Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Issue ni kwamba unawezaje kutoa mahari kwa binti ambaye hujui baba wala ndugu yeyote upande wa baba yake?
 
Uo ndiyo utaratibu wa mahari, hata ukioa unajua umeoa kweli maana unajua ndugu za binti pande zote mbilina zimeshiriki kukupa mke.
 
Tatizo vijana wa siku hizi mnakimbilia usasa mwingi ndiyo maana mnakataa kuoa, mnakataa kuzaa, mnakataa kuwa na familia, mnakubali jinsia moja kuoana. Taratibu zenye misingi imara mnaziita ni za zamani.

Kutoa mahari ni zaidi ya inavyoelezwa maana wewe unatafsiri ya kwamba binti ananunuliwa. Hiyo tafsiri yako siyo kweli na ina upitishwaji mkubwa sana.

Familia ni taasisi kuu na ni ya zamani ikiwa na misingi yake iliyonyooka. Ukiyumba kutekeleza misingi ya kuanzisha familia ujue hutafika mbali, baada ya miezi miwili utaanza kukataa ndoa. Kaa wa wakubwa wakufundishe.
 
Na hapo ndipo Gender Equality inatakiwa.
Haiwezekani kwenye maslahi Mwanamke asipewe kipaombele lakini kwenye majukumu ya kimalezi Watu wanamkimbia. Hiyo sio Haki.
Tatizo ni upande mmoja wa mama kupokea mahari bila upande wa pili wa baba kushiriki.

Unajua umuhimu wa pande zote mbili kushiriki kumuozesha binti?
 
Hapo ndo changamoto ilipo. Nitaoaje binti asiye na ndugu upande wa baba. Je mtoto wetu akija kuleta mchumba ambaye ni ndugu wa mama yake upande wa baba?
 
Lakini huo ndio mfumo wa kale, mfumo wa wazee!

Je tusiamini katika kale?
Ya kale ni dhambi, ndiyo maana generations zinaweza kuendelea. Wanaofuata usasa wamekimbia hata kuzaa, sasa next generation itatoka wapi?
 
Naongezea atafute hela,huwezi ukawa na hela alafu ukataka kufatilia mpaka hela ilikoenda,kama mtoto amelelewa ujombani unachouliza hapa ni nini?
Hela siyo tatizo. Tatizo ni kwanini upande wa pili haujahusika kuozeshwa binti?
 
Tatizo sio vijana, tatizo ni taratibu zisizo na maana, zisizo na faida na zimepitwa na wakati.

Mimi kama kijana ninaekwenda kuanzisha familia na mwenzangu, kutoa mahari kunatusaidia nini kwa mazingira ya sasa????

Kwamba nikitoa mahari ndo utapatikana upendo, furaha na Amani ndani ya nyumba??

Mahari ni biashara iliyowanufaisha watu huko nyuma, ilikuwa ni moja wapo ya vitu vilivyoziingizia familia mali hususani mifugo, vyakula n.k. ni utaratibu uliopitwa na wakati hauna maana tena kwa maisha ya sasa.
 
Mm ni muislamu mahari ni yangu anayepokea ni yoyote yule then napewa mzigo wangu saaafi.
 
Lakini si tumekubaliana wajumbe tena kwa nguvu moja hakuna kuoa single mother
 
Hapa kabinti kamoja tu,kameshatandikwa mimba kanalea saa hii.
Yaani ngoja tu
 

Hii personal attack ni Kwa ajili ya KATAJWA SINGLE MAZA au?

#YNWA
 
Mkuu naona unataka kuoa mpenzi wangu... Mm nikisha makizana nae kuhusu namna ya kumlipia mahari yake sasa wewe naona unaingilia kunichukulia mchumba wangu shauri yako
 
Hapo ndo changamoto ilipo. Nitaoaje binti asiye na ndugu upande wa baba. Je mtoto wetu akija kuleta mchumba ambaye ni ndugu wa mama yake upande wa baba?
Kwa sababu huna akili tunataka kutueleza yatima wanaolelewa kwenye vituo vya Watoto yatima hawana haki ya kuolewa Kwa sababu hawana ndugu?

Wewe ni mpumbavu wa kwanza Kwa sababu hata mpumbavu wa mwisho ana afadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…