndo uitwe mwenye Imani
.
 
KAMA NA WEWE UPO KWENYE MADHEHEBU YA DINI BASI JUA TU KUWA NA WEWE NDIYO WALE WALE WAPUMBAVU
 
Dini na uwepo wa MUNGU is so complicated tunaishi Kwa Imani tu kuamini . Mfano mwanadamu anaeza asiliamini jambo flani katika maisha au asimwamini mtu flani , je akiwaza dini na uwepo wa MUNGU akawa na mashaka akawa haamini je anakuwa na kosa? Mana MUNGU kamuumba na hisia za uaminifu Yani kuamini au kutokuamini jambo pia kamuumba na maarifa na maarifa hayo hayo ndo mwanadamu kayatumia kufikiria juu ya uwepo aliyemuumba .Note; swala ni kuamini na kutokuamini Wala sio kukaidi mana hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa MUNGU yupo ama hayupo . Ko usiseme flani amekaidi dini sijui anamkufuru MUNGU mana swala ni IMANI ( kuamini au kutokuamini)
 

🤣🤣🤣🤣
 
Kiranga
 
Habari za mwenyezi Mungu ni hadithi za kutungwa na watu tu, kiuhalisia, nje ya hizo hadithi za kutungwa na watu, huyo Mungu hayupo.
 
Umemaliza Bro,Hamna Haja ya kuongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…