Duuuh mbona una hasira sana, tumefika hatua jamii imeacha kabisa misingi ya kiimani na hata Mila na desturi zinatazamwa kwa macho ya makengeza, katika mazingira ya namna hiyo katu hatuwezi kutoboa!
Mtoa mada nimemuelewa na amelenga jambo jema tu ila mnavyomshambulia inaonyesha wazi namna mlivyojaa hasira vifuani mwenu, si desturi zetu kuozesha binti au kijana kuoa kama kuuza au kununua mapapai, kuna taratibu zake na moja ya taratibu ni pamoja na wazazi wa pande zote kufahamiana na kutengeneza undugu Kwa kadri ya taratibu za Kila jamii, baada ya hapo wanandoa wapya wanapaswa baraka za wazazi wao na kuendelea na maisha!
Kwa maelezo ya mtoa mada, baba wa binti ni mpuuzi tu kama walivyo wapuuzi wengine, Kwa kumtelekeza bintiye hata asijue alipo, (amemtwisha mzigo mzito binti yake na itamtesa sehemu kubwa ya maisha yake) japo haiondoi DNA zake kwa huyo mtoto! Hivyo muoaji kuuliza ana maana nzuri mnooo... (Ila ukiangalia kwa jicho la nyama hwezi kuona)
Nawakumbusha watu wenye jazba kama wewe, kwamba biblia takatifu haijabadilika, na maandiko hayabadilishwi na nyakati na kuyafanya yawe yanaendana na "situation" nooo!, tumeamriwa kuwaheshimu baba na mama, ili tupate maisha marefu na heri duniani, hakuna clarification ya aina ya baba au mama wa kumheshimu!
Katika uumbaji Mungu aliumba mtu ke na me, na Kila mmoja alipewa wajibu wake, Kwa namna yoyote iwayo hakuna excuse ya kufanya hayo mambo interchangeably, hakuna! Japo kupitia feminism movements uhalisia huu unafifishwa na tunaacha miongozo ya kiimani na desturi zetu badala yake tunaangalia Mila, tamaduni na desturi za wengine, TUTAFELI SANAAA, that is why ka kadri muda unavyokwenda watoto wengi wa kiume wanaolelewa na mama tu utawaona wakiwa na tabia za kike kike tu, na watu tunaona sawa, mwisho wa siku idadi ya mashoga na wasagaji inaongezeka kwa kuwa uanaume umepuuzwa!